Kwa Miswada hii na yanayofwanywa Bungeni ccm wanamalizia kujichimbia shimo

Kilala Makusaro

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
688
382
Binafsi nashidwa kuelewa kwanini ccm huwa hawasomi alama za nyakati.
Juzi hapa Kinana aliwaambia wabunge wa ccm kuwa wanatabia ya kusema ndioo kila kitu bila kusoma na kuelewa hivyo kupitisha hoja za ovyoovyo.

Nimejiuliza ccm hawaoni kuwa kuendelea kukomalia miswada hii hadi kuwafukuza upinzani wanajenga picha gani kwa wananchi.

Nikakumbuka usemi wa sikio la kufa halisikii dawa. Wakati huu wakiwa na mgogoro wa vyeo ndani ya ccm kwa kutumia nguvu kubwa kumzuia Lowassa huku akiwa amewazidi kwa mbinu mbalimbali chafu au vinginevyo na kuonesha picha kuiteka ccm, haikupaswa kabisa kuja na hoja za kuwaudhi wananchi.

Wakati huo huo wakijua ni majuzi escrow imekivuruga chama na hata vidonda vyake ndani ya taifa havijapona.

Kwa hali hii naiona ccm ikizamishwa shimoni october na hii inanipa ujasiri kuwaambia maccm mmelichimba hili shimo wenyewe sasa jiandaeni kuingia.
 
tena inabid ccm iwe makin na mambo yake wajue kuwa wananchi wanawaangalia na kuwatafakar wenyewe wanaona ni sawa au sifa lakin wajue wanawatengenezea upinzan fursa ya kukubalika zaid na zaid
 
Back
Top Bottom