Kwa mara ya kwanza nashuhudia unga bei juu kuliko mchele

Jul 31, 2014
20
9
Jamani wadau na wakereketwa JF,

Kama uliwahi kushuhudia hili jambo sio miaka hii ungali sasa bei juu kuliko mchele sijui tunaelekea wapi au wapi tumekosea. Au ndio falsafa ya kuwa ukitaka kumtawala binadamu lazima umtie njaa ili akusikilize.

Ni hayo tu
 
Mambo mengine tujiongeze, hili linatokana na uhaba wa chakula na hakuna aliyeficha chakula.
Mikoa mingi haikupata mvua za kutosha, ulitegemea iweje?
 
Jamani wadau na wakereketwa Jf kama uliwahi kushuhudia hili jambo sio miaka hii ungali sasa bei juu kuliko mchele sijui tunaelekea wapi au wapi tumekosea. Au ndio Falsafa ya kuwa ukitaka kumtawala binadamu lazima umtie njaa ili akusikilize. Ni hayo tu
Peleka kwenye siasa huku hatujadili hizo ishu unless uiframe iendane na maudhui ya huku. Kutaja tu bidhaa ya kilimo so kigezo tosha cha topic kuwa huku..
 
Acheni siasa, sababu ya unga kupanda mbona kila mtu anaielewa.
Vijana hii inabidi tuchukue kama fursa wengi tujiingize kwenye kilimo. Bei zitapoa tu.
 
Jamani wadau na wakereketwa Jf kama uliwahi kushuhudia hili jambo sio miaka hii ungali sasa bei juu kuliko mchele sijui tunaelekea wapi au wapi tumekosea. Au ndio Falsafa ya kuwa ukitaka kumtawala binadamu lazima umtie njaa ili akusikilize. Ni hayo tu
Mbona kama umerukwa na akili kidogo. Ukame unahusishaje na falsafa Je Kenya Yemen na Malawi wanaopelekewa mahindi na UN watasemaje?
 
Mambo mengine tujiongeze, hili linatokana na uhaba wa chakula na hakuna aliyeficha chakula.
Mikoa mingi haikupata mvua za kutosha, ulitegemea iweje?
Ugeni kwenye hili ndio unawasumbua,ukweli ni kwamba bado serikali hapa ina sehemu ya lawama.

Hivi ni nani asiyefahamu kwamba ukimwi hauna kinga?Hivi ni nani asiyefahamu kwamba 90% ya maambukizi ya ukimwi chanzo ni zinaa ambayo inaepukika?Sasa kwa msingi huo serikali wanahangaikia nini kupoteza mabilioni kwenye ARV wakati watu hawataki kuacha zinaaa?
Mfano huu ugeuzie kwenye mahindi utaona uhusika wa serikali.

Kwa wasiofahamu awamu zote zilizopita Ben na JK walizingatia sana kuhifadhi vyakula kwenye maghala ya taifa na walikitoa kwa vibali kwa bei nafuu kuuzia wafanya biashara pale panapotokea dilili za mfumuko wa bei.

Mwaka jana serikali ilipuuza kuhifadhi chakula na haya ndio madhara yake.Sio kweli kwamba mwaka jana mavuno yalikuwa machache kiasi cha.serikali kushindwa kununua mahindi kwa wakulima na kuhifadhi kwani mpaka mwezi wa tisa serikali ilifungua mipaka mahindi mengi yalivushwa kenya wakidai taifa linachaka.cha.ziada
 
Back
Top Bottom