Kangosha
Senior Member
- Sep 18, 2023
- 139
- 266
Katika kipindi cha awamu ya tano na ya sita kuliibuka viongozi na machawa ambao kila maendeleo yaliyofanyika walikuwa wakisema kuwa kafanya Rais pasipo kumgusa mwananchi ambaye kodi yake ndio imetumika.
Yaani kila mradi utasikia mtu anasema Mh Rais ametoa bilioni kazaa kwa ajili ya mradi huu, yaani utadhani kilichofanyika ni hisani na wala sio haki ya mwananchi.
Ujinga huu ulizidi kushamiri kwenye awamu ya sita. Nashauri viongozi wa awamu ya sita kwenye ungwe ya pili wabadilike katika hili.
Angalieni namna ambavyo mtaonyesha kwamba mradi fulani umetekelezwa kwa juhudi za wananchi kulipa kodi. Waambieni kuwa barabara na vituo vya mwendokasi ni mali inayotokana na kodi zao na sio Rais katoa hela kujenga hiyo miundombinu.
Waelezeni kuwa miradi ya visima na barabara inafanywa au imetekelezwa kwa fedha zao. Wasisitizeni kuwa wanavyokuwa wanaharibu ni kwamba wanaharibu vitu ambavyo vimejengwa kwa fedha zao.
Leo hii unakuta jichawa linamsifia Rais kuwa ndiye ametoa hela ya mradi fulani pasipo kumgusa mwananchi ambaye kodi yake ndio imetumika. Rais anatakiwa tumsifie kwa kusimamia na kupanga vizuri matumizi ya kodi zetu.
Tukifanya hivi kwa kiasi fulani itapunguza uharibifu wa mali za umma na kuongeza morali ya kulipa kodi.
Nawapongeza sana TRA kwenye tangazo lao linalorushwaga kwenye mechi za live Azam TV.
Wao hueleza kabisa kuwa tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi na huonyesha miradi ambayo imetekelezwa kwa kodi zetu.