Kwa masharti haya UDSM ni wabaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa masharti haya UDSM ni wabaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,752
  Trophy Points: 280
  Date::1/16/2009
  Kwa masharti haya UDSM ni wabaguzi
  Mwananchi​

  MWISHONI mwa mwaka jana wanafunzi wa shahada ya kwanza kutoka vyuo vikuu saba vya umma nchini, walisimamishwa masomo kutokana na mgomo wao wa kupinga sera ya uchangiaji elimu ya juu.

  Mgomo huo ulioanzia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na baadaye kusambaa hadi katika vyuo vingine, ulilenga kuishinikiza serikali iwape mikopo wanafunzi wote kwa asilimia 100 bila kubagua.

  Wanafunzi hao walikuwa wanapinga utaratibu wa sasa wa kuwatenga kwenye makundi, wengine kupewa mikopo kwa asilimia 100 na wengine hadi asilimia 20 tu.

  Baada ya wanafunzi kusimamishwa, uongozi wa vyuo uliweka masharti magumu zaidi ya kurejea kwao kama vile kujaza fomu maalum.

  Mathalani, mbali ya kulipa ada yote, uongozi wa UDSM umetangaza kufutwa kwa sheria zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi (Daruso) na kutoa vitambulisho vipya.

  Kutokana na ugumu wa masharti hayo na kwa kuwa mkazo wa uongozi wa UDSM uko katika kupata pesa kwa asilimia ile ambayo kila mwanafunzi anapaswa kutoa, ni asilimia 33 tu ya wanafunzi wote wa shahada ya kwanza waliotekeleza na ambao kimsingi ndio wataruhusiwa kuingia darasani kuanzia Jumatatu.

  Hii ina maana kuwa asilimia 67 watakuwa wamejifukuzisha chuo kwa kushindwa kutekeleza masharti yaliyowekwa na chuo.

  Wadau mbalimbali wa elimu walikuwa wanadhani ya kuwa katika kipindi chote cha kuanzia Novemba 12, 2008 waliposimamishwa wanafunzi hao, mamlaka zinazohusika, yaani vyuo vikuu, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na serikali zingeyafanyia kazi kwa umakini madai ya wanafunzi.

  Lakini badala yake wameyatupa kiasi kwamba asilimia 67 ya wanafunzi wengi wao kutoka familia masikini wanatarajiwa kukosa elimu ya juu kwa sababu ya umasikini wao.

  Hapa tunaanza kushuhudia ubaguzi ukianza kujitokeza katika sekta ya elimu kwamba, watoto wa masikini hawana nafasi tena ya kupata elimu ya juu, ikimaanisha kuwa vyuo vya umma sasa ni sawa na vyuo binafsi ambako mwanafuzi asiyelipa ada hufukuzwa.

  Na hapa ndipo tunajiuliza kwamba, UDSM wanafaidika vipi kwa wanafunzi wengi kiasi hicho kutimuliwa? Ni kwanini zinatolewa kauli kwamba, hakuna mwanafunzi atakayekosa masomo kwa sababu ya umasikini, lakini wengi wanafukuzwa? Tunarudia kutoa ushauri kwamba, sera ya uchangiaji wa elimu ya juu ipitiwe upya ili kutoa haki sawa kwa wanafuzi wote.
   
 2. S

  Sheikh Member

  #2
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UDSM : Sasa Kisiwa cha 'udikteta' ndani ya Nchi ya Kidemokrasia Tanzania

  AMRI, vitisho, mabavu, unyanyasaji na matumizi ya vyombo vya dola bila sababu za kibusara na kihekima ila vitisho na kuonesha musuli kati ya kina David na Golliath kumegeuza eneo la Chuo Kikuu mlimani kuwa kisiwa cha udikteta ndani ya demokrasia yetu.

  Mahala hapa ambapo kwa kawaida ni patulivu kama mbuga za Ngorongoro kila kiumbe aghalabu akiwa anajishughulisha na yanayomhusu mpaka apate wakuu wanapogeuza chuo kuwa uwanja wa vita ili kuwatisha wakuu wa serikali kwamba mambo hapa ni magumu sana kumbe wana yao wanayoyaficha.


  Ninawauliza wakubwa hivi siku zote mdogo au mwanafunzi ndiye anayeonekana mwenye makosa lakini sio mkubwa?

  Hivi mbona nchi zingine hakuna migomo ya wanafunzi kama nchini kweetu. Mbona tumeunda tume nyingi lakini hatuuundi tume kuchunguza tatizo ni nini na nini kifanyike ili migomo katika vyuo vikuu ibaki kwenye kaburi la sahau.

  Elimu ni kukomoana au kusaidiana ili nchi iwe na rasilimali watu tosha na endelevu kuhakikisha maendeleo ya aina mbalimbali yanaptikana.

  Taswira inayoumbwa hivi sasa na uongozi wa UDSM inaweza kubashiri nini kitakachotokea kama viongozi wa juu wa UDSM ghafla watakuwa ndio viongozi wa Tanzania. Inatisha!

  Wanafunzi wa vyuo vikuu katika nchi nyingine huwa ni rasilimali muhimu katika uendelezaji utafiti na ubunfu wa mambo mnalimbali mapya au uboeshaji wa yale yaliyopo hivi sasa. Umri wa wanafunzi wa vyuo kisaikolojia ni umri ambapo ubunifu na uvumbuzi miongoni mwao ndio unafikia kipeo chake cha juu kabisa.

  Hapa Tanzania tunauchezea umri huo. Badala ya kuwapa vijana changamoto za utafiti na ubunifu sisi tunakula fedha za misaada kwa kujenga mahekalu ambayo kwa mujibu Babu Bubu fisadi wana miaka 2 au mitatu tu ya kuishi humo ....... na kisha kuwasakazia wanafunzi paka! Aibu iliyoje!!!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli masharti zaidi ya kambi ya jeshi......sitaki kufikiria jinsi mlimani palivyogeuka kisiwani tena kisiwa cha ulinzi mkali vile.....sijui ngoja tuone leo ndio day 2 ......ila nadhan gharama kubwa sana kuweka yale masharti hasa watu kutoingia,no dala,hakuna kupita.....du haya ngoja tuone.
   
 4. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tatizo hapa ni kuchanganya siasa na shughuli za uendeshaji wa Chuo maana shughuli za ufundishaji haziwezi kuendeshwa bila fedha.

  Waandishi wa Habari na wakosoaji inapasa tujiulize mbona hatukuwahi kusikia ubaguzi wa aina hii siku za nyuma kabla ya Serikali kuleta sera ya uchangiaji Elimu? With my naked eye naona hapa tatizo ni wanasiasa. Mwanasiasa leo anahubiri kuwa hakuna mwanafunzi kufukuzwa kwa ukosefu wa ada, huyohuyo anageuka na kusema wanafunzi lazima wachangie 60% (what the hell is this?)

  Nadhani mwandishi anapaswa kujiuliza na kuchambua zaidi ya kukilaumu Chuo maana Chuo kinafata sera iliyowekwa na Serikali. Wa kulaumiwa hapa ni Serikali na siasa zake.
   
 5. a

  akili Member

  #5
  Jan 18, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi watoto wa wakubwa wa Chuo Kikuu, shemeji na wajomba zao wanasoma wapi Tanzania au Marekani?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,752
  Trophy Points: 280
  Date::1/18/2009
  UDSM yaongeza muda wa udahili
  Boniface Meena
  Mwananchi​

  CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), kimeongeza muda wa wanafunzi kutuma upya maombi ya udahili chuoni hapo, hadi Januari 29 mwaka huu.

  Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi kukamilisha uwasilishaji wa kiwango cha ada wanachostahili, kutoa kwa mwaka wa masomo 2008/09 kabla ya kuruhusiwa kujiunga na masomo katika muhula huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala alisema" Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeongeza muda wa wanafunzi kutuma upya maombi ya udahili chuoni hapo, hadi Januari 29 mwaka huu."

  Awali, wanafunzi hao walitakiwa wawe wametimiza masharti ya udahili wao tangu Januari 2 mwaka huu.

  Akizungumzia kufunguliwa kwa vyuo hivyo Mukandala alisema majina ya wanafunzi waliotimiza masharti yote ya kudahiliwa upya tayari yameingizwa katika tovuti ya chuo hicho na kuwataka wanafunzi kuanza upya udahili kesho.

  "Majina ya wanafunzi ambao tayari wametimiza masharti yote ya kudahiliwa upya yamewekwa kwenye tovuti ya chuo na kuanzia Jumatatu (kesho) wanafunzi wanatakiwa waanze udahili upya," alisema Profesa Mukandala.

  Alibainisha kuwa kila mwanafunzi atatakiwa kuvaa kitambulisho chake kipya na kwamba hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuingia bwenini, darasani au kwenye mihadhara bila kuvaa kitambulisho hicho.

  Alisema itakuwa ni uvunjaji wa sheria kwa mtu yeyote kuingia chuoni bila kitambulisho halali au ruhusa maalumu.

  Katika hatua nyingine, Profesa Mukandala ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kufutwa kwa Chama cha Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO) na kueleza usahihi ni kwamba chama hicho hakijafutwa.

  Alifafanua kuwa kimsingi kwa kanuni na taratibu za chuo hicho baada ya kusimamishwa masomo, wanafunzi wote walipoteza udahili wao.

  Aliongeza kutokana na kutokuwepo wanafunzi halali wa chuo hicho, wote waliokuwa viongozi wa Daruso nao pia walipoteza nyadhifa zao za uongozi.

  "Kwa mantiki hiyo, itakuwa kinyume cha sheria kwa mwanafunzi yeyote kufanya chochote kile kwa kisingizio cha kuwa kiongozi wa wanafunzi aliyechaguliwa," alisema Mukandala.

  Wakati Mukandala akisisitiza hivyo aliyekuwa Rais wa Daruso, Anthony Machibya amepingana na kauli hiyo na kusema, wao bado ni viongozi halali na wenye mamlaka hivyo uongozi wa chuo hauwezi kuwafuta kwa kuwa hauna mamlaka hayo.

  Alisema wao ni wanafunzi halali wa chuo hicho na kuwataka wanafunzi wote waliosimamishwa masomo kurudi chuoni, punde taarifa kufunguliwa chuo zikiwafikia kwani wao pia ni wanafunzi halali wa UDSM.

  Kuhusu rufaa za wanafunzi ambazo Waziri wa Elemu na Mafunzo ya Ufundi, Jumanne Maghembe amedai zipelekwe kwake, Machibya alisema waziri huyo anadanganya kwa kuwa tayari anazo rufaa nyingi za wanafunzi mkononi mwake kwa muda mrefu na hajatoa majibu kwa rufaa hata moja.

  Machibya pia alishangaa waziri huyo pamoja na Profesa Mukandala kueleza kuwa wanafunzi wengi wametimiza masharti bila kutoa idadi yao kitu ambacho kinaonyesha kutokufanyika vitu kwa umakini.

  Alisema kwa takwimu ambazo serikali yake inazo ni kuwa kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi waliotimiza masharti ni 3,100 kati ya wanafunzi 11,300 kitu ambacho kinaonyesha wengi watabaki nyumbani.


  Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Umma (Uvijuta), Silinde David, alisema wanafunzi waliofukuzwa vyuoni walikuwa ni 31,443 na hadi hivi sasa walioweza kulipa ni asilimia 13 ya wanafunzi hao huku asilimia 87 ambayo ni sawa na wanafunzi 27,289 hawajalipa.
   
Loading...