Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufuli

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
Shikamoo Mheshimiwa Rais.

Awali ya yote nikupe pole kwa majukumu mazito tuliyokutwika.

Mhemiwa Rais, nakuandikia barua hii nikiwa mtanzania kamili ninayetokea mkoa wa Ruvuma wilaya ya Namtumbo. Kwanza nikupongeze kwa kufanya ziara mkoani kwetu kwa hakika tulikumiss sana. Tunajua ujio wako ni neema kubwa kwetu.

Mheshmiwa Rais, sisi wana Ruvuma kiukweli, tunakushukuru wewe binafsi pamoja na Serikali unayoiongoza kwa upendeleo wa kipekee kwenye miradi ya maendeleo. Kwa muda mrefu sana kero yetu kubwa wana Ruvuma ilikuwa barabara na Umeme wa uhakika kitu ambacho ilisababisha mkoa wetu kukosa uwekezaji mkubwa wa viwanda. Lakini hadi sasa tunapozungumza barabara ya kutoka Songea Mjini - Namtumbo na Namtumbo -Tunduru na pia Songea Mjini - Mbinga zote zimekamilika kwa kiwango cha lami. Na ile ya mbinga Mbambabay ikiwa inaendelea kujengwa na tumesikia jana ukimtaka mkandarasi akamilishe ujenzi wake ifikapo mwaka 2020 na wewe mwenyewe uweze kuifungua.Tunakushukuru sana.

Mheshimiwa Rais, mkoa wetu kwasasa umefunguliwa vizuri sana kiasi kwamba, sasa hivi, mwananchi akitaka kwenda Dsm ana hiyari ya kuchagua njia, apite barabara ya Tunduru Mtwara Lindi au apite Njombe, Iringa Morogoro. Kwakweli tunafuraha kubwa isiyo kifani.

Mheshimwa Rais, kwenye suala la umeme halikadhali nalo kwa upande wake limekaa vizuri, tayari grid ya taifa kutokea Makambako imeshatua Ruvuma na kusambazwa kwenye wilaya zote na baadhi ya vijiji. Tunashukuru pia kwa ujio wako umeweza kutuongezea kiasi cha shilingi bilion 31 ili kusaidia vijiji vyote vya mkoa wa Ruvuma viweze kupata umeme. Tuseme nini tena juu yako zaidi ya kukushukuru. Asante sana mhedhimiwa Rais wetu. Kwa hakika umetutoa kimasomaso na sidhani kama kuna mkoa wowote uliyopendelewa kama mkoa wetu. Niseme tu wazi kuwa tunaona fahari kuwa Rais wetu na tunatembea kifua mbele.

Mheshimiwa Rais pamoja na shukrani zetu kwako bado tuna maombi ya ziada tunaomba uzidi kututazama kwa jicho la upendelei. Kwanza barabara ya kutoka Songea Mjini hadi Njombe. Kwakweli barabara hii imekuwa finyu sana kiasi kwamba imekuwa ikisababisha ajali za mara kwa mara. Nadhani kwa sababu unatumia usafiri wa barabara utaweza kuliona hili. Ni moja kati ya barabara ambazo toka zimejengwa enzi ya mkoloni hazijapata kuboreshwa upya. Tunatamani sana barabara hiyo ijengwe upya ili kutoa fursa ya kutanuliwa na hatimaye iweze kukidhi mahitaji ya sasa.

Mhemiwa Rais pia kwenye eneo hili la Barabara napenda kutoa maombi maalum kwa barabara ya Lumecha - Londo - Malinyi - Lupiro - Ifakara hadi Mikumi nayo mchakato wake wa kujengwa kwa lami uweze kukimbizwa. Barabara hii ina umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa mkoa wa Ruvuma, Morogoro na Tanzania kwa ujumla. Kwani kwa kukamilika barabara hii itasaidia kuufungua mkoa wa Ruvuma pamoja na Mkoa wa Morogoro kwenye masuala ya masoko na fursa mbalimbali za kibiashara. Lakini zaidi ya yote, itakuwa imepunguza umbali wa kutoka Songea hadi Dsm na pia Songea hadi Dodoma makao makuu ya nchi yetu.

Mheshimiwa Rais mkoa wa Ruvuma umepakana na nchi ya Msumbiji na Malawi. Tunaomba tujengewe barabara ya lami kutoka Likuyu Fusi Songea hadi Mkwenda kwenye mji wa mpakani na Msumbuji kwenye daraja la Umoja 2 katika mto Ruvuma ambapo daraja lake tayari limekwisha kujengwa na kukamilika. Kujengwa kwa barabara hii itasaidia kuufungua mkoa wa Ruvuma kiuchumi. Ukiwa Ruvuma, Msumbiji ni jirani zaidi. Kupitia barabara hiyo itasaidia kutanua wigo wa biashara na hivyo kufanya Songea kuwa lango kuu la biashara kwa nchi ya Msumbiji na Malawi. Lakini kwa upande wa Malawi ikikamilika barabara ya Mbinga Mbambabay tayari itakuwa imerahisisha biashara na Malawi na kuifanya rasmi Mbinga kuwa Mbinguni.

Mheshimwa Rais kimsingi wananchi wa Ruvuma ni wakulima wa kweli. Kwenye suala la kulima hakuna mwananchi anayetumwa kulima. Kila mtu anajua wajibu wake. Ruvuma ni moja ya mikoa yenye kuzalisha kiwango kikubwa cha mazao ya biashara na chakula. Tunazalisha Korosho, tunazalisha Tumbaku, Tunazalisha kahawa, Tunazalisha mahindi, maharage, karanga, ufuta, mpunga, soya, viazi vitamu na mazao mengi mengi. Na pia siku za hivi karibuni tumeanza kuzalisha Tangawizi kwa wingi sana.

