Kwa mshahara huu utatoboa lini?

Kwa mshahara huu utatoboa lini?

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,851
View attachment 1136786
Huo hapo ni mshahara wa mwalimu mwenye degree, kakaa darasani miaka mingi lakini anaishia kulipwa kiasi hicho sawa na Tsh 15000/= kwa siku.

Kwa mshahara huo ulipie nyumba, umeme na maji, mshahara huo utoe mahitaji ya familia, usaidie ndugu kule kijijini, ni kiasi gani utatunza kwa ajili ya maendeleo?

Hivi kwa mshahara huu unaweza kutunza mpaka ujenge nyumba ya kawaida tu ya milioni 30, unaweza kutunza na kununua kagari kweli?

Na hapo utakuta mtu anajisifu kabisa mimi ni mwalimu.
 
Mkuu mbona mshahara mnono huo....wazazi wetu walikuwa wanalipwa chini ya hapo,walijenga wakatusomesha.

Nadhani hapo ndo mahali pa kuweka vipaombele,jambo gani liaze.

Na kuishi maisha ya kawaida si kushindana hakika unatoboa
 
Ukiwa Mwalimu tafuta kazi nyingine,muibie mwajiri muda uweze kufanya harakati zako za kuingiza pesa la sivyo kwa salary hiyo maisha mazuri utayaona Insta mpaka unastaafu..
 
15000 kwa siku ndogo?

Hizo bili za umeme na maji unalipa kila siku?
 
HELSB Unadaiwa million 100 au inamaamisha nni hapo?
 
Akistafu anachukia pesa zake anazotunziwa acha kupotosha wutu
 
Kwanini mwalimu wanamyanyasa hivi?

Mwanasiasa darasa la saba yupo bungeni
Kila siku posho 300k. Na mwisho wa mwezi
12million kibindoni anakunja.
 
hakuna haki tanzania kazi kubwa mshahara kiduchu halafu hapo utegemee ufanisi tunajidanganya mishahara ni lazima iongezwe iendanane na hali halisi ya uchumi
 
heslb wanakudai 109m mkuu,au macho yangu mabovu?
 
Mkuu mahali unapoishi walimu wote wamepanga? Hakuna mwalimu mwenye maisha mazuri?

Pengine unazungumzia walimu zubaifu ila ualimu ni kazi ambayo mtu unaweza kufanikiwa mapema sana.

Mimi ni Mwalimu natamani ungenitembelea.

Unatakiwa kujibana mwanzo ili kutafuta mtaji, ukishapata tu hata 1m hapo tayari umetoboa.

Tatizo wengi mnaishi kwa kutegemea salary, inatakiwa salary ikupe mtaji then fungua magoli tofauti iwe kilimo, ufugaji, uvuvi, duka, genge, mgahawa, mitumba etc.

Watu wengi wanataka wakiajiriwa tu wawe na maisha mazuri, hawataki kujibana kutengeneza kesho yao.

Huo mshahara ni mkubwa sana.

Pale UDSM kuna watu wanafanya kazi ya usafi wanalipwa below 150,000, nyumbani wanafamilia, wamepanga, wanalipa bills za maji, umeme nk ila wanaishi na wengine wamejenga lakini sababu ni kuwa wamejibana na kuplan vizuri. Huwezi kuwa unapokea Sh. 200,000 alafu unatumia 200,000. Au unapokea Sh. 100,000 alafu unaishi nyumba yenye kpdi ya Sh. 60,000 huo ni upumbavu.

Ishi hata nyumba isiyo na sakafu wala umeme wakati unajipanga kutafuta mtaji. Ukidhani degree yako inathamani sana basi endelea kula bata na kulalamika mshahara mdogo....
 
Pesa nyingi sana hiyo,mimi mwenyewe niko kwenye mchakato wa ujenzi wa nyumba kwa kutumia salary savings kama huo na mia mia za goli natumia kwa matumizi ya kawaida
 
Mkuu mahali unapoishi walimu wote wamepanga? Hakuna mwalimu mwenye maisha mazuri?

Pengine unazungumzia walimu zubaifu ila ualimu ni kazi ambayo mtu unaweza kufanikiwa mapema sana.

Mimi ni Mwalimu natamani ungenitembelea.

Unatakiwa kujibana mwanzo ili kutafuta mtaji, ukishapata tu hata 1m hapo tayari umetoboa.

Tatizo wengi mnaishi kwa kutegemea salary, inatakiwa salary ikupe mtaji then fungua magoli tofauti iwe kilimo, ufugaji, uvuvi, duka, genge, mgahawa, mitumba etc.

Watu wengi wanataka wakiajiriwa tu wawe na maisha mazuri, hawataki kujibana kutengeneza kesho yao.

Huo mshahara ni mkubwa sana.

Pale UDSM kuna watu wanafanya kazi ya usafi wanalipwa below 150,000, nyumbani wanafamilia, wamepanga, wanalipa bills za maji, umeme nk ila wanaishi na wengine wamejenga lakini sababu ni kuwa wamejibana na kuplan vizuri. Huwezi kuwa unapokea Sh. 200,000 alafu unatumia 200,000. Au unapokea Sh. 100,000 alafu unaishi nyumba yenye kpdi ya Sh. 60,000 huo ni upumbavu.

Ishi hata nyumba isiyo na sakafu wala umeme wakati unajipanga kutafuta mtaji. Ukidhani degree yako inathamani sana basi endelea kula bata na kulalamika mshahara mdogo....
Kwaiyo walimu wanavyolalama hawalipwi vizuri, maisha yao sio mazuri; kumbe ni janja janja. mabeberu hapa watakuwa wanahusika.

Asante mwalimu kwa kutupa mrejesho
Walimu oyeeee, maghufuli oyeeeeee
 
Kiranja Mkuu alikuwa mwalimu, mke wa kiranja mkuu ni mwalimu, Waziri mkuu alikuwa mwalimu....huko kwetu kuna msemo "mambo mawili ambayo binadamu huyasahau kwa haraka ni umaskini na utasa"
Nimecheka kama mazuri, na huo mkopo wa wa elimu ya juu a
Untitled.jpg
lisomea Cambridge?
 
View attachment 1136786
Huo hapo ni mshahara wa mwalimu mwenye degree, kakaa darasani miaka mingi lakini anaishia kulipwa kiasi hicho sawa na Tsh 15000/= kwa siku.

Kwa mshahara huo ulipie nyumba, umeme na maji, mshahara huo utoe mahitaji ya familia, usaidie ndugu kule kijijini, ni kiasi gani utatunza kwa ajili ya maendeleo?

Hivi kwa mshahara huu unaweza kutunza mpaka ujenge nyumba ya kawaida tu ya milioni 30, unaweza kutunza na kununua kagari kweli?

Na hapo utakuta mtu anajisifu kabisa mimi ni mwalimu.
Lazima uanze ujasiriamali mkuu
 
Back
Top Bottom