Moja ya hotuba zenye kutia hofu ni hii ya kiongozi wetu. Anasema vyuo vingine vitajifuta vyenyewe. Mkuu ujue kujenga shule au chuo sio pesa ya mchezo, ujue vyuo hivyo havifi kwa sababu wenyewe ni matapeli hapana. kule Shinyanga askofu wa kanisa la AIC amefukuzwa kazi baada ya shule ya kanisa kujiendesha kwa hasara na kusababisha kuuzwa na bank ya CRDB.
Kwa sasa hivi wimbi la shule binafsi kufungwa na watoto kufukuzwa shule limepamba moto, wiki iliyopita shule ya msingi Jordan imewafukuza watoto wote kisa mzungu aliyekuwa anatoa pesa amejiondoa na wamiliki hawana fedha za kuendesha shule. Ujue shule sio sawa na roli kuwa likikosa mizigo utaliegesha na kupiga greese kama Mwijage alivyoshauri.
Utaratibu wa kuwapangia wanafunzi wa vyuo ulifanywa kihuni na maamuzi yale yaliyumbisha vyuo vingi vya binafsi, wakati chuo cha UDOM wakipewa wanafunzi elfu saba tena wote wakilipiwa ada na serikali chuo kama SAUT kilipunguziwa wanafunzi kutoka elfu tatu hadi chini ya elfu moja. Tulilipigia kelele humu lakini wapi! Hakuna aliyelisikiliza haya mbona umerudi kulekule.