Kutoka National hadi IGOMBE ni kama kilomita 40 hivi, ina maana Serikali haiwezi kujenga hii barabara kwa kiwango cha lami kwa kutenga sh. Bilioni 10 kila mwezi kwa mkandarasi?
Na hii barabara ya Sabasaba hadi Buswelu nayo bado haijaanza kujengwa kwa lami sijui tatizo ni nini? kila mara ahadi-ahadi...
Harudi tena huyo,Wana ilemela tumeshajifunza hatuchagui tena upinzani hawana maono kabisa. Mama Mabula na kijana wetu Mr.Wanga pigeni kazi.
shagi upo kaka, salamu zao huko nawamisi.....Habari za leo wanaJF
Ndugu yangu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela Mwanza, kama mimi ningekuwa ndiyo weye (Mkurugenzi wa Manispaa Ilemela) basi ningemuagiza mhandisi wa manispaa kushughulikia barabara ya National hadi wilayani kwa kujenga mitaro imara ya kusafirisha maji.
Na ningemwagiza aweke makaRavati katika eneo la shule ya msingi Gedeli, Buswelu center na Bondeni ili kuifanya barabara isiharibike kwa maji ya mvua yanayopita juu ya barabara.
Lakini kikubwa kuliko vyote ningeifanya barabara hiyo kupitia fedha za makusanyo ya halmashauri ijengwe kwa kiwango cha lami kuanzia hapo National hadi eneo maarufu la "Mbogamboga" hapo Buswelu center.
Bahati mbaya tu ni kwamba mimi siyo mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela.
Veve ngosha mmpe hata makonda tuWana ilemela tumeshajifunza hatuchagui tena upinzani hawana maono kabisa. Mama Mabula na kijana wetu Mr.Wanga pigeni kazi.
Hivi hapa Tanzania kwa wakurugenzi Kuna mpiga dili zaidi ya huyu jamaa? Aliuza Nyumba za Halmashauri pale Ghana next to Rock City Mall akina Kinana wamejenga ghorofa na petrol stations. Huyu weka mbali na fedhaBwana Wanga ni jembe sana, mipango iko njiani kukamilisha barabara hizi kwa kiwango cha lami, wala hakuna mwananchi anyekwamisha ujenzi kisa lami, wapo wapiga dili ofisini kwake ndio wanaombabaisha.
Tuungane nae tupige kelele hadi hao wapiga dili waondoke, sie atujengee barabara fidia atatupa badae na tutabomoa wenyewe, sisi shida yetu barabara sio fidia.
Mkuu,maeneo ya milimani kulianza kujengwa barabara za mawe chini ya uongozi wa wabunge wa chadema,zilijengwa nyingi na zilisaidia,chini ya hewa wabunge wa ccm wamefuta kabisa ujenzi wa barabara hizo,majimboni hawaonekani,jiji limejaa keroHivi halmashauri ya manispaa ya Ilemela imewahi kujenga barabara ya lami hata moja toka imeanzishwa? Hii nchi ya kipumbavu Sana, mtu anakuwa mkurugenzi wa manispaa au jiji busy kujenga mabarabara ya vumbi na matope. Kifuku matope kiangazi vumbi halafu tunaita jiji au manispaa. Nani kasema duniani hapa majiji yanajenga barabara za matope? Only in Tanzania. Tuangalie watu wa kuwapa ukurugenzi wa majiji na manispaa sio kuokoteza tu
Tuuunganeni kwa pamoja wakazi wa Buswelu Majengo mapya, Nyamadoke, Ilalila, Buteja, Buyombe, Kigala, Bujingwa, Mbogamboga nk kwa kupiga kelele kila siku humu JF ili mkurugenzi asikie kelele zetu.
Namfahamu mkurugenzi ni member humu na hizi post anazisoma saaaana, hivo kwa pamoja tutamfanya achukue hatua.
Na ninaaamini tukipiga "kelele" kwa namna pia ya kutoa ushauri atatuelewa zaidi kwa kuwa yeye ni mtu muelewa.