Kwa mara ya kwanza bei ya mahindi iko chini kuliko kipindi cha mavuno, ni kilio kwa wakulima na wafanyabiashara

Huu uzi umenitisha. Jana tu nilitaka niwezeke senti zangu kwenye kilimo cha mahindi. Nilitafuta na shamba la kukodi kabisa kama bahati nimeambiwa pale hapafai pako pengine pazuri zaidi.

Kwa hali hii ulioielezea nimeghairi bora nikawekeze sehemu nyingine
Kweli mkuu sasa hiv mambo imekaa vibaya kuliko kulima mahind ni bora kununua na kuuza utaona faida
 
Wee Jamaa punga kabisa, kichwa cha panzi ubongo wa mende unataka gunia liuzwe milion haraf sisi wa chin ya dola moja kwa siku tufe njaa, kwanza mahindi sio zao la biashara, wapandishe bei mazao kama pamba, kahawa, korosho nk, bora ungeingia na thread za kutunga (story) kama na ww unataka uonekane umo JF kama kina Money Penny na Beira Boy hapo kwenye mahindi unagusa uhai wa watu!

Wewe sio mzima ukishanunua kwa bei ndogo ukamtia hasara mkulima msimu ujao hawezi kuwa na nguvu ya kulima tena na wewe tegemea kufa njaa.
 
wewe ni mwehu nini chakula kuwa bei ya chini ni kilio?
Mkuu kwani ni lazima mtoa mada umwite mwehu wakati amejaribu ktuoa maoni yake? Wewe huwezi kutoa maoni yako bila kumkashifu mwenzio?
Anajenga hoja kwamba mwisho wa siku wakulima hawataweza kugharamia shughuli za kilimo na hivyo hata walaji hawatapata chakula hata kwa bei kubwa kwasababu watafilisika!
 
Mpiga dili huyo! Hata hajui kuwa bei ya staple kuwa chini (food security) ni mojawapo ya kigezo cha kuimarika kwa uchumi wa nchi! Mleta uzi alitakiwa afurahi badala ya kusikitika na kulaani kushuka kwa bei ya mahindi.
Wengi hapa si wakulima Ndio maana mwachangia kwa kuudhi.
Mimi nimeiza jana gunia 25 kwa shilingi 625,000/- Sawa na 25,000/- kwa gunia. Mahindi Haya ningeuza Mara nilipovuna junk ningepata 1,000,000/- tena bila ya kuingia gharama za ubebaji na uhifadhi. Mwaka huu nimelazimika kupunguza kiwango cha kulima. Changieni mjuavyo lkn inaumiza Sana.
 
Tanzania bora tunayoitaka, hata wabunge wenyewe, ni ile food secure ambayo bei za vyakula ziko chini. bei za pembejeo zita-follow suit, nazo zitashuka pia. Huo ndio uchumi bora tuliousubiri kwa siku nyingi sana. Kama watu wanasema hakuna pesa mifukoni, kushuka kwa bei ya chakula na bidhaa nyingine ni ishara kuwa uchumi unaimarika kuelekea uwezo wa watu kununua bidhaa (purchasing power) na kisha sarafu yetu kuimarika. Huo ndio uchumi.
Nani kakwambia kuwa bei za pembejeo zinashuka?

Hizi ni stori za vijiweni huko Sinza hamjui yanayoendelea mashambani kwa wakulima.

Mkulima anaumia sana.
 
Mkuu kwani ni lazima mtoa mada umwite mwehu wakati amejaribu ktuoa maoni yake? Wewe huwezi kutoa maoni yako bila kumkashifu mwenzio?
Anajenga hoja kwamba mwisho wa siku wakulima hawataweza kugharamia shughuli za kilimo na hivyo hata walaji hawatapata chakula hata kwa bei kubwa kwasababu watafilisika!
mimi nijuavyo kipimo cha uchumi wa nchi kustablize ni bei ya chakula kushuka, waanzishe vikundi ili waweze kusafirisha nchi za nje kuliko na njaa serikali isharuhusu.
 
Unakodi shamba kwa laki mbili ekari moja, kulima kwa tractor elf 50, mbolea ya kupandia mfuko mmoja elf 50, ya kukuzia elf 50 na ya kuzalishia elf 50, vibarua kupalilia kwa palizi mbili laki 1. vibarua kuvuna pamoja na kupiga mahindi elf 50. mifuko ya kuhifadhia mahindi mfuko mmoja elf 4x mifuko 10=40. gharama nzima ya kuhudumia ekari moja ni laki 5 na nusu nakuja kuvuna magunia 15 kila gunia nauza kwa elf 30 napata laki 4.5 Kwa maisha haya si bora nikapige debe kituo cha mabasi ya mikoani ubungo
 
pamoja na kufurahia mahindi yapo ni ni bei nzuri kwa sisi wengine lakini agenda kuu labda ingekuwa je hawa wakulima wataweza kulima kwa mwaka huu kama watauza mahindi waliyopata mwaka jana kwa hasara? na Je, ni kweli ni kwa hasara? Maana lazima serikali iweze kubalance pande zote yaani mkulima afaidike na mnunuaji naye afaidike
 
Mpiga dili huyo! Hata hajui kuwa bei ya staple kuwa chini (food security) ni mojawapo ya kigezo cha kuimarika kwa uchumi wa nchi! Mleta uzi alitakiwa afurahi badala ya kusikitika na kulaani kushuka kwa bei ya mahindi.

Achana naye huyo. Hajui kuwa one of the reason ya umasikini ni pamoja na food insecurity.
 
mimi nijuavyo kipimo cha uchumi wa nchi kustablize ni bei ya chakula kushuka, waanzishe vikundi ili waweze kusafirisha nchi za nje kuliko na njaa serikali isharuhusu.
Elimu ya uchumi imekupitia mbali sana kijana, huwezi shusha bei ya mazao kwa kutegemea gharama za mkulima halafu useme huko ni kukua kiuchumi labla uchumi wa huko kwenu, serikali itoe ruzuku kwa wakulima waweze fidia hasara yanayopata kwa kushusha bei za pembejeo.
 
wewe ni mwehu nini chakula kuwa bei ya chini ni kilio?
Vipi wewe, umenusurika kusombwa na maji Jangwani au? Mbona mkali vile? Huyo ni mkulima, unazijua pembejeo za kilimo au wewe unasubiria tu uletewe? Bei ya chini ya mahindi siyo nzuri kwa mkulima ila nzuri kwa mlaji. Mkulima asipolima wewe utapata wapi mahindi? Pambaneni na mtaro wenu wa jangwani tu.
 
Back
Top Bottom