Kwa idadi hii ya waomba mikopo heslb 2013/14 wote watapata kwa 100%

Brother James

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
233
172
Leo HESLB wametoa taarifa kwa Umma juu ya idadi ya waombaji wa mikopo kama ilivyoandikwa chini:

1.0 UTANGULIZIBodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2013. Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).2.0 WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA
Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kutokana na utaratibu huu, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa. Hii ni muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014

.
3.0 IDADI YA WANAFUNZI WALIOKWISHAOMBA MIKOPO KUFIKIA MEI 30, 2013
Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni 424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.
Na.
Waombaji wa mara ya kwanza waliokamilisha kujaza fomu
Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji
Wanafunzi wanaoendelea na masomo waliojaza fomu na kukamilisha
424
5320
60367

4.0 HITIMISHO

Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:(i) Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.(ii) Kutumia huduma ya msaada kwa wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi. Huduma hiyo inapatika kwa kupiga namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri siku ya jumamosi.(iii) Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.
IMETOLEWA NA:

BODI YA WAKURUGENZI

BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Budget ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni kutoa mikopo kwa jumla ya waombaji 98,025; yaani waombaji wapya watakao pata mikopo ni watu 35,649 na waombaji wanaoendelea na masomo ni 62,376.
 
Back
Top Bottom