Kwa manufaa yako.

Kwa manufaa yako.

Joined
Oct 29, 2012
Posts
86
Reaction score
4
(1)Mi mtunzi wa shairi, mwenyewe najitangaza.
Kwa utungaji hodari, mimi hapa ninaweza.
Kwa mashairi mazuri, mimi hapa ninauza.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(2).Mashairi ya mizani, vina vya kati na mwisho.
Nawatungia jamani, mkinipa hio posho.
We sema shairi gani, nitunge leo na kesho.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(3).Mashairi ya kidini, au ya hadithi fupi?
Ya mapenzi na utani, au unataka yapi?
Vichekesho burudani, we sema nitunge vipi.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(4).Mashairi ya mikasa, naweza kukutungia.
Au yale ya siasa, hayo yote nayajua.
Kwa kiasi tu cha pesa, kazi ninakufanyia.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(5).Ukitaka jiliwaza, shairi zuri nakupa.
Mawazo utapoteza, haki ya Mungu naapa.
Anza kujieleza, shairi niweze kupa.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(6).Kwa shairi la mapenzi, kwa yule umpendae.
La zawadi na pongezi, rafikio ashangae.
Gharama ni maongezi, we mwenyewe niambie.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(7).Ukitaka kunipata, ni rahisi tena sana.
Ubeti unaofwata, namba inaonekana.
Utapiga itaita, tuweze wasiliana.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.

(8).Andika sifuri sita, kisha fwata tano tatu.
Nne mbili yajikita, mbili saba roho kwatu.
Saba tena kisha sita, wanipata mimi mtu.
Kama wataka shairi, nilipe nikutungie.
 
Back
Top Bottom