Kwa mnaotumia au mliowahi kutumia m-pawa ya vodacom nataka kukopa laki 5 nitapewa?

Yusomwasha

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
2,092
838
wakuu kwa mnaotumia m-pawa nikitaka kukopa laki 5 niweke shilingi ngapi ili niweze kukopa?
na nitatakiwa kurejesha shilingi ngapi?
 
mhhhhhhhhhhhhh kwani ulivoingia mpawa ukaingia sehemu ya mkopo hujaapewa kiasi unachotakiwa kukopa?
 
Mikopo ya Mpawa haina msaada kiviile, maana wao wanakopesha kiasi pungufu ya ulichoweka kwenye akaunti yao. ambapo kwa mimi ni bora ku-draw hizo zilizopo kutumia then kuweka akiba baadae nikipata, kuliko kukopa na kulipa pamoja na riba=11% hivi
 
wakuu kwa mnaotumia m-pawa nikitaka kukopa laki 5 niweke shilingi ngapi ili niweze kukopa?
na nitatakiwa kurejesha shilingi ngapi?

Mkuu huwezi pewa 5laks mapema kihivyo lazima uanzie kiwango watakachokupangia starting 15,000 sasa jinsi utakavyokuwa unakopa na kulipa na kuweka akiba ndiyo jinsi kiwango chako cha kukopa ndivyo kinapanda! Lazima wakuscan kwa muda kidogo ndo utapata mzigo unaotaka.
 
mbona naskia nikiweka 150000 naweza kukopa laki 5?
hamna mkuu haiwezekani.

Halafu ukiweka pesa kiwango cha kukukopesha hakiweki hapohapo,polepole watakua wanakuongeza kufuatana na unavyoweka.
Hata uweke milioni 1 leo hawawezi ghafla kukupa laki 3,
ni taaratibu ngazi kwa ngazi
 
Lazima uwe na fedha kwenye M-PESA ndiyo ukope.

Haina maana ni bora uchukue fedha zako utumie halafu uweke tena akiba kwenye M-PESA
 
Back
Top Bottom