Kwa jicho la tatu, chaguo la Mbowe kwenye uongozi wa juu CHADEMA ni Wakili msomi Tundu Lissu

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,568
2,000
Kwa tunaofikiria na kuusoma mchezo tumeshang'amua. Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Freeman A. Mbowe (Mb) ambaye anagombea tena nafasi hiyo 'amemchagua' Wakili Msomi mwenzangu Tundu Lissu kuwa 'mrithi' wake kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA.

Kitendo cha Mbowe kumtangaza Lissu kuwa anagombea Umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa bashasha na mbwembwe ni kielelezo na uthibitisho wa ung'amuzi huu. Ni kwa kuwa tu Lissu hakuonyesha nia ya kugombea Uenyekiti moja kwa moja.

Baada ya uchaguzi na kupata ushindi kama inavyotarajiwa kwa Mbowe na Lissu, taratibu Mbowe ataanza 'kumuachia' chama Lissu kimajukumu. Mbowe, pamoja na kuchukuliwa na kulipiwa fomu ya Uenyekiti, moyoni mwake anatamani kupumzika na kuwa Mshauri wa chama. Ndiyo maana ameamua kutumia mbinu ya kuwa na Lissu ili amuachie chama.

Lissu atakuwa busy kwa shughuli za kichama kuliko Makamu Mwenyekiti yeyote aliyetangulia.

Kimsingi, Lissu ndiye atakuwa kiongozi mkuu wa CHADEMA kuanzia Disemba.

Mbowe hataki aonekane kwenye uhalisia wa mambo. Yawezekana, Mbowe, katikati ya muhula wake, akajiweka kando na kumuachia rasmi uongozi wa chama Wakili Msomi mwenzangu Lissu!
 

Date20210317

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
3,756
2,000
Hata Chacha Wangwe walisemaga hivyo hivyo!
Umenichekesha sana mkuu ingawa hichi ulichosema nacho si cha kupuuza sana.

Mbowe anaweza akawa anamtumia Lissu ili kuounguza maneno kama atapita kuwa mwenyekiti kwa maana watu watakua na mawazo kama ya mleta tjread so watakua tayar kufunika kombe ili mwanaharam apite akiwa na hopes kuwa Lissu atachukua mikoba maana huyu naamin wengi wanampenda na hana kambi.
 

Mwanzi1

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,940
2,000
Na pata tabu kuamini kama kweli Lissu alipolipewa fomu, akaijaza na kuweka saini akiwa na moyo mweupe bila kinyongo. Labda kama wakiiweka hiyo fomu hadharami ili kila mtu ajiridhishe. kilichomleta Lissu hadi Nairobi ni kufuata uwenyekiti wa chadema, na kama angepewa hiyo fursa, hata Kwa miguu angevuka boda.Lakini kwasabubu hiyo fursa haipo, kajionea potelea mbali, narudi zangu Ulaya. Ndio maana napata tabu kukubali kama hiyo fomu ipo, na kweli imejazwa na yeye mwenyewe. Tunaomjua Lissu, kama fomu angekuwa amejaza mwenyewe tena Kwa roho nyeupe, angekuwa amesha jitangaza hadharami pale pale Nairobi.

Anyway nikirudi kwenye hoja yako, nimesema mara nyingi humu JF kwamba Chadema inawenyewe, mtu kama Lissu ambaye ni too radical, inawapadhisha sana "wenye" chama kuweza kum-control pindi akipewa mamlaka ya chama au hata ya nchi. Kuna watu wenye maslahi mapana sana Chadema wengine ni mpaka wakuu wa nchi fulani-fulani hapa duniani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom