Kwa kheri Profesa Muhongo, mwanamiamba mwamba.

Kyampisi

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
265
187
Nipende kumpongeza mh rais John Magufuli kwa jitihada zake za dhati kabisa anazozifanya kuhakikisha watanzania tunanufaika na rasilimali zetu.

Nchi hii ina kila aina ya tunu kiongozi akiwa na roho nzuri kwa watanzania pamoja na uthubutu usio na woga hakika Tanzania itakuwa ya tofauti kabisa.

Tunaibiwa sana.

Muhongo ni profesa ambaye binafsi namkubali sana, alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa waziri wa nishati,

kulikuwa na hali ngumu sana ya umeme alipoingia mambo yakawa mazuri.

Kwa bahati mbaya Escrow ikamwondoa, akaja Simbachawene, hakufanya vizuri kwa kweli, hali ilikuwa mbaya,

yalikuwa ni mateso, redio wiki nzima zimekata, umeme unawaka wastani wa masaa 5 kwa siku, kupata maji ikawa shida,

ofisi za umma zilizokuwa hazina ma genereta huduma zikazorota n.k, n.k.

Urejeo wa Muhongo awamu ya tano ukarudisha faraja, hakufanya kazi ili atokee kwenye kurasa za mbele,

Alifanya kazi kwa ajiri ya umma.

Mbali na TANESCO kuwa na changamo kibao amejitahidi kuhakikisha tunapata umeme wa uhakika.

Kwa huku niliko umeme unawaka hata siku 5 bila kukatika hata nukta, mpaka hapa haya ni mafaniko.

Ameacha hali ikiwa nzuri (kwa huku ninakoishi)

Kwa huyu atakayekuja asije akaona kwa kuwa huyu kaondoka kwa kukaa kimya, akaacha kufanya kazi akaanza kutafuta kiki za kumridhisha mh. rais.

Hii wizara ni ngumu!

Kwa mara nyingine tena umeondoka kwa makosa yasiyo yako. KWA KHERI PROF MUHONGO, MWANA MIAMBA MWAMBA!
 
Back
Top Bottom