Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,175
- 25,446
Kwa tunaofikiria na kuusoma mchezo tumeshang'amua. Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Freeman A. Mbowe (Mb) ambaye anagombea tena nafasi hiyo 'amemchagua' Wakili Msomi mwenzangu Tundu Lissu kuwa 'mrithi' wake kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA.
Kitendo cha Mbowe kumtangaza Lissu kuwa anagombea Umakamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa bashasha na mbwembwe ni kielelezo na uthibitisho wa ung'amuzi huu. Ni kwa kuwa tu Lissu hakuonyesha nia ya kugombea Uenyekiti moja kwa moja.
Baada ya uchaguzi na kupata ushindi kama inavyotarajiwa kwa Mbowe na Lissu, taratibu Mbowe ataanza 'kumuachia' chama Lissu kimajukumu. Mbowe, pamoja na kuchukuliwa na kulipiwa fomu ya Uenyekiti, moyoni mwake anatamani kupumzika na kuwa Mshauri wa chama. Ndiyo maana ameamua kutumia mbinu ya kuwa na Lissu ili amuachie chama.
Lissu atakuwa busy kwa shughuli za kichama kuliko Makamu Mwenyekiti yeyote aliyetangulia.
Kimsingi, Lissu ndiye atakuwa kiongozi mkuu wa CHADEMA kuanzia Disemba.
Mbowe hataki aonekane kwenye uhalisia wa mambo. Yawezekana, Mbowe, katikati ya muhula wake, akajiweka kando na kumuachia rasmi uongozi wa chama Wakili Msomi mwenzangu Lissu!