Kwa mashabiki wote wa Yanga: Manara anabaki kuwa shujaa aliyeshindikana katika utani wa jadi

Alkam Alkam

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
602
509
MANARA ANABAKI KUWA SHUJAA ALIYESHINDIKANA KATIKA UTANI WA JADI.

Niliwahi kuandika siku za karibu Yanga wakitaniwa utani unaoakisi ukweli wanakimbilia kumtusi Mo au Manara. Mnajua ni kwa nini? Wanaamini Mo ndio anaiwezesha Simba kuwepo hapo ilipo na ndio maana inakuwa juu yao.

Na wanaamini mtu aliyewashinda kwa uwezo wao wa kuzusha na kulaghai watu ni Manara. Ikumbukwe Manara alilelewa kwao. Hivyo mbinu zao zote anazijua. Hivyo inakuwa rahisi kwake kujua wapi apige waumie. Si anaujua udhaifu wao?

Nimemsikia Bumburi akiporomosha matusi ya nguoni kama kawaida ya wapuuzi wote walivyo. Ni mpuuzi tu ndio anaweza kufika mahali bila kujali chochote akaamua kuporomosha matusi hadharani hakuna jina lingine zuri la kumwita bali ni Mpuuzi.

Eti amekasirishwa kutaniwa baada ya kunusurika kwenye ajali baada ya tairi ya basi lao kupasuka hivyo alihitaji pole na sio kutaniwa. Utani una mipaka? Kilimjaza Bumburi sio hicho. Kilichomjaza na hasira za kutaniwa kusafirisha timu kwa basi bovu lisilofanyiwa ukarabati mpaka Shinyanga huku wakijinadi timu imehama kwenye umaskini na sasa ina hiduma kama wapatazo Simba. Sasa kauli na vitendo ni tofauti. Na kusafiri na basi huwezi kuficha. Hivyo kutaniwa kwenye hili ndiko kuliko mjaza na akakosa majibu. Akaamua kuwa Mpuuzi.

Manara anajua utani na ndio maana mpaka leo hajawahi kuitwa au kushutumiwa popote kuwa anatakiwa kujibu kauli zake. Zaidi tu ya Wanayanga kumchukia na kusema anaisema timu yao vibaya. Hivi mlitaka Manara aisema Yanga vizuri? Au mlitaka Manara asiitaja Yanga? Si Manara tu hata Mimi nikipata nafasi ya kuikejeli Yanga na kuwashusha thamani nitafanya hivyo.

Niwakumbushe baadha ya utani Yanga waliowahi kuwafanyia Simba na hakuna aliyewahi kuwatukana.

1 Miaka ya 1990 waliwahi kuja na shanga pale Uhuru wakaturushia kwa marundo wakidai Simba tunafuga mashoga na hakuna aliyewatukana bali tuliishia kucheka.

2. Jery Muro aliwahi kusema Yanga ya Manji itainunua Simba na kupeleka wachezaji wake wote wakacheze soka la ufukweni. Hakuna aliyewaporomoshea matusi bali tulicheka tu.

3. Yanga hawa hawa kupitia kifo cha Marehemu Mafisango tena kupitia msemaji wao waliwahi kutuambia tumekula fedha za rambi rambi na hatuwezi kuwa mabingwa mpaka turudishe rambi rambi hakuna aliyepaniki na kuwaporomoshea matusi.

4. Hawa hawa tulipopata ajali tukitokea Dodoma na kumpoteza mpendwa wetu bado walitutania kwamba ajali ile ilisababishwa na matunguri tuliyobeba na tumemtoa kafara ili tutwae kombe la Fa. Hakuna aliyewaporomoshea matusi.

Kinachowauma Yanga wote sio ajali ni kutaniwa mambo yanayoakisi ukweli na wanaona kabisa washazidiwa mno na hawana majibu hivyo wanakimbilia kwenye matusi. Ni kawaida ya mtu yeyote dhaifu akiidhiwa hoja hukimbilia kwenye matusi.

Kwa hili Bumbuli amejidhalilisha, ameidhalilisha klabu yake na amedhalilisha mashabiki wote wa soka nchini. Anatakiwa ajitafakari kama kweli ana wazazi na amelelewa katika maadili ya kitanzania. Au ni mtu wa aina fulani ila huwa anafanikiwa kuficha tabia zake halisi na sasa ameoneka Bumburi halisi na sura yake ndio hiyo.

