Kwa jamaa zangu wananaotafuta ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa jamaa zangu wananaotafuta ajira

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Maundumula, Feb 2, 2012.

 1. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Habari zenu bandugu,

  Kwa jamaa zangu wanaotafuta kazi japo mzingatie haya machache


  1) Hakikisha CV yako ni fupi kwa kadiri inavyowezekana max page 2 ukishindwa kabisa 3 .Kama huwezi kuandika CV tafuta mtu akusaidie.

  2)Kabla hujaenda kwenye Interview jaribu kuzungumza na mtu yeyote anayefanya kazi kwenye hiyo taasisi/kampuni muulize yeye alifanya interview ya namna gani kama anakumbuka chukua "desa" hamna tatizo, ukishindwa basi pitia kwenye tovuti yao usome japo mawili tatu ikiwemo mission na vision ni mambo ya msingi haya.

  3) Siku ya interview kuwa comfortable kama huna utaratibu wa kuamka asubuhi kunywa chai basi usinywe,jiweke safi hata kama unalipenda sana hilo "Afro" basi japo lipake mafuta uchane nywele ikibidi lipunguze. Si vizuri kwenda na manywele machafu au suruali chini ya makalio.

  4) Jitahidi ku make "Eye contact" muangalie anayekuuliza swali kama hujasikia swali au hujaelewa sema. Muombe arudie swali.

  5)Ukiulizwa swali ambalo unahisi unaliweza sana usijibu kwa kifupi mwaga utirio hadi wakukubali, coz muda wa interview labda 30 minutes ukishapunguza 10 minutes na maswali yanakuwa machache. Kama swali hujui kabisa sema sijui.

  6)Usiwe na kigugumizi kutaja mshahara unaotaka (Fanya ka research kadogo ujue scale zao ili usije kuingia chaka ukapata kazi ukawa unalalamika mshahara mdogo kuliko wenzako au ukakosa kwa sababu hii)

  7) Beba vyeti vyako original in case wakihitaji wavione.

  8) Wakikupa nafasi ya kuuliza maswali waulize, na vizuri ukiuliza ni lini watakujibu ili ujue kama ni successful au vipi.

  9)Usidanganye kwenye Interview au usiweke kwenye CV vitu ambavyo huwezi kuvitetea au qualifications ambazo huna.

  10)Hakikisha ma referee wako wanakufahamu na wanafahamu kama wao ni referee's wako, usiweke mtu asiye na taarifa.
   
 2. m

  majimbi Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunakushukuru mkuu
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Ahsante mkuu lakini ajira za sasa ni za vimemo jamaa angu kapiga interview zaidi ya 30 na yupo fit mpaka leo anasota
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Jamaa yako ana elimu gani?

  Je huwa anatumia mbinu zipi kutafuta kazi? Huwa wanamwita kwenye Interview au hawamwiti kabisa?
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu kwa haya
  Yatasaidia wengi na haswa hata sisi ambao tunasaka ajira au kubadilisha mazingira aise
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  All the best bro,

  Kubadilisha ajira ndio mpango maana uking'ang'ana sehemu moja unakuta increment hailipi sometimes.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Na sometime waajiri wanakuzoea hata ukiwasilisha madai yako wanakuuliza na wewe
  As if huna haki ya kuomba increment ya aina yoyote
  na hata ukifanya kazi nzuri hupati hata bonus kwa kuwa wewe ni mzoefu
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hahaha!

  Ukiona hivyo kaka huo ni muda muafaka kusonga mbele unaachana nao fasta.

  Maana wanakuja watu wapya wana negoatiate mshahara wanakupita. Wewe hata ukipandishwa cheo mwezi wa May wanakwambia mshahara utaongezeka march mwakani wakisha adjust na hainaga arrears most of the time.

  Dawa yao hawa kuwakimbia mwenzako nimejiwekea miaka 2 tu baasi! huwa siongezi
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mchakatio huo upo sana mkuu
  Kuamua mustakabali wa maisha mbele maana waajiri sasa wamekuwa vimeo
  hakuna nyongeza hakuna kupanda cheo wala nini
  na wanapokuja waajiri wapya utaona tuu mambo yanavyochangamkiwa chapu chapu huku wale wa zamani wanazidi kuanguka tuu
   
 10. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ahsante sana kiongozi,umenikumbusha interview ya kwanza tuliitwa fresher's wa FTC kutoka DIT wiki mbili kabla hatujamaliza chuo,tulikuwa jopo la madent baada ya technical questions candidate mmoja kaulizwa swali la social unapendelea nini? Akajibu kwa mbwembwe napendelea sana kununua na kusoma magazeti hasa ambayo si ya udaku,kama vile Daily news,Guardian,East Africa n.k mjanja moja akamwotea na kumwuliza swali daily news linauzwa sh ngapi akasema sh 200/= wakati huo lilishapanda muda mrefu sana linauzwa 500/= Jopo zima halina mbavu! Mwingine kaulizwa kataja mshahara mudogo sana kama wa kiwanda cha Urafiki ili wamkubali kumbe ndo kapigwa chini hana confidence mbona mshahara huu hautoshi ha kwa nauli tu?
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ukikaa mahala mda mrefu wanakuzoea alafu maslai yanakuwa constant as if maisha yamesimama wakati inflation kila leo inapanda na TANESCO wanapanda.
  Sometimes hawa MAHR wanaishi mwezini,mtu anakuuliza kwa nini tukuongeze mshahara wakati nae ni sehemu ya maisha ambayo nawe unaishi.Nimegundua mara nyingi wanalean kwa mwekezaji hasa kwa private companies bila kujua kuwa waafrika wenzake ndo tutakaomzika
   
 12. F

  Ferds JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  kote nakubaliana na wewe, ila hapo point na 1, wengine wanaihitaji a well detailed resume, ukisema page 2 au 3 mh naingia wasiwasi kidogo, nachojua mimi wale watafutaji tujitahidi kuwa makini ktk uandishi wa cover latters na cv zetu ziwe zimeandikwa vyema, in brief lakini ikiwa na details zako zote muhimu,hasa zile ambazo zinendana na kazi uliyoomba.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ferds,

  Nakubaliana na wewe kwamba ni muhimu details zote za muhimu zionekane lakini kwa mtu anayetoka chuo unahangaika kutafuta kazi mwajiri anapokea CV 1000 ya kwako ina page 5 sidhani kama inalipa aisee kwa sababu jamaa wana not more than 30 seconds kuangalia kila moja.
   
 14. m

  mazimba john Member

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yeah ni kweli i have evidence on that kuna vacancies zilitangazwa zilikuwa kama hamsini hivi watu waliofanya application walikuwa ni zaidi ya elfu tano so if your cv has more than 3 pages make hardtime kwa yule anaeipitia, he or she will be bored
   
 15. e

  erickmuganyizi Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninashukuru sana bro maana umetupa mwanga ss tunaoanza kutafuta ajira
   
Loading...