Kwa mambo haya, ni vyema tukajifunza kwa wachaga

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Nianze kwa kusema mimi sio machaga Wala sitokei kanda ya kaskazini.

Kilimanjaro Ni mkoa ambao ukifika mjini unaweza kusema umebaki nyuma kimaendeleo. Ukijitahidi nenda maeneo ya vijijini, utaona kila mahali Kuna umeme, maji, migomba, ng'ombe au mbuzi na na hata kakibanda ka biashara

Nimejaribu Sana kufuatilia maisha ya Hawa watu. Nimeona tushukiriane. Pamoja na mapungufu wanayoweza kuwa nayo Haya Ni Mambo yanawafanya wachaga waendelee

1. Mfumo wao wa urithi. Mchanga akiwa na watoto hasa wa kiume lazima awarithishe ardhi. Hata tukija kwenye vitabu vitakatifu, ardhi ni urithi wa kwanza aliopewa mwanadamu. Hii imefanya kila mtu awe anelaendeleza pale alipopewa maana huwa ni aibu wenzako wanajenga alafu wewe umeweka shamba.hii ndio sababu Kilimanjaro kila sehemu nzuri. Sehemu zingine watu ni kuzaa bila hata kujua mtoto atapata nini au utamuachia nini.


2. Wachagga wengi wanathamini sana elimu. Ni vigumu sana kumkuta mchanga hafikirii kupeleka mtoto shule. Kuna dada nimemuona anafanya kazi ya kukusanya pesa vyoo vya manispaa hapa dar. Huyu dada anasomesha mtoto wake shule nzuri na anajitahidi kweli.taifa haliwezi kuendelezwa na wajinga. Adui mkubwa kwa nchi zetu hizi ni ujinga. Ndio maana watu wako tayari kuacha matibabu na kwenda kwenye kikombe au mahali pengine.mtu toka asubuhi anaangalia habari za free mason na anaona amejua sasa sijui akijua hayo mambo yanamsaidia nini. Hawa jamaa kutoka na elimu wako kila mahali na wanajitahidi kweli kujituma kutafuta pesa na mali. Makabila mengine tuige hii kitu. Kuna makabiliano kuoa wake wengi ni sifa bila hata kujali damu yao italelewaje

3. Wachaga wanathamini sana damu yao. Ukitaka kuthibitisha hili mpe mimba mtoto wa mchaga. Wazazi watachukia sababu ya aibu lakini watamsaidia mtoto na kulea yule mtoto. Wengi wa wachaga watachukua yule kiumbe na kumwendeleza mtoto wao kufikia malengo. Angalia makabila mengine, mtoto atalazimishwa kuolewa na kukimbia shule. Angalia rafiki zangu wamatengo kule mbinga vijijini. Kuna umuhimu wa kujifunza kwa hawa watu kabisa.
Lakini pia pia hata kunyenyuana hawa jamaa hawaachani.

4. Wachaga sio watu wanaopenda masifa sifa sana. Yaani ukikuta mchaga kanunua gari nzuri ujue account yake inasoma vizuri kwa kweli. Sasa msikilize baba cocku. Yaani hata akiwa na baiskeli atajinyenyua sana.
Wachaga hawapendi kuabudiwa..yaani ukimfanyia kazi atapenda na wewe uinuke. Njoo kwa wajomba wanyaki, yeye anataka akipata wengine mumuone kama mtu special sana.hawa jamaa wanasaidiana sana, angalia biashara zao.

5. Wachaga hawanaga imani za hovyo hovyo. Ebu angalia maeneo kama mbeya. Eti wanatafuta mtu anaitwa lamba lamba kufukuza wachawi vijijini. Watu wanatumia masaa kadhaa kuhangaika na maimamu ambayo hayaleti maendeleo. Mara kupiga NONDO watu, mara kkuchuna ngozi, mara matukio kibao.Watu ni ushirikina wanasahau kusoma na kufanya maendeleo. Sehemu zenye imani nzito za kishirikina mara nyingi utakuta maendeleo yao duni. sana. Angalia hata uchagani maeneo ya uru wanakoamini ushirikina utakuta hata maendeleo yao sio sawa na wengine kama, Machame, marangu,rombo, na hata kibosho.