Vyovyote iwavyo na kwa namma yoyote hakuna namna yoyote ya kuhalalisha matusi ila lugha nzuri ya mtukanaji daima ni PUNGUANI NA MPUUZI.
 
kuna siku dauda watu watakuja kumuelewa pia..

Screenshot_2020-06-12-14-07-50.jpg
Screenshot_2020-06-12-14-08-06.jpg
 
Huyu Haji Manara ana maneno ya shombo Sana Binafsi siungi maneno kabisa ni kwà ushujaa upi alionyesha Hadi umpe hiko cheo, Haji Kama Haji kipindi Simba haijiwezi ulikuwa unamskia wapi!? Angefanya hayo yote kipindi kile wakiwa katika Hali ngumu leo hii ningekuwa mmoja wa watu tunaetambua huo ushujaa

Haji Manara Hana lolote tatizo ni mswahili tu mjanja mjanja na anajua kutumia lugha za mitaani Basi na huo ndio kwà ujinga wetu na elimu ndogo tunaita ushujaa ukitaka kujua Haji Manara Hakuna Kitu Jaribu kufatilia interview zake hasa alizokuwa WASAFI FM ndio utajua jamaa uswahili tu una mbeba Ila Hana ushujaa wowote zadi ashukuru mungu kipindi chake ni kipindi cha neema tu!!
 
Wengine wanasafiri kwa basi wengine kwa ndege. Hapo tayari wale waliosafiri kwa basi wanajisikiaje? Si wanajiona hawana thamani?
 
Manara ni mpumbavu, ye akitaniwa na Jery Muro analia mwezi mzima, hana akili ni mjinga sana, na hajui utani
 
Mkitaniwa msiwe mnakimbilia TTF. PIA ishu ya tairi ni kuwa kinachofanya kaz kinaweza kuharibika. Hata ndege zinapata ajali.
 
Timu imesafiri.Iwe kwa miguu au kwa Basi, wengine kwanin muumie? FUATILIENI TIMU ZENU hata Kama ni za nje.
 
Hakuna lolote kwamba ameshindikana.
1. Watu hawafiki nae mpaka mwisho kwenye utani nae. Hiyo ksbb maalum.
2. Simba waoga mno. Wakitaniwa hawachelewi hata kwenda polisi,mpaka kokote wanaenda kwa ajili ya kulialia kuhusu huo huo utani,wakitaniwa kisawa sawa,. Ikibidi hata kutembea na cd kwenye media zote
 
Manara amejua kuwapatia kandambili.

Tembezeni bakuli tuikwamue yanga pale msituni.

Nasikia hata mafuta wanaweka ya kidebe😁

Shukrani za pekee ziwaendee bodaboda!
Maana kila ikipita bodaboda inastopishwa na dereva anaulizwa "mwana we chama gani?" akijichanganya tu akasema "yanga" wanamwambia achangie mafuta na fasta kuna mchezaji anafungua tenki la mafuta la bodaboda na "kupiga nyoka" hata ikipatikana nusu lita wanashuru mno😁😁

Vyura Ni nimaaa! Aibu tupu.
 
Kutokana na u albino wake watu huwa hawamjibu inavyopaswa ili isionekane ananyanyaswa, na yeye hutumia mwanya huo kuongea ujinga mwingi, Jerry alipimjibu, Manara alikuwa anazunguka kila station kulalamika kudhalilishwa huku akitema mate kama cobra.
 
Lazima atukanwe hakuna njia nyingine ya kumjibu mpuuzi ambaye anadhani popularity yake ni kuisema Yanga namwomba Bumbuli aongeze matusi ndiyo lugha anayoifahamu Manara
 
MANARA ANABAKI KUWA SHUJAA ALIYESHINDIKANA KATIKA UTANI WA JADI.

Niliwahi kuandika siku za karibu Yanga wakitaniwa utani unaoakisi ukweli wanakimbilia kumtusi Mo au Manara. Mnajua ni kwa nini? Wanaamini Mo ndio anaiwezesha Simba kuwepo hapo ilipo na ndio maana inakuwa juu yao.

