Mheshimiwa Sana dr.Mary Michael Nagu waziri na mbunge wa jimbo la Hanag, nakuletea lalamiko la wananchi wa kijiji cha Getasam ambao wamekwama hata kutoa mazao Yao mashambani kutokana na korongo kubwa lililokatika nakutenganisha vitongoji vya kijiji hicho,aidha inasemekana tangu uchaguzi wa 2010 hujawahi kufika kijijini hapo.wanachi wa kijiji hicho wanahitaji daraja amabalo litawawezesha jusafirisha mazao Yao kutoka mashambani kwenda majumbani na pia soko la mazao ambalo lipo Endasaki,aidha wananchi hao wamebaki katika mazingira magumu angali wanamwakilishi tena waziri katika serikali hii sikivu.Tunaomba tujengewe daraja mheshmiwa nbunge.