MGILEADI
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,621
- 1,543
Kikosi kizuri ila mpira kitu kingine aisee. Timu inaweze ikawa nzuri ila makosa madogo kabisa yakaigharimu timu mazima. Au unaweza kuta timu nzuri ukashangaa wanapoteana.
Kabisa! Siku hizi saikolojia ina nafasi kubwa sana kupata ushindi. 1998, Brazil alipigwa na Ufaranza 3-0 kutokana na mfadhaiko alioupata Ronaldo siku moja kabla ya mechi. Hali hiyo ilivunja morali ya timu nzima. Wafaransa baada ya Zidane kutolewa waliishiwa nguvu wakapoteza kombe kwa Italia. Masserati beki wa Italia inawezekana alimuudhi Zidane makusudi ili afanye faulo atolewe. Huwezi kujua mambo haya ya mpira wakati mwingine.
Kadhalika majuzi mwaka 2014 mbele ya Uerumani, kocha wa Brazil, Scolari alipaniki sana baada ya Thiago Silva kupewa kadi ya pili ya njano na hivyo kutolewa na kukosa mechi ya fainali. Hii ikitokea baada ya tegemeo lao Neymar kuumia. Hatujui kama ile umizwa ya Neymar ilikuwa ni ya makusudi ama lah! Lakini Brazil walikwishatolewa kwa matukio hayo mawili kambini mwao. Scolari alihangaika kuziba mapengo hayo mawili na wapinzani wao Ujerumani wakapanga mchezo wakijua msumbufu Neymar hayupo.
Nakumbuka Romario mchezaji wa Brazili akiichezea Barcelona miezi michache kabla ya kombe la dunia kombe la Mabingwa. Hakucheza kabisa "akiogopa kuumizwa na wajanja" timu yake ikilalal goli 5-0 na timu nadhani ya AC Milan. Lakini baadaye tuliona wote makali yake Marekani mwaka 1994 ambapo walilibeba kombe.
Wapenzi wa Brazil waombe Neymar apone kwani bado ni tegemeo kubwa sana ingawa inaonekana Brazil walpata funzo mwaka 2014. Kwani ni dhahiri kuwa wanaweza kucheza bila Neymar na wakashinda. Ila kisaikoloia bado itawasumbua wakimkosa.
Ni kweli mpira hautabiriki.