Kwa msioelewa movie ya Binti, someni hapa

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
Nimeitazama muvi ya Binti, niseme tu ni moja ya filamu nzuri sana ya Kitanzania ambayo inapaswa kutazwa na kila Mtanzania, unajua kwa nini? Ni kwa sababu inaonyesha mapito ya mabinti wanne tofauti.

Muvi hii imegawanyika sehemu nne. Nitakwenda kuzizungumzia sehemu hizo nne, kuwa makini na mimi twende sawa.

BINTI WA KWANZA:

Hapa kuna binti anaitwa Tumaini, huyu ni muhangaikaji, haamini kwenye mahusiano, anachokiamini ni kufikia ndoto zake kwa kupambana tu.

Scene ya kwanza inamuonyesha akiamka kitandani. Ukutani kuna picha ya Mo Dewji! Kumbuka jamaa ni bilionea, Tumaini amebandika picha hiyo ukutani kama njia moja ya kumkumbusha kwamba anatakiwa kupambana, asilalelale kama amekufa.

Binti huyu akiamka asubuhi, kitu cha kwanza ni kuchukua mayai na kuyasambaza, anapomaliza hapo, anakaanga chapati na kwenda kwenye mini supermarket na kuuza. Huyu akili yake siku zote inafikiria kuhusu kufanikiwa tu.

Na kama umeiangalia, pale kazini kwake, yaani Supermarket alikuwa na kitabu cha Reginard Mengi kinachohusu safari yake ya mafanikio, hayo yote tunaonyeshwa ili kujua ni kitu gani alichokuwanacho Tumaini. Si Binti anayemtegemea mwanaume, ni binti anayeamini kufanikiwa ni kupambana tu.

BINTI WA PILI:

Binti wa pili anaitwa Angel. Huyu ni aina ya mabinti wale wanaojiita slay queen. Anahusudu pesa kuliko kitu chochote kile. Alikutana na mwanaume, wakapendana lakini mahusiano yalikuwa ya mateso sana ila hakutaka kuondoka.

Hii huwatokea mabinti wengi, wanateseka kwenye mahusiano ila hawataki kutoka kwa kuwa jamaa ana pesa, akiondoka, atapata vipi pesa? Aliweza kuishi na jamaa mpaka akapata ujauzito.

Alipoona mambo yamemfikia puani, akaamua kuondoka, na mimba akatoa. Angel ametupa somo zuri tu kwamba mabinti hawatakiwi kung’ang’ania kwenye mahusiano ya kikatili kisa pesa.

Wakati Tumaini akipambania maisha yake, Angel alitaka kuyafikia maisha aliyokuwa akiyataka kwa kupitia njia ya mkato, mwisho wa siku aliambulia mateso ya kupigwa kila siku na kukaripiwa.

BINTI WA TATU:

Huyu ni Stela. Ni binti anayeishi na mume wake. Ana kila kitu, maisha mazuri, kazi nzuri, kila alichokuwa akikitaka, alikipata isipokuwa kitu kimoja tu. Mtoto.

Hakuwa na mtoto, na kila alipopata mimba, ilitoka. Hilo lilimtesa sana, alitembelea hospitalini kama sokoni, alikwenda huko kila siku kuona tatizo ni nini.

Huyu ametupa somo kubwa, kwamba unaweza kupata kila kitu ila bado ukawa haupo sawa. Wakati anakutana na Binti wa pili, Angel, msichana huyo alimuona mwenzake yupo kwenye mahusiano mazuri, maisha ya furaha, hakujua ni kwa namna gani suala la mtoto lilikuwa linamuumiza.

Stela alikwenda hospitalini, holaa! Akaenda kanisani kuombewa, holaa! Mpaka mwisho wa siku akapata wazo la kwenda kwa mganga, alifanya yote haya kwa kuwa alihitaji mtoto tu.

Hapa tunapewa somo kubwa kwamba usitamani maisha ya fulani, hujui ni matatizo ya aina gani anapitia. Angel alitoa mimba kwa kuwa mwanaume alikuwa mkorofi, ila mwenzake, Stela alikuwa anatafuta mtoto. Inashangaza!

BINTI WA NNE:

Hapa tunakuna na Rose. Huyu yupo kwenye ndoa. Anafanya kazi nzuri, na mume wake pia anafanya kazi nzuri tu. Tatizo kubwa alilokuwanalo ni kutokupata ushirikiano kutoka kwa mumewe.

Mwanaume hajali kuhusu mtoto wake, yaani aliamini kazi ya malezi ni ya mwanamke tu, mbaya zaidi, mtoto wao mmoja aliyeitwa Chris alikuwa mgonjwa, hivyo mwanamke alikuwa akihangaika mno lakini mumewe walaaaa.

HITIMISHO.

Tumaini alitaka maisha mazuri, akahangaika, akakutana na Angel ambaye alikuwa akiishi maisha aliyoyatamani Tumaini pasipo kujua binti huyo alikuwa akipitia matatizo gani.

Mara baada ya Angel kumuona Stela na jamaa yake, alitamani sana kama ingetokea yeye na mpenzi wake kuwa namna ile, walionekana kupendana mno, hakujua ni matatizo gani wawili hao walikuwa wakipitia ndani ya nyumba.

Baada ya Stela kumuona Rose akiwa na mtoto wake, alitamani sana na yeye apate mtoto kama ilivyokuwa kwa rafiki yake huyo bila kujua ni matatizo gani alikuwa akipitia na mume wake ndani ya ndoa.

Kwa kifupi ni kwamba muvi nzima imetufundisha kutokutamani maisha ya mtu mwingine. Kila mtu ana changamoto zake, inawezekana unayetamani maisha yake anapitia matatizo makubwa kuliko wewe.

Nampongeza Seko Shamte kwa kuandaa kitu kizuri. Hongera sana wewe na timu yako.

Imeandikwa na Nyemo Chilongani
 
Hiyo Binti ni mbovu. Haileweki kama ni documentary au ni filamu. Haina muendelezo wa visa, character wala story ni ya hovyo na kama ni hivi basi itafika kipindi filamu za Kiswahili hazitopata watazamaji Netflix

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kama kisa kipi hakikuwa na muendelezo?
 
hii muvi ni kali mpaka wanaija wameitupiia kwenye website zao ila taratibu wataielewa
 
Kama movie za kiswahili ndio zitakuwa hvyo basi itanisaidia kuhifadhi bando langu....kuacha vipande vipande vinavyoishia katkat sio sawa,story nzuri ila inaacha ujimalizie mwenyewe.Sidhan km hyo ni movie nadhan ni documentary maybe au kitu kingne uko.
 
Chilojnr & DENLSON fanyeni kuitazama BINTI upya ili muweze kupata correct interpretation of the film.
Screenshot_20220117-192751_WhatsApp.jpg
 
Naam uchambuzi mzuri japo sijaiona ila nshpata picha ni film Kali sana nazani ntatenga muda wa kuitazama thoo mimi sio shabiki wa muvi za bongo...
 
Sasa iyo binti inatofauti na story za bongo muvi za kila siku. Nilitamani kuitazama ila kwa Maelezo yako hapa ni mbaya na haifai kutazamika
 
Nimeitazama muvi ya Binti, niseme tu ni moja ya filamu nzuri sana ya Kitanzania ambayo inapaswa kutazwa na kila Mtanzania, unajua kwa nini? Ni kwa sababu inaonyesha mapito ya mabinti wanne tofauti.

Muvi hii imegawanyika sehemu nne. Nitakwenda kuzizungumzia sehemu hizo nne, kuwa makini na mimi twende sawa.

BINTI WA KWANZA:

Hapa kuna binti anaitwa Tumaini, huyu ni muhangaikaji, haamini kwenye mahusiano, anachokiamini ni kufikia ndoto zake kwa kupambana tu.

Scene ya kwanza inamuonyesha akiamka kitandani. Ukutani kuna picha ya Mo Dewji! Kumbuka jamaa ni bilionea, Tumaini amebandika picha hiyo ukutani kama njia moja ya kumkumbusha kwamba anatakiwa kupambana, asilalelale kama amekufa.

Binti huyu akiamka asubuhi, kitu cha kwanza ni kuchukua mayai na kuyasambaza, anapomaliza hapo, anakaanga chapati na kwenda kwenye mini supermarket na kuuza. Huyu akili yake siku zote inafikiria kuhusu kufanikiwa tu.

Na kama umeiangalia, pale kazini kwake, yaani Supermarket alikuwa na kitabu cha Reginard Mengi kinachohusu safari yake ya mafanikio, hayo yote tunaonyeshwa ili kujua ni kitu gani alichokuwanacho Tumaini. Si Binti anayemtegemea mwanaume, ni binti anayeamini kufanikiwa ni kupambana tu.

BINTI WA PILI:

Binti wa pili anaitwa Angel. Huyu ni aina ya mabinti wale wanaojiita slay queen. Anahusudu pesa kuliko kitu chochote kile. Alikutana na mwanaume, wakapendana lakini mahusiano yalikuwa ya mateso sana ila hakutaka kuondoka.

Hii huwatokea mabinti wengi, wanateseka kwenye mahusiano ila hawataki kutoka kwa kuwa jamaa ana pesa, akiondoka, atapata vipi pesa? Aliweza kuishi na jamaa mpaka akapata ujauzito.

Alipoona mambo yamemfikia puani, akaamua kuondoka, na mimba akatoa. Angel ametupa somo zuri tu kwamba mabinti hawatakiwi kung’ang’ania kwenye mahusiano ya kikatili kisa pesa.

Wakati Tumaini akipambania maisha yake, Angel alitaka kuyafikia maisha aliyokuwa akiyataka kwa kupitia njia ya mkato, mwisho wa siku aliambulia mateso ya kupigwa kila siku na kukaripiwa.

BINTI WA TATU:

Huyu ni Stela. Ni binti anayeishi na mume wake. Ana kila kitu, maisha mazuri, kazi nzuri, kila alichokuwa akikitaka, alikipata isipokuwa kitu kimoja tu. Mtoto.

Hakuwa na mtoto, na kila alipopata mimba, ilitoka. Hilo lilimtesa sana, alitembelea hospitalini kama sokoni, alikwenda huko kila siku kuona tatizo ni nini.

Huyu ametupa somo kubwa, kwamba unaweza kupata kila kitu ila bado ukawa haupo sawa. Wakati anakutana na Binti wa pili, Angel, msichana huyo alimuona mwenzake yupo kwenye mahusiano mazuri, maisha ya furaha, hakujua ni kwa namna gani suala la mtoto lilikuwa linamuumiza.

Stela alikwenda hospitalini, holaa! Akaenda kanisani kuombewa, holaa! Mpaka mwisho wa siku akapata wazo la kwenda kwa mganga, alifanya yote haya kwa kuwa alihitaji mtoto tu.

Hapa tunapewa somo kubwa kwamba usitamani maisha ya fulani, hujui ni matatizo ya aina gani anapitia. Angel alitoa mimba kwa kuwa mwanaume alikuwa mkorofi, ila mwenzake, Stela alikuwa anatafuta mtoto. Inashangaza!

BINTI WA NNE:

Hapa tunakuna na Rose. Huyu yupo kwenye ndoa. Anafanya kazi nzuri, na mume wake pia anafanya kazi nzuri tu. Tatizo kubwa alilokuwanalo ni kutokupata ushirikiano kutoka kwa mumewe.

Mwanaume hajali kuhusu mtoto wake, yaani aliamini kazi ya malezi ni ya mwanamke tu, mbaya zaidi, mtoto wao mmoja aliyeitwa Chris alikuwa mgonjwa, hivyo mwanamke alikuwa akihangaika mno lakini mumewe walaaaa.

HITIMISHO.

Tumaini alitaka maisha mazuri, akahangaika, akakutana na Angel ambaye alikuwa akiishi maisha aliyoyatamani Tumaini pasipo kujua binti huyo alikuwa akipitia matatizo gani.

Mara baada ya Angel kumuona Stela na jamaa yake, alitamani sana kama ingetokea yeye na mpenzi wake kuwa namna ile, walionekana kupendana mno, hakujua ni matatizo gani wawili hao walikuwa wakipitia ndani ya nyumba.

Baada ya Stela kumuona Rose akiwa na mtoto wake, alitamani sana na yeye apate mtoto kama ilivyokuwa kwa rafiki yake huyo bila kujua ni matatizo gani alikuwa akipitia na mume wake ndani ya ndoa.

Kwa kifupi ni kwamba muvi nzima imetufundisha kutokutamani maisha ya mtu mwingine. Kila mtu ana changamoto zake, inawezekana unayetamani maisha yake anapitia matatizo makubwa kuliko wewe.

Nampongeza Seko Shamte kwa kuandaa kitu kizuri. Hongera sana wewe na timu yako.

Imeandikwa na Nyemo Chilongani
Umethibitisha ubovu wa filamu yenyewe.
Filamu inatakiwa ijielezee yenyewe na siyo kwa kuelezewa kwa thread au gazeti.
Hiyo filamu mtunzi alitaka watazamaji tuwe tunawaza kama alivyokuwa anawaza na sio kuelewa tunachoona.
 
Kwa kweli filamu ipo kama documentary story zake haziishi, kwa mfano story ya binti wa kwanza story yake imeishia hapo alipokutana na rafiki yake haieleweki kama alifanikiwa ndoto zake au vipi. Na hata hao mabinti wengine ni hivyo hivyo na pia mi nimeona ni mpangilio mbovu kuangalia kisa kimoja mpaka kinaponza kingine wakati unaangalia unakuwa unasubiri labda utaletewa muendelezo wa story iliyopita kumbe ndo imeisha hiyo hutarudishwa nyuma tena
 
Back
Top Bottom