Na wanaamini mtu aliyewashinda kwa uwezo wao wa kuzusha na kulaghai watu ni Manara. Ikumbukwe Manara alilelewa kwao. Hivyo mbinu zao zote anazijua. Hivyo inakuwa rahisi kwake kujua wapi apige waumie. Si anaujua udhaifu wao?

Nimemsikia Bumburi akiporomosha matusi ya nguoni kama kawaida ya wapuuzi wote walivyo. Ni mpuuzi tu ndio anaweza kufika mahali bila kujali chochote akaamua kuporomosha matusi hadharani hakuna jina lingine zuri la kumwita bali ni Mpuuzi.

Eti amekasirishwa kutaniwa baada ya kunusurika kwenye ajali baada ya tairi ya basi lao kupasuka hivyo alihitaji pole na sio kutaniwa. Utani una mipaka? Kilimjaza Bumburi sio hicho. Kilichomjaza na hasira za kutaniwa kusafirisha timu kwa basi bovu lisilofanyiwa ukarabati mpaka Shinyanga huku wakijinadi timu imehama kwenye umaskini na sasa ina hiduma kama wapatazo Simba. Sasa kauli na vitendo ni tofauti. Na kusafiri na basi huwezi kuficha. Hivyo kutaniwa kwenye hili ndiko kuliko mjaza na akakosa majibu. Akaamua kuwa Mpuuzi.

Manara anajua utani na ndio maana mpaka leo hajawahi kuitwa au kushutumiwa popote kuwa anatakiwa kujibu kauli zake. Zaidi tu ya Wanayanga kumchukia na kusema anaisema timu yao vibaya. Hivi mlitaka Manara aisema Yanga vizuri? Au mlitaka Manara asiitaja Yanga? Si Manara tu hata Mimi nikipata nafasi ya kuikejeli Yanga na kuwashusha thamani nitafanya hivyo.

Niwakumbushe baadha ya utani Yanga waliowahi kuwafanyia Simba na hakuna aliyewahi kuwatukana.

1 Miaka ya 1990 waliwahi kuja na shanga pale Uhuru wakaturushia kwa marundo wakidai Simba tunafuga mashoga na hakuna aliyewatukana bali tuliishia kucheka.

2. Jery Muro aliwahi kusema Yanga ya Manji itainunua Simba na kupeleka wachezaji wake wote wakacheze soka la ufukweni. Hakuna aliyewaporomoshea matusi bali tulicheka tu.

3. Yanga hawa hawa kupitia kifo cha Marehemu Mafisango tena kupitia msemaji wao waliwahi kutuambia tumekula fedha za rambi rambi na hatuwezi kuwa mabingwa mpaka turudishe rambi rambi hakuna aliyepaniki na kuwaporomoshea matusi.

4. Hawa hawa tulipopata ajali tukitokea Dodoma na kumpoteza mpendwa wetu bado walitutania kwamba ajali ile ilisababishwa na matunguri tuliyobeba na tumemtoa kafara ili tutwae kombe la Fa. Hakuna aliyewaporomoshea matusi.

Kinachowauma Yanga wote sio ajali ni kutaniwa mambo yanayoakisi ukweli na wanaona kabisa washazidiwa mno na hawana majibu hivyo wanakimbilia kwenye matusi. Ni kawaida ya mtu yeyote dhaifu akiidhiwa hoja hukimbilia kwenye matusi.

Kwa hili Bumbuli amejidhalilisha, ameidhalilisha klabu yake na amedhalilisha mashabiki wote wa soka nchini. Anatakiwa ajitafakari kama kweli ana wazazi na amelelewa katika maadili ya kitanzania. Au ni mtu wa aina fulani ila huwa anafanikiwa kuficha tabia zake halisi na sasa ameoneka Bumburi halisi na sura yake ndio hiyo.

Vyovyote iwavyo na kwa namma yoyote hakuna namna yoyote ya kuhalalisha matusi ila lugha nzuri ya mtukanaji daima ni PUNGUANI NA MPUUZI.
Kalia tako moja FC.
 
Si ndio utani wenyewe?
Utani ni mila na desturi ya waswahili!Huhitaji cheti cha form four kujua hili!Unataka uzungu kwa timu za Simba na Yanga?Utani huu ndio unanogesha mpira ila siyo matusi na kumu attack mtu personally.

Kuweni waungwana kama utani hamuuwezi kwa nini msibaki kushabikia taarabu?

Back
Top Bottom