Kwa kina dada tu

ramadhani kimweri

Senior Member
Apr 22, 2016
165
169
SPECIAL KWA WADADA

Umepata Bwana, Umempenda Kweli kweli na Umemlalamikia Sana Eti Kwanini Hakupeleki Kwa Wazazi Wake Kukutambulisha, Jamaa Akagoma Sana mwishowe akaona isiwe Kesi Akakupeleka

Wewe badala hata utake hiyo advantage umefika tu Siku ya Kwanza Umeshinda Unachati, Siku ya Pili Umeshinda Unachati Tena ndio unajisifia kwenye groups upo ukweni Kumbe Wao Wanakutazama Tu na kukupimia Wala Hawakwambii Kitu

Siku ya Tatu Wanakwambia Leo Ni Zamu Yako Kupika, Unaingia Jikoni unaona Kila Kitu Kigeni
Vya Huku Unaweka Kule, Vya kule Unaweka Huku (Yaani Hujui Kupika Chochote)

Sufuria Unashika Kama Umeshika Power Bank, Unapika Na Lipstick, Mdomo Mwekunduuu Utafikiri Mtoto wa Jini Katoka Kufundishwa Kunyonya Damu tena huku Umevaa Saa, Umevaa Culture Zimejaa Nusu Ya Mkono, Umevaa Mini Skirt Kama Wafanyakazi Wa Emirates

Msosi wa Wakwe Huwezi Kupika. Ukiambiwa Hufai Kuolewa Unavuta Mdomo Utafikiri Umenyimwa USB Cable Ubust Smartphone Yako
Unaanza Kulalamika Wakwe Hawakupendi, Unalalamika Weee, Unashindwa Kuelewa Kuwa Wewe Ndo Tatizo.

Usitake Kuolewa Ukidhani Mumeo Atakula Chips na Wewe Utakuwa Utakula Pizza Kila Siku, Jifunze Hata Kuchemsha Chai Basi Au Unadhani Google Wataleta App Ambayo Unaweka USB Kwenye Simu Yako Alafu Unaielekezea Kwenye Sahani Inaproduce Msosi

#JIPANGE DADA Usidhani Ndoa Ni Kama Kupiga selfie
IBN KIMEERI
 
Baeleze baelewe. Sorry kumbe ni kwa wadada tu, kwaheri
 
Heheheeee....unaeza ukajipikilisha na ukanangwa vile vile
 
Hii ni taarifa bora kwangu tangu huu mwaka uanze. Na kama waandishi wa hapa JF mngekuwa kama huyu mgosi Kimweri hili lingekuwa jukwaa bora duniani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom