Kwa hili, watanzania tunakwenda wapi?

JENSENE

Member
Mar 7, 2011
52
6
Watanzania ndugu zangu, hebu tufikiri kwa makini juu ya hatma yetu. Mambo mengi yanatuzidia sasa mfumuko wa bei, huduma mbovu ya afya, elimu duni, miundombinu mibovu, maji, kunyang'anywa ardhi, umeme, na mengine. Ila kwa leo tujaribu kuchambua hili la umeme japokuwa limeongelewa mara nyingi.
Takribani mwezi sasa kumekuwa na tatizo la kukatika katika kwa umeme, wakati serikali yetu ilituahidi kuisha kwa tatizo hilo. Mwanzoni tatizo ilikuwa ni upungufu wa maji. Lakini kwa sasa nashindwa kuelewa tatizo hasa ni nini kukatika umeme kila mara? Watanzania tunashindwa kufa shughuli zetu zina tumia umeme je tutajikwamua lini na hali? "A good man is the one who do good things all the time, not due tothe influence others" let join in discussion.
 
Back
Top Bottom