Na pata tabu kuamini kama kweli Lissu alipolipewa fomu, akaijaza na kuweka saini akiwa na moyo mweupe bila kinyongo. Labda kama wakiiweka hiyo fomu hadharami ili kila mtu ajiridhishe. kilichomleta Lissu hadi Nairobi ni kufuata uwenyekiti wa chadema, na kama angepewa hiyo fursa, hata Kwa miguu angevuka boda.Lakini kwasabubu hiyo fursa haipo, kajionea potelea mbali, narudi zangu Ulaya. Ndio maana napata tabu kukubali kama hiyo fomu ipo, na kweli imejazwa na yeye mwenyewe. Tunaomjua Lissu, kama fomu angekuwa amejaza mwenyewe tena Kwa roho nyeupe, angekuwa amesha jitangaza hadharami pale pale Nairobi.
Anyway nikirudi kwenye hoja yako, nimesema mara nyingi humu JF kwamba Chadema inawenyewe, mtu kama Lissu ambaye ni too radical, inawapadhisha sana "wenye" chama kuweza kum-control pindi akipewa mamlaka ya chama au hata ya nchi. Kuna watu wenye maslahi mapana sana Chadema wengine ni mpaka wakuu wa nchi fulani-fulani hapa duniani.