Kwa mtindo huu tuna safari ndefu sana kwenye elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mtindo huu tuna safari ndefu sana kwenye elimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENGETI, Feb 17, 2012.

 1. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  waheshimiwa wana JF.
  kwa heshima kabisa nashuka hapa jukwaani nikiamini kuwa wote mliopo humu ni the greatest thinkers na JF ni Greatest thinker tank. Baada ya matokea ya Darasa la saba 2011 na ya kidato cha nne 2011 kutoka ni wazi kuwa tuna debate kubwa kuhusu kufeli kwa watoto wetu na wadogo zetu.
  sasa naomba nikupeni kituko ambacho si kuwa kinasikitisha tu bali ni janga kuu tunalotengeneza kwa siku za usoni ingawa tayari limeshaanza kujitokeza kwa moshi ambao umeanza kufukuta dhidi ya ajira kwa vijana wengi na pia kupuuzwa kwa watumishi/wataalam wazalendo na viongozi wetu (mgomo wa madaktari kama mfano mmoja)
  baada tu ya matokeo ya darasa la saba kutangazwa Waziri wa Elimu Bw. Philipo mulugo alisema kuwa wale wote wanaotajwa kuwa wamefaulu wata face qualifying exam ili kujua ukweli kuwa wamefaulu au wamefaulishwa. Mtihani ulifanyika nadhani kati tarehe 16 january na february 10, 2012
  matokeo kwa baadhi ya shule za hapa Mwanga mkoa wa kilimanjaro ambayo imefutiwa matokeo ya watoto wa STD VII 350 ni kama ifuatavyo kwa shule ambazo nipo karibu nazo ingawa hali ni mbaya
  1. Vudoi Secondary kati ya watoto 180 wa kidato cha kwanza watoto 28 walibainika hawajui kusoma na kuandika!
  2. Kifaru idadi hiyo hiyo waliobainika kutojua kusoma 16!
  Naendelea kukusanya matokeo ya shule nyingine nitawajulisha.
  Lakini Mkuu wa Wilaya Athumani Hassani Mdoe Taarishi namba moja. anawapongeza walimu wa S/M zote za wilaya kwa ufaulu bila kuangalia tatizo la hao waliofaulu na hawajui kusoma na kuandika!
  Imagine shule za kata No Walimu, No Maabara,No mazingira mazuri ya mtoto kusoma na mwalimu kufundisha, tunaumba object gani kwenye hili
  Tazama barua ya Mkuu wa Wilaya ya kuwapongeza eti wandelee kwa nguvu na kasi zaidi ya kufyatua mambumbu wao wako nyuma yao
  nawasilisha kwa maoni zaidi ambaye wilaya yake ina ujinga huu atuwekee hapa.
   

  Attached Files:

 2. m

  massau Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli kaka hali inatisha coz wanafunz wengi form4 wanafeli kutokana na mssingi mbovu waliotoka na primary,ukizingatia na shule za kata zilivyo tafta hizo habari ili na ss wana jf tuzipate
   
 3. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama watanzania wote wakiwa waelewa ni nani atakaedanganyika na tshirt za magamba?
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli miaka 20 ijayo Tz itakuwa ya mambumbu na wajinga ambayo iliyoandaliwa na serikali ya leo
   
 5. S

  Sanchez Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi nilikutana na mwanafunzi wa form 3 shule moja handeni Tanga, kwenye maojiano nae aliniambia shule yao ina walimu 2 tu.sasa hapo tunategemea kupata nini baadae kama siyo malaya na majambazi?Tafakari...............chukua hatua.
   
 6. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuwa sirias kidogo kuna wadogo zako wapo shuleni jamaa yangu. kama wewe upo matawi hao wadogo zako watayanyausha upo mkuu
   
 7. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni CCM!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  A time bomb in the making.............serikali inataka kuwalazimisha vijana wajisikie wamesoma, kumbe ni 8 X 8 - 64.

  kuna a combination of factors:

  1) Walimu wachache sana
  2) Vitabu vya kiada na ziada ndo kabisaa usiseme
  3) teaching aids ndo anasa siku hizi.........Hii ni sikirini, inakuwa ya kibuluu....
  4) Wanafunzi wasio na sifa wanachaguliwa kwenda sekondari (kumbuka shule za kata zimeshajengwa, na zinahitaji binadamu wa kujaza shule hizo.

