Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,162
- 3,162
Wako Watanzania wasiojua uhalisia
Tanzania kama nchi inaelekea kuwa na watu milioni 50. Kati ya hao, walipa kodi hawafiki hata milioni tatu, yaani kundi la watu milioni tatu ndilo linaendesha maisha ya watu milioni 50 kwa afya, miundombinu, maji nk. Maana Watanzania wengi ni walima mihogo na mahindi ya kujikimu, hawana pa kuwakamata ili walipe kodi. Kundi lingine ni vijana jobless waliomaliza vyuo vikuu, sekondari na Shule za msingi, hawalipi kodi zaidi ya kuwapiga vibomu ndugu zao wawape hata nauli.
Kwa misingi hiyo, ni ujinga kusema eti msaada wa mzungu hauhitajiki, unahitajika sana, ndio tuko na maliasili, utalii, lakini vyote hivi vime prove kuwa bado havijafika level ya ku support budget kwa 100%. Kwa kifupi, kujitegenea bila viwanda tunajidanganya.
Kwa kusema hayo, kigezo kikuu cha mzungu kutoa msaada ni demokrasia, ndio hivyo sasa kuanzia mwenyekiti wa kitongoji hadi wabunge, kwa fitina za kila namna wamehakikisha ni ccm wote. Hivyo, Inaelekea Wapinzani watawaandikia umoja wa Ulaya, Marekani kuhusu hali ya kidemokrasia nchini.
Tena wataandika huku wakiweka vielelezo vya mabox fake ya kura, damu za watu nk.
Hivyo, hali itakuwa mbaya kwa wafanyabiashara, wafanyakazi maana mzunguko wa pesa hautakuwepo. Tutegemee mbinyo ambao haukuwahi kutokea, Tutegemee anguko la thamani ya pesa nk.