makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 37,570
- 108,900
Wee wa mjimwema eeehh
Kama kuna kitu huwa naishangaa serikali na intelijensia ya polisi ni kuhusu ardhi.
Leo hii anapatikana mtu kama huyu, anaweka matangazo ya kuuza ardhi, tena kwenye media kama hivi na watu wanajitokeza kununua na serikali za mitaa/vijiji zinaweka mihuri. Miaka 5/10 mbele, unasikia sokomoko la kufa mtu kwamba hawa watu wametapeliwa, ardhi ni ya mtu mwingine au ni hifadhi au pori la akiba, au hata mali ya mwekezaji. Hii inayoitwa intelijensia sio kazi yake kuzuia yasitokee?
Nasema hivi kwa kuwa, serikali yenyewe ipo nyuma sana kwenye kupima viwanja na mashamba. Watu wanaposikia wito kama huu lazima haraka watawahi huko. Sasa wao wanakuwa wapi?
Kule Bagamoyo, kundi la watu linauza viwanja kuanzia Mapinga hadi Bagamoyo. Matukio ya watu kutapeliwa ni zaidi ya 80, lakini sijasikia mitego wala ukamataji wa watu hawa...sana sana wanaishia kutoa tahadhari, sasa mwananchi atamtambuaje tapeli ikiwa serikali za mitaa zinahusika?
WE BWANA KAMA HAYA MASHAMBA UNAYOUZA SIO YAKO, MUNGU NA AKULAANI, ila kama ni ya kwako ukiuza usinisahau hata laki moja