6. Pia ni watu wa kukumbuka fadhila. Mimi nimewahi kumsaidia jamaa mmoja mrombo. Nilimsaidia kukunua uwanja mzuri dar. Baada ya kumaliza kazi ambayo nilifanya bila intention ya kulipwa maana alikuwa rafiki yangu. Jamaa alipona nimeamka ishi hati ikiwa kamili alinipa million tatu ili niongeze ninunue na mimi plot. Hawa jamaa wanapenda maendeleo sana na sio wabinafsi. Sasa Kutana na watani wangu waha. Piga kazi uwezavyo lakini utaishia kupigwa Majungu tu. Sio wote jamani. Tuwaige wachaga.

7. Wanawake wa kichaga ni watafutaji balaa. Wanafanana na wanawake wa kinyakyusa. Yaani hata umwachie watoto ili mradi umempa mji atalea familia. Sasa pata wale wenzetu wa ngoma. Wao ni kumuombea mzazi afe ili wauze nyumba wagawane pesa wakatanue kwenye ngoma. Tujifunze kwa wenzetu wachaga.
8. Wachaga wakiona unafanikiwa baadala ya kutafuta uchawi wakuroge watakuja kukuuliza mbinu. Mimi niliwahi kufuga kwao. Walipoona mifugo yangu inafanya vizuri wanakijiji wengi walikuwa wakifika kuniomba niwafundishe ninavyofanya.
Ukienda sehemu zingine utapata Majungu na visa kibao. Ndio maana hawaendelei.

Nimezunguka sehemu nyingi kutokana na kazi yangu, lakini hawa wachaga wana kitu cha kujifunza sisi tusio wachaga
Tujifunze kwa wachaga. Kumchukia mwenye nacho hakukufanyi upate. Jifunze kwa wenye nacho na waliofanikiwa na waliokuzidi.
 
Hawa Watu Bila Unafiki Ni Kama Wamebarikiwa Kuanzia Mlima Kilimanjaro, Uoto Mzuri Wa Asili, Hali Nzuri Ya Hewa, Uzuri Watoto Wa Kike, Elimu, Utajiri Na Maendeleo Kwa Ujumla.

Kuna Siri Niliwahi Sikia Walitaka Kufanya Nchi Yao Huko Moshi Ila Nyerere Alishitukia Mpango Wao Ukabuma.

Baya Lao Moja Ni Wapo Kwa Kasi Kwenye Mambo Ya Kina James Delicious. Mwenye Kujua Sababu Anijuze Kwanini?
 
Nakubaliana na hilo mkuu,nimekaa babati mitaa ya majengo mapya nimekaa Arusha kwa Morombo na njiro pia nna week moja tu nilikuwa kirua-vunjo pia nimepita pita sana Marangu,Himo wamejitahidi sana tofauti na sehemu zingine Tanzania nzima,hawa jamaa hawana(ga) wivu wa kipumbafu labda tatizo la wizi na ulevi vimekithiri sana hadi vijijini ndani ndani
 
Wanaowachukia wachaga ni sababu ya ujinga wao. Wachaga wanajihusisha sana. Yaani hata ukiwa kwenye mahusiano na mwanamke wa kichaga anakupush sana kufanya maendeleo
Najua kuna hili wimbi la kuwachukia wachaga out of no where. But ukweli wanaujua kuwa hawa jamaa ni watafutaji kweli. Mchaga hachezi na muda hata siku moja. Hapotezi nafasi pale anapoipata . Toka wadogo wanajengewa mentality ya utafutaji.
 
Tatizo lao sio waaminifu na kupenda nyama. Kuanzia usafi. Kazi. Elimu wako juu.
 
Hivi ni kweli wanathamini sana pesa kuliko utu, ukiwa na mali mwanamke anakudedisha. Vipi kuhusu kwenda kufanya matambiko kila mwisho wa mwaka, hii kitu ni kweli? Anyway, tuwapongeze na tuige mazuri yao
 
Mzee,soma alama za nyakati wachaga wasaiv ,si saw na wachaga wazamn.wachaga wa saiv,ni shidaah tupu.ni wachache San,wap hvo
 
Mzee,soma alama za nyakati wachaga wasaiv ,si saw na wachaga wazamn.wachaga wa saiv,ni shidaah tupu.ni wachache San,wap hvo
Kama ametoka uchagani kabisa. I mean amekulia mazingira ya uchagani. Kijijn au moshi kabisa huyo atakuwa mtafutaji. Lakin hawa wachaga wa kuzaliwa mjini hamna jipya
 
AF ,mtoa Maada.mbna,km ww n mchaga,uliepat kuish mbeya.unaunafiki mwingi sana,kwa kuwachukia wanyaki.
 
Mm nipo hapa nakunywa pombe ya maindi inaitwa dadii tam sana hii kitu ukinywa tuu hauhic njaa
 
Back
Top Bottom