Kwa Mh. Lukuvi

Kwa Mh. Lukuvi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,300
Reaction score
17,577
Watanzania tunaongezeka lakini ardhi haiongezeki, hivyo mipango mizuri ya matumizi ya ardhi inahitajika. Kwenye mipango yako ya matumizi ya ardhi makazi, misitu, kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, wanyama na viwanda vimepangiwa asilimia ngapi kila moja ya ardhi ya Tanzania? Wapi kunatakiwa kujengwa ghorofa na wapi kujengwe nyumba fupi? Bila mipango madhubuti ya ardhi inayoweza kufundishwa hata shule za msingi na sekondari migogoro ya ardhi Tanzania haiwezi kwisha. Ni rahisi sana kuchoma moto nyumba za waliovamia hifadhani lakini Ni vigumu sana kuwaonyesha watu wapi pa kulima, kuchungia na kujenga.
 
Back
Top Bottom