Mheshimiwa Rais, Shida yetu kubwa iko kwenye upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa ajili ya kuuzia mazao yetu. Mazao ya chakula tunazalisha hadi ziada. Tunashukuru kwa kutupatia soko la mahindi kupitia WFP, tunaomba na mazao mengine uweze kuangalia namna ya kuturahisishia upatikanaji wa masoko yake.

Mheshimiwa Rais, namna pekee ambayo tutaweza kupata masoko ni kupitia mfumo wa aidha kufungua mipaka na kuruhusu wageni kuingia na kununua mazao au serikali yenyewe ikanunua mazao ya wakulima kupitia NRFA na kwenda kuuza nchi zenye njaa na vita mfano Somalia, Sudani kusini, Congo DRC nk. Hapo utakuwa umetusaidia sana hasa ukizingatia kuwa kilimo kwetu ndiyo kazi. Kupitia kilimo tunajenga, kusomesha watoto na pia kujipatia mahitaji yetu mengine ya muhimu. Kilimo bila masoko ni kazi bure.

Mheshimiwa Rais kwa sababu una majukumu mengi naomba nisikuchoshe kwa barua ndefu. Nakushukuru kwa kupata wasaa wa kusoma barua yangu. Naomba nikutakie afya njema, amani na utulivu katika kipindi chote cha uongozi wako na maisha yako yote kwa ujumla. Mwenyezi Mungu akubariki sana.

Wasalaam

Inaonekana Mkoa wa Ruvuma wote sio Mbinga tu ni kama mbinguni na bado unamwomba Rais atoe upendeleo mambo mengine mengi huku ukijua sehemu KUBWA ya nchi haina hata hayo unayoshukuru yametekelezwa huko kwenu. Kuna Mikoa toka tupate uhuru bado haina umeme wala barabara za kuaminika lakini wewe unaomba baraba kuunganisha Mkoa wako na nchi jirani. Ubinafsi wa hali ya juu.
 
Barabara ya Songea- Njombe haikujengwa wakati wa mkoloni ilijengwa miaka ya 1980's

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka vizuri hata Mimi ujenzi wa barabara hii,jamaa kanishtua kusema ilijengwa Na wakoloni,barabara ilianza kujengwa pale makambako 1980 Na ilikamilika mwaka 1986

Tatizo mkuu wakati huo alikuwa anavua samaki kwa hiyo hajui kilichokuwa kinaendelea duniani. Kama kumbukumbu zangu ziko sawa barabara hii ilijengwa na kampuni ya Balfour Beatty ya Uingereza, enzi za Mwalimu Nyerere.
 
Mkuu pamoja na barua yako nzuri, ni vyema pia ukaangalia mkoa wa Ruvuma unachangia kiasi gani kwenye pato la taifa,ukishajua ufanyie uhariri barua yako kwa vile ulivyoomba kama mnastahili zaidi ya vilivyopo au viongezwe zaidi.
 
Halafu pia bwana ngoma tunaomba hizo barabara mlizonazo mpaka sasa tunaomba mbadilike kwa kulima ngano zaidi kuliko mahindi, kwani ushahidi wa kisayansi watu wanaokula mahindi/ugali hawana akili. Ushahidi ni huu ambao watu wa huko ni maskini japo wanakula na kushiba, sababu hasa ni ulaji wa ugali. Pia fungua vitabu vya dini uone kama Mungu aliwahi kumuagiza Nuhu atunze mahindi zaidi ya ngano kwenye Safina na pia kama kuna mahali popote kwenye vitabu hivyo vinaongelea mahindi kama chakula cha binadamu.

Iwapo mtaendelea kulima mahindi kwa wingi na kutumia hizo barabara kusambaza mahindi hayo nchi nzima ni dhahiri mtakuwa mnaendeleza ujinga ndani ya taifa, lakini mkilima ngano mtaliokoa taifa hili. Limeni ngano tuuze Ulaya sio mahindi ya kuwauzia waafrika wenzetu wanaopigana kwa ujinga wao na wa viongozi wao wanaotumia vyombo vya dola kukaa madarakani. Tukiwa na ngano tutauza Ulaya, Amerika na Asia kwenye watu wanaotumia chakula kinacholeta akili.
 
Ni moja kati ya barabara ambazo toka zimejengwa enzi ya mkoloni hazijapata kuboreshwa upya. Tunatamani sana barabara hiyo ijengwe upya ili kutoa fursa ya kutanuliwa na hatimaye iweze kukidhi mahitaji ya sasa

Usiwe mwongo barabara hiyo imejengwa mwaka 1980 hadi 1984, jiwe lake la msingi la uzinduzi wa ujenzi liliwekwa na Marehemu Aboud Jumbe akiwa Rais wa Zanzibar na liliwekwa pale Njombe airport, ujenzi wake ulikuwa ukamilike 1985 lakini kampuni ya Balfour Beaty ilikamilisha ujenzi wake mapema zaidi kabla ya muda wake nadhani kama sijakosea ilizinduliwa na Hayati Mwl Nyerere au Mzee Mwinyi na uzinduzi ulifanyikia Songea japo sikumbuki vizuri

Je Mwl Nyerere alikuwa mkoloni?
 
Nakumbuka vizuri hata Mimi ujenzi wa barabara hii,jamaa kanishtua kusema ilijengwa Na wakoloni,barabara ilianza kujengwa pale makambako 1980 Na ilikamilika mwaka 1986

Imekamilika kabla ya hapo Mkuu ila ilikabidhiwa nadhani mwishoni mwa 1985
 
Back
Top Bottom