  5) mnajua mgomo mbaya kuliko yote duaniani ni upi?...................tupeane 5yrs, mtaona maajabu Tanzania.
   
 9. MBURE JASHA

  MBURE JASHA JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo kwenye red nadhani mgomo wa dizaini hiyo wenye effect baada ya muda ni Mgomo wa walimu na si miaka mitano tu ni Kila baada ya miaka saba mgomo unajibu. tayari walimu waneshagoma hao. tushapata intake zaidi ya mbili au tatu hivi tangu walimu waanze mgomo na mgomo bado uanendelea. Mtoto anaanza kukutana na mgomo wa mwalimu tangu STD 1 akifika STD VIII kwishney ndio hao wasiojua kkk.


   
 10. comson

  comson JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  sema malaya na wezi wenye uelewa....... Tanzania yetu inaharibiwa na watu wachache kama hawa....
   
 11. comson

  comson JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  imetoka kwenye zama za kufaulu na kutochaguliwa mpaka zama za kufeli na kuchaguliwa............. halafu wapumbavu wachache wanaita haya ni maendeleo wakati watoto zao wanaenda shule nzuri na bado wanafeli..............................
   
 12. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Huyo dc lazima alikuwa maekunywa chimpumu kabla ya kuandika hiyo barua ya pongezi
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,111
  Trophy Points: 280
  Mtengeti,

  ..hii habari niliisoma nikasikitika sana ila sikupata muda wa kuileta hapa JF ijadiliwe. nakushukuru kwa kuileta hapa JF ijadiliwe.

  ..kwa kweli sielewi kwanini Wabunge na Wanaharakati hawa-demand a change in our education system. Kwa kweli taifa linajumiwa na kupigwa vita mbele ya macho yetu. Hakuna njia ya uhakika ya kuangamiza taifa lolote lile zaidi ya kustawisha UJINGA na CHUKI miongoni mwa wananchi wake, and that is exactly what is happening in Tanzania.

  ..Halafu kitimbi hicho kimetokea kwenye jimbo la aliyekuwa Waziri wa Elimu, Professor Jumanne Maghembe?!! Hivi majimbo mengine yana hali gani??

  ..Zaidi, Naibu Waziri wa Elimu kutamka kwamba wanafunzi watapewa "entrance exam" ktk shule za sekondari ni kuonyesha kwamba Wizara haina imani na matokeo ya mtihani wa taifa ya darasa la 7. Now, how did we get there??

  ..Lakini kana kwamba kashfa matokeo ya mitihani ya darasa la 7 na kidato cha 4 haitoshi, kuna habari kwamba Wizara ya Elimu/Serikali ina mpango wa kupeleka mswada wa bungeni ili kupitisha sheria ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia toka shule ya msingi mpaka sekondari.

  ..kwa maana nyingine watoto wa walalahoi wafundishwe Kiswahili, wakati huohuo watoto wa wakubwa/vigogo wafundishwe Kingereza kwenye ma-academy. This is the same thing they did wakati wa mpango wa UPE. Watoto wa walalahoi walilundikwa kwenye shule za serikali, halafu viongozi wakawa wanapeleka watoto wao kusoma Kenya.
   
 14. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijaona tatizo la mkuu huyo wa wilaya,
  Always waheshimiwa wanaongea na takwimu, ikiwa wilaya imekuwa ya kwanza na waliotoa taarifa hiyo ni mamlaka ya elimu inayotambulika kwa nini mkuu wa wilaya asiwapongeze walimu na wadau wa elimu ya msingi wa wilayani?
   
 15. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo tuendelee kuwa wapuuzi kwa sababu kuna wagawa tshirt?
   
Loading...