Kwa kauli hii ya mbunge musukuma na ndugai; ni wazi CCM ndio watu wanaoitwa wasiojulikana

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,476
2,651
Wasalaam, ukisikiliza kauli alioitoa bungeni leo, ukimwangalia usoni mh musukuma utagundua anachuki kubwa dhidi ya mbunge lissu. Usikiliza kauli ya mh spika ndugai ya kuunga mkono alichosema musukuma utagundua ccm ndio wale watu waliojipa jina "watu wasiojulikana. Inawezekana kabisa kauli hii ni ya ccm ila wamemtuma huyu musukuma kulianzisha dude. Hapa nakumbuka na ninaanza kuamini ni kweli kuna njama za kumvua ubunge mh tundu lissu.

Hapa inaonyesha ccm wanahusika kwa namna moja ama nyingine na jaribio la mauaji(politics assassination) dhidi ya mbunge wa singinda mashariki mh lissu. Watanzania wote tunaona hata ukivaa miwani ya mbao, kwamba mh lissu bado anatembea na wheel chair na magongo pia bado anaonekana ana vyuma vingi mwilini, isitoshe anaejua mgonjwa kapona au LA ni jopo LA madakitari wanaomtibibu lissu. Hawa madakitari ndo watasema mgonjwa akipona, wataandika ripoti yao na kudischarge mgonjwa arudi nyumbani.

Ccm wanausubutu upi kwa kuzuia mshahara kwa mh lissu? Tujiulize je hawa kina musukuma na ccm ni watanzania kweli na wazalendo? Uko wapi Utu wa mtu? Nilitegemea mh ndugai na serikari ya ccm wangemsaidia mtanzania huyu kumlipia gharama za matibabu na kumwombea kwa mola mtukufu apone upesi. Ni ibilisi gani kawaingia ccm? Nilitegemea spika angetoa mwongozo dhidi ya kàuli ile na ingepigiwa kura, sio kusapoti kauli ya kijinga iliotolewa na musukumu. Ikubukwe lissu ni mtanzania na hakujipeleka huko kustarehe Bali anatibia majeraha yake baada ya kushambuliwa kwa risasi kama zote vile 30+.
Ova
 
Ukimuangalia Msukuma ni wazi katumwa kuuliza hili swali. Spika alijiandaa vzr kumjibu.
Amesahau aliumwa akalazwa India muda mrefu tukafunga tukiomba arudi salama. Mungu ni mwema atajibu soon ndani ya miezi mitatu tutajua ni nani mnafiki
 
Ilifahamika wazi kwa wanaCCM na Serikali yao kuwa na nia ovu kwa wapinzani wao na hasa TL.

Kinachofanyika hivi sasa ni kukamilisha torati.

Ni Mungu tu ndiye aliyemponya TL vinginevyo angezikwa kimya kimya. No mkusanyiko, no maombi, no kuomboleza. Na pengine RPC tayari Walikuwa wameshapokea maelekezo. Hii inadhihirishwa wazi na upigaji marufuku T-shirt za Pray for TL.

Hakuna asiyefahamu kuwa juhudi zote zinazofanywa ni kuhakikisha TL anarudi nchini na pale tu akifika either amalizwe at a moment or awekwe kizuizini na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi by that time akipewa dawa za kummaliza Pole Pole.

Binafsi napendekeza TL asirudi. Ni hatari sana kurudi hasa kwa wakati huu ambao wakuu wa nchi wanatetemeka pale jina lake linapotajwa na vyombo vya kimataifa.

Msajili wa vyama vya siasa anasubiri sheria isainiwe ili aweze kumfuta TL uanachama rasmi. Hii ndio kete yao ya mwisho. Before uchaguzi wa 2020 TL atakuwa amefutwa uanachama so hatakuwa na haki ya kumkimbiza mputamputa mpiga push up wa CCM.
 
Na alipopona alirudi.

Sasa Huyo Tobo kapata tu nafuu kasogeza tumbo eti BBC, DW, VOA n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwa Mtanzania kindakindaki (wale wakuasiliwa hususan walikuja kama wakimbizi tunaweza kuwasamehe maana huko kwenye asili yao haya mamabo ni ya kawaida) anayeunga mkono unyama huu, ukatili huu, inabidi ajitazame tena kwenye kioo na ajiulize iwapo ni yeye!!!
 
Ilifahamika wazi kwa wanaCCM na Serikali yao kuwa na nia ovu kwa wapinzani wao na hasa TL.

Kinachofanyika hivi sasa ni kukamilisha torati.

Ni Mungu tu ndiye aliyemponya TL vinginevyo angezikwa kimya kimya. No mkusanyiko, no maombi, no kuomboleza. Na pengine RPC tayari Walikuwa wameshapokea maelekezo. Hii inadhihirishwa wazi na upigaji marufuku T-shirt za Pray for TL.

Hakuna asiyefahamu kuwa juhudi zote zinazofanywa ni kuhakikisha TL anarudi nchini na pale tu akifika either amalizwe at a moment or awekwe kizuizini na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi by that time akipewa dawa za kummaliza Pole Pole.

Binafsi napendekeza TL asirudi. Ni hatari sana kurudi hasa kwa wakati huu ambao wakuu wa nchi wanatetemeka pale jina lake linapotajwa na vyombo vya kimataifa.

Msajili wa vyama vya siasa anasubiri sheria isainiwe ili aweze kumfuta TL uanachama rasmi. Hii ndio kete yao ya mwisho. Before uchaguzi wa 2020 TL atakuwa amefutwa uanachama so hatakuwa na haki ya kumkimbiza mputamputa mpiga push up wa CCM.
Kwa namna international community inavyomwangalia wakimfanyia chochote watakua wamejiloga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimuangalia Msukuma ni wazi katumwa kuuliza hili swali. Spika alijiandaa vzr kumjibu.
Amesahau aliumwa akalazwa India muda mrefu tukafunga tukiomba arudi salama. Mungu ni mwema atajibu soon ndani ya miezi mitatu tutajua ni nani mnafiki
Haya mambo ya kutumana umenikumbusha Zitto na Mudhihir enzi za Buzwagi!
 
Wafanye tu wanavyoona inafaa ila wakumbuke kuwa kila Jambo linalo fanyika au kufanywa na Watu lina Matokeo yake ,walipo mpiga Risasi kwa Nia ya kumuua hakuna alie jua Matokeo haya.
 
Back
Top Bottom