Kwa kauli ya Magufuli leo dhidi ya Makonda,naihitaji sauti ya Lema na Lissu

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,652
2,628
Wanaukumbi

Rejea kauli ya Rais Magufuli akimtaka Bashite kufanya kazi, binafsi imenifedhehesha sana.

Ili angalau niipende tena Tanzania nahitaji Press Conference ya Mbunge WA Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Rais wa Tanganyika Law Society Tundu Anthipas Mughway Lissu,juu ya Bashite kuendelea kuhudumu ktk ofisi ya umma
 
Hii ina maana sana kwa Ccm. Mmejifunza jambo. Mlidhani mmetuletea rais wa Watanzania kumbe mmempa urais wake mwenyewe.
Sasa mna kwenda kumpa na chama chake Ccm ya Magufuli na siyo Ccm ya wana Ccm.
 
Kwa kauli ile ya kumpa kiburi Kondas, basi hata akifa atasema asizikwe tuwe tunamuonaona jinsi alivyo "mchapakodi" asiye na vyeti! We've got all the time in the world.... be patient, time will tell everything presently!
 
Wanaukumbi

Rejea kauli ya Rais Magufuli akimtaka Bashite kufanya kazi, binafsi imenifedhehesha sana.

Ili angalau niipende tena Tanzania nahitaji Press Conference ya Mbunge WA Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Rais wa Tanganyika Law Society Tundu Anthipas Mughway Lissu,juu ya Bashite kuendelea kuhudumu ktk ofisi ya umma
Hili ndilo tatizo kubwa kabisa la Tanzania yetu. i.e Wananchi wote kukaaa na kuangalia matukio ya kijinga na kizembe na yenye madhara kwao kama wanaangalia sinema ya kufurahisha. Kila mtu amekaa na anasubiri Lissu na Lema wampiganie. Yeye Kimyaa! Na wanasiasa akiwemo Magufuli wameshajua udhaifu wetu ndio maana wanaongoza kama baba mkali anayewaongoza watoto na mke wake.
 
Mheshimiwa President Tundu A. Lissu apumzike kidogo sasa kupanga upya silaha

Yeye ni Rais sasa

Aanze kama Rais

Tunakusubiri baada ya mapumziko yako, Mr POTLS

Our Hopes Never Fail!

Hiyo avatar ... imenifanya niwaze sana hadi kusahau hoja ya msingi. Ila sawa, huyo wa kwenye avatar
 
hivi kwanini Ruge asiende kumfungulia kesi huyo Makonda?
maana naona tunalazimisha watu wengine ambao hawahusiki wakamtetee Ruge wakati yeye anaweza kujitetea!
mahakama zipo kwanini asimfungulie kesi....!

ndo mana kila siku tutazidi kuonekana 4:1
 
Wanaukumbi

Rejea kauli ya Rais Magufuli akimtaka Bashite kufanya kazi, binafsi imenifedhehesha sana.

Ili angalau niipende tena Tanzania nahitaji Press Conference ya Mbunge WA Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Rais wa Tanganyika Law Society Tundu Anthipas Mughway Lissu,juu ya Bashite kuendelea kuhudumu ktk ofisi ya umma
Vipi Mange na Gwajima? Mmewatosa?
 
Kwa wenye uvivu wa kufikiri watashangilia,kuchekelea n.a. kuunga mkono msimamo n.a. matamshi ya Magufuli.Lakini kwa wanaotumia vizuri bongo n.a. akili zao watajiuliza haya:
A.Kuna watu wako juu ya sheria.
B.Utawala wa sheria ni ndoto chini ya awamu hii?
C.Utii wa sheria ni hiari n.a. si lazima.(kuchagua unafuu kwa masilahi binafsi)
D.Wenye nguvu n.a. mamlaka kufanya watakavyo!
E.Mahakama,vyombo vya usalama majaribuni.
HIVYO: Tutegemee hali ya kukosekana kwa ustaarabu, viongozi kukengeuka, vitendo vya uvunjifu wa amani kutamalaki, raia kutokuwa n.a. imani n.a. vyombo vya maamuzi.
MADHARA: Tutafakari pamoja .Lakini ni ishara mbaya ya mengi yatashuhudiwa.
 
hivi kwanini Ruge asiende kumfungulia kesi huyo Makonda?
maana naona tunalazimisha watu wengine ambao hawahusiki wakamtetee Ruge wakati yeye anaweza kujitetea!
mahakama zipo kwanini asimfungulie kesi....!

ndo mana kila siku tutazidi kuonekana 4:1
Unajua kitu kinaitwa tax notification
 
Back
Top Bottom