Kwa kauli hii ya wakili wa Serikali dhidi ya Sugu, Serikali inahusika na Wasiojulikana

Hilo LA kuwaweka Ndani kwa usalama wao polisi wako sahihi.Raisi ana wapenzi wengi kila kona ukimtukana wanakufuatilia kinya kimya wanapiga nondo ya kichwa unakauka huombi hata maji.Polisi watakuwa wameona hatari inayokuja kwa sugu kuepusha Shari na kushinda wamemzingira kumlinda wakaona heri akae Ndani kwenye ulinzi Massa 24.Lock up yuko salama salimini.Napendekeza akae huko hadi hasira za wapenda ziwe zimepungua.Kupungua hasira kwaweza chukua miezi mitatu hadi sita ile aliyokaa Lema rumande
Pumba nyingine hii
 
Mbona na vibaka wa lumumba kutwa kucha humu mitandaoni ni Chadema na Mbowe tu?
Namlaumu Mwanasiasa aliyepitishwa kwa viwango vyake ikaonekana anatosha kuwa kiongozi wa chama chake. Hawa wana CCM na wana CHADEMA wa JF hatuelewi ubora wao. Wengine wanaweza kuwa ni vijana wa kidato fulani. Hawa walioko majukwaani kwa nafasi zao lazima waonyeshe ukomavu. Siasa isiwe ni matusi kwa rais kila leo wakati hakuna lolote mpaka 2020.
 
Hii sirikali buanaaa acha waendelee kulikoroga soon watalinywa
Wakili ataje hao wanaomfuatilia Sugu kumbe wanawajua sasa shida iko wapi?
Wakili afunguliwe mashtaka aiambie Jamhuri ni kina nani WASIOJULIKANA Tz ibaki salama
 
Mkuu mbona unatishia amani raia?
Umeliona hilo tusi alilonitukana? Wewe ungalimuacha hivi hivi? Mimi simuachi. Lazima nimrekebishe ipasavyo. Vibaka wanaokwapua simu wanachomwa moto. Hawa wanaotukana wenzao ni zaidi ya vibaka wa simu, wanahatarisha usalama wa taifa, hivyo adhabu yao lazima iwe zaidi ya hao vibaka wa simu.
 
Huyo Wakili ni lazima abanwe hapo kwenye rangi ili atoe maelezo ya kina na yanayoeleweka.

  • Wapi kapata taarifa hizo
  • Wanafuatiliwa kuanzia lini
  • Na hao wanaomfuatilia ni akina nani
  • Na wametumwa na nani hao wanaowafuatilia? Muuaji au mwanaye!?
Ukifikiria kimantiki na kwa hoja ya wakili ni kama vile usalama wa watuhumiwa hautakuwa na mbinu au sehemu mbadala zaidi ya rumande. Sababu kama kuna watu wanawatafuta wataendelea kuwatafuta bila kikomo cha muda. Huyo wakili amewapenda sana watuhumiwa?
 
Watakuwa ni wale wale waliotaka kuchukua uhai wa Lissu the Great. Watu wasiojulikana walio magogoni.

Ukifikiria kimantiki na kwa hoja ya wakili ni kama vile usalama wa watuhumiwa hautakuwa na mbinu au sehemu mbadala zaidi ya rumande. Sababu kama kuna watu wanawatafuta wataendelea kuwatafuta bila kikomo cha muda. Huyo wakili amewapenda sana watuhumiwa?
 
Vipi wakishinda kesi wakatakiw kurudi uraiani na kuwa huru,hao wanaowafuatilia watakua wameacha tayari au ndiyo watakuwa wanawasubiri kuwapokea na kutimiza azma yao?

Huyo wakili anayo madini muhimu sana kuipa mahakama ili yafanyiwe kazi.
 
Wakili kwa kauli hii kuna haja naye kuhojiwa maana kauli hii ina mashiko ila inabidi aiambie mahakama watu hao wanaofuatilia hao watu kwa lengo lipi. Ila pia wanasiasa watumie vizuri majukwaa ya kisiasa bila kuathiri upande mwingine.
 
Dah Sugu kakwama,hajajifunza tu kwa Lema?
Halafu Mbowe alikwishawaonya wapayukaji wachunge ndimi zao
 
Leo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kusomewa mashtaka ya uchochezi, kwa madai ya kumuita Rais Magufuli "muuaji" walipohutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbeya, December 30 mwaka jana.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Hakimu wa mahakama hiyo Michael Mteite alitangaza kuwa dhamana ipo wazi kwa watuhumiwa. Lakini kabla hajataja masharti ya dhamana, Wakili wa Serikali, Joseph Pande aliiomba mahakama kuzuia dhamana kwa usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.

Wakili huyo alisema kuwa anazo taarifa kuwa watu hao wanafuatiliwa, na wanaweza kujeruhiwa kutokana na maneno ya fedheha yanayomtaja rais kuwa muuaji, hivyo kwa ajili ya usalama wao ni bora wabakie rumande.

Hakimu Mteite alikubaliana na ombi hilo la jamhuri ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu itakapotajwa tena, na kuagiza Sugu na Masonga wapelekwe rumande katika gereza la Ruanda.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
1. Taarifa za Sugu na Masonga kufuatiliwa Wakili Pande amezipata wapi? Tukisema nae alikuwa kwenye mpango huo wa kuwafuatilia kina Sugu tutakuwa tunakosea?

2. Sugu na Masonga wanafuatiliwa na nani? Kwa kuwa hajawataja watu hao zaidi ya kusema "wananchi" je tukisema ni watu wasiojulikana tutakuwa tunakosea?

3. Na kama ni watu wasiojulikana, haoni kwamba anamaanisha serikali ina uhusiano na watu hao? Na he hiyo haiwezi kuiingiza serikali hatiani kwenye matukio yote yaliyofanywa na watu wasiojulikana kama shambulio la Lissu etc?

4. Wakili Pande alipata lini taarifa kuwa Sugu na Masonga wanafuatiliwa? Kwanini hakuzitoa taarifa hizo mapema ktk kituo chochote cha polisi hadi leo mahakamani? Je wangejeruhiwa au kuuawa kabla ya kufikishwa mahakamani leo, haoni kama angekuwa amewasaidia wahalifu kuficha taarifa?

5. Kwa kuwa anakiri Sugu na Masonga wanafuatiliwa ili waumizwe kwa kumsema vibaya Rais, na kwa kuwa baadhi ya watu waliowahi kumsema vibaya Rais wamejeruhiwa na wengine kupotezwa (wakiwemo Tundu Lissu na Ben Saanane), je Wakili Pande anamaanisha kuwa kuna "kikosi maalumu" kinachoshughulikia wanaomsema vibaya Rais?

Wasiwasi wangu mie ni "usalama" huko gerezani. Mungu awanusuru.
 
Lakini viongozi na wanasiasa wetu pia wwjifunze namna ya kutumia majukwaa vizuri. Hii hambagui mtu kwa chama chake,ni wote wasiotumia majukwaa ya siasa vizuri
 
Kutokana na mambo haya kuleta mkanganyiko mwingi Sana ndani ya jamii yetu ni vema Kama kweli huyo wakili Joseph ametamka hayo ni vema awekwe chini ya ulinzi ili uchunguzi ufanyike kuhusu ukweli wa hiyo kauli take.
Kwa kuwa anausemea upande fulani yawezekana kosa lake halitapewa uzito
 
Back
Top Bottom