Kwa mara ya kwanza Kova kawa mstaarabu, wengine ngunguri igeni

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,753
7,075
Wana JF,

Kwa kweli Kova ametumia fursa hii vizuri kutoonesha munkali wa vitisho tulivyo vizoea baada ya kusikia umati wa watu wanaojiaandaa kumsindikiza Lowassa wamejaa Buguruni kusubiri rais wao /wetu mtarajiwa, Kova baada ya kuwasha mic katika redio ya clouds kuzuia msafara wa wasindikizaji na kuwataka kutumia barabara moja tu kwa kusema kwamba mgombea ni wa CHADEMA, huko Buguruni kwa CUF hakuna ruhusa, lakini baada ya kuambiwa kuna nyomi inatisha kaamua kuwambia kuwa haya nimeruhusu lakini muwe waangalifu msilete fujo.

Msafara umefanikiwa kwa kiwango kikubwa, hata CCM wengi walikuwepo ambao wiki ijayo wanajiunga rasmi kwenye boti kubwa ya SAFINA.

Angalu polisi wamerudi na virungu vyao havijaonja mtu, hata vibaka walitulia sana.
 
Zamani walidhani opposition ni maigizo sasa wanaona kumbe kweli
 
Mbowe alisema kuwa Lowasa ni Boss wao ,pengine wamemheshimu ,wamesaliti agizo la kuzuia mkusanyiko haramu.
 
Nilitarajia kusikia yakisemwa kwamba Kova pia amenunuliwa na EL, Badala yake lugha imebadilika (na kua Kova kawa mstaarabu). Kweli kiswahili kimekua aiseeee.....
 
akimpiga mabom rais wake mtarajiwa, akishaingia ikulu yeye na familia yake na mali zake watakimbilia wapi? unafikiri hawajui? wao wenyewe wanatamani wasingekuwa kwenye hizo nyazifa zao ili waungane kwenye maandamano kumuunga lowasa, wamevaa magwanda wanaogopa wakifanya hivyo tu watapigwa tu, ila kiukweli hakuna mtz mpenda mabadiliko ambaye anampinga edo.
 
Polisi ni vijana wa lowassa! Security System ya nchi ipo mikono mwa Lowassa! Trust me!
 
Kova amesoma upepo anatetea kibarua chake,anaelewa Lowassa hazuiliki kuingia IKULU!
 
Sasa ule umati utaanzaje kuutawanya haswa?? ni kuwaachia tu..police ndio wanaoanzisha fujo siku zote
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom