Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Jana kuna matukio mawili makubwa ya kitaifa yalikuwa yanaendelea nchini. Jijini Dar es Salaam, kikao cha Dharura cha Kamati Kuu CHADEMA kilianza ambapo kitafanyika kwa siku mbili yaani Julai 23 hadi 24.
Mjini Dodoma, Chama Cha Mapinduzi kilikuwa na Mkutano Mkuu Maalum ambapk Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Jakaya Kikwete alimkabidhi Mikoba Mwenyekiti Mpya, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli.
Lengo la CHADEMA kuitisha kikao cha Dharura cha Kamati Kuu siku ambayo CCM inafanya uchaguzi wa Mwenyekiti lilikuwa ni kwanza kabisa kuteka headlines za magazeti na vyombo vya habari. Siku zote CHADEMA wanajinasibu kuwa wao ndio wanapendwa na inapotokea wakafanya matukio pamoja basi ni taarifa za CHADEMA ndizo hupewa kipaumbele.
Nimepitia magazeti yoye hakika taarifa za CCM kwa ujumla wake zimetawala. Kila gazeti limeandika kwa ustadi wake lakini kwenye habari kuu lazima utaona jina la Kikwete, Magufuli na CCM. Pia rangi za kijani na njano zimetawala kwenye magazeti yote.
Kilichoniacha mdomo wazi ni hili tukio la Gazeti la Mbowe kuupa kisogo Mkutano wa CHADEMA na kulipamba gazeti na habari za CCM. Naona sasa wameona bora kufanya biashara kuliko kutumika kukiuza chama ambacho hakiuziki. Ka dhati ya moyo wangu niwapongeze Tanzania Daima kwa kubadilika. Japo Taarifa kuu ilikuwa na lengo la kumpamba Lowasa, ila kiukweli mwonekano wa gazeti hilo kwa siku ya keo umeniacha mdomo wazi.. Lazima tuheshimiane