MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Siombei hivyo na sitaki iwe hivyo,lakini lazima Ukweli usemwe unapohitajika kusemwa.
Hivi unatoaje watu waliokua mtaani wakifanya shughuli zao binafsi na kuwateua kua wakurugenzi wa halmashauri au makatibu tawala? Hawa watu hawana uzoefu wowote wa uendeshaji wa shughuli za mifumo ya serikali za mitaa wala utumishi wa umma, unawaachaje maafisa mipango wazoefu na shughuli hizi?
Unawaachaje makatibu tarafa na watendaji wa kata tena wengi wenye elimu nzuri tu? Wapo maafisa kilimo, maafisa mifugo, maafisa elimu, maafisa afya, maafisa utumishi, wahasibu wengine wengi walioitumikia serikali kwa muda mrefu wakiwa viongozi wa juu katika serikali za mitaa na administrative structure ya serikali ni wazoefu nayo. Tena wengine ni wazoefu na ni wajumbe katika kamati mbali mbali za mipango ya maendeleo ya wilaya na tena wengine ni washiriki wazuri wa vikao na madiwani Katika kupanga mipango hiyo.
Kiongozi kama karibu taarifa au mtendaji wa kata ni watu wazoefu kwelikweli kwenye vikao vingi ndani ya halmashauri, kama mtu ana elimu ya kutosha kuna ugumu gani kumpandisha hadhi kuwa Mkurugenzi au katibu tawala wa halmashauri? Atakutia hasara gani sasa hapo? Ndio maana migogoro ya wakulima na wafugaji haiishi maeneo mbali mbali kwa sababu ya baadhi ya viongozi kukosa weledi katika uendeshaji wa serikali za mitaa kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi za chini kuitatua.
Haya mimi ninayaona awamu hii tu mengine labda yalifanywa na mwalimu Nyerere enzi za chama kimoja maana hakuwa na namna na pia kulikua na idadi ndogo ya wasomi.
Bado narudia kusema there is something going wrong, tutaota viwanda miaka na miaka lakini hatutakaa tusonge mbele tutabaki hivi hivi tu. Huu utaratibu wa sasa kuwapata viongozi hawa sio mzuri kabisa! Kama kuna mtu anafikiria kua hivi vyeo havina majukumu ni kujidanganya tu, ni suala la muda tu tutaona baadhi wakitenguliwa huku wengine wakikimbia ofisi wenyewe.
Hatujafikiria kabisa hasara ya gharama itakayopata serikali kumwandaa na mfunda kiongozi mpya mpaka azoee mazingira ya utumishi wa umma na kipimo cha gharama zitakazotumika kumwandaa kiongozi uzoefu! Gharama ya muda ni muhimu na kubwa sana kuliko zote hasa kwa muda huu ambao tunasema "hapa kazi tu", utendaji wa mtu ambaye hajawahi kukalia kiti cha Ofisi ya umma ni tofauti na mtu ambaye ni mzoefu wa siku nyingi katika utumishi wa umma.
Sipigi kelele bure tu humu lakini kama mdau kuna kitu mbeleni naona hakitakua sawa kabisa. Tunaweza kukwama vibaya sana.