Kwa mfumo huu wa TRA wengi tutafunga Biashara

Habari wadau;
Ni hivi;Nilitembelewa na wakaguzi wa TRA ofisini kwangu.Walipofika walianza kuniuliza maswali mengi na nikawapa nyaraka zote walizotaka na kwa mujibu wa Taarifa zangu kodi yangu nilishalipa yaani sikuwa na deni.

Basi baada ya kuona niko safi wakaanza kuniuliza maswali ya kipuuzi.Moja wapo ilikuwa niwaonyeshe risiti ninazowapa wateja wanaponunua nikawapa wakajumlisha sana kisha wakasema mbona kodi unayolipa ni ndogo kuliko mapato yako?

Nikawatazama kwa jicho la dharau kisha nikiwauliza kivipi?Wakanipa maelezo mazuri sana.Nikiwaambia hivi kodi inatozwa kwenye faida au kwenye mapato wakasema kwenye faida basi nikawaulizambona hamjauliza taarifa za matumizi?Wakasema tupatie basi nikawapatia.

Katika matumizi ikaonekana kwa faida ninayopata basi hata kodi ninayolipa nikubwa hivi inabidi nipunguze kiwango cha kodi kwani kwa faida niliyopata ni kama vile tunagawana robo kwa 75.Yaani mimi nabaki na 25 wao wanakula 75% ya faida yangu.

Walipoona hivo wakaanza kukagua risiti zangu za matumizi,kwa kuwa mimi ni mjasiriamali na biashara yangu ni ya kuuza chakula kwa hiyo kiasi kikubwa cha manunuzi yangu hayana risiti kwa hiyo tulianza kubishana sana na hawa watu wakaweka kofuli kwenye ofisi yangu wakitaka niende TRA ofisini kwao.

Kiukweli kutokana na biashara kuwa ngumu na kwa kuwa kodi yangu inaisha mwisho wa mwezi wa pili niliwaambia sawa na walipomaliza kufunga usiku nimeita fundi welding nimevunja lile kofuli lao nimebeba materials zangu zote,kisha nimeenda polisi kufungua kesi kuwa nimevamiwa na majambazi wameiba kila kitu.na niko hapa TRA na RB yangu ya kuibiwa nawaona wanavojichnaganya tu kunitishia huku wakifikiri mimi sielewi ninachofanya.Yaani mfungie masufuria yanu,bakuli,majiko nakadhalika kwa sababu tu mnataka kunikamua.

Kakamueni wake zenu na kama mmechafukwa mnifunge basi ila kodi silipi tena huko ninakoenda naenda kufungua biashara bila kulipa kodi.Huu wizi wizi sitaki tena kufanyiwa nimechoka
Pole sana mkuu,hao washenzi,natamani niwe mmoja wa "wasiojurikana"ili nikutane nao kitaani kwetu,niwatumbue
 
Tutazoea tuu; mnakwenda Nairobi mnafahamu ukinunua hata CHIPS KAVU; unapewa risiti ya machine.

Ila ndugu zangu wa TRA kudai risiti kwa bidhaa zilizonunuliwa toka sekta isiyo rasmi (wakulima na masokoni) mtafanya sekta rasmi isifanye biashara na sekta isiyorasmi na hii itapelekea sekta rasmi kudumaa kwani ile isiyorasmi itakufa kwa kukosa biasha toka sekta rasmi.

Nachotaka kusema, mahoteli huenda yakawa sasa yananunua mbogamboga, matunda, nyama toka Super Markets badala ya sokoni au kwa wakulima. Na hawa wenye super markets kwa kuwa sekta isiyorasmi hawana EFD, wataamua kuagiza mbogamboga, mtunda na bidhaa nyingine zinazozalishwa na sekta isiyorasmi toka nje ya nchi.

Busara zitumike ili kukuza sekta zote za uchumi; sheria zipo lakini zisitumike kumyima bibi yangu pale kijijini kuuza maparachichi na ndizi ,mbivu hotel zilizokaribu na kwake
Tupe mrejesho wa utitiri wa kodi kuanzia Huduma za Afya Elimu na mfumko wa bei.Mbona pesa mnakusanya lakini mnazihamishia nje ya nchi? Serkali hii moto wa milele ni sehemu yenu.
 
Tupe mrejesho wa utitiri wa kodi kuanzia Huduma za Afya Elimu na mfumko wa bei.Mbona pesa mnakusanya lakini mnazihamishia nje ya nchi? Serkali hii moto wa milele ni sehemu yenu.
Kijana mimi siko serikalini; uchambuzi ule unatokana changamoto zinatoka kwa wateja wangu
 
Back
Top Bottom