Kwa hili upinzani Bungeni unasubiri nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili upinzani Bungeni unasubiri nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lawson, Jul 5, 2011.

 1. L

  Lawson Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Japo mimi ni kipenzi kikubwa cha hotuba za baba wa taifa hasa pale alipokuwa anajaribu kutumia lugha nyepesi nyepesi kuzima mambo makubwa yaliyokuwa yanatishia amani ya nchi kwa umakini mkubwa. Ila sijawahi, wala sitawahi hata sikumoja kuunga mkono falsafa yake ya kufanya Tanzania kuwa socialist state kitu kinachotugalimu hadi leo.

  Siku hizi viongozi wetu nao wamejiweka kwenye viatu vya Nyerere nakujidai kutolea maamuzi magumu kwa lugha nyepesi (hata kucheka cheka) bila kujua kuwa kipaji hicho hawana.

  Katika toleo jipya la kitabu chake (Nyerere) UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA (Toleo la kizazi kipya) nimefulahishwa sana na kauli yake kwamba uongozi mara zote ni kuongoza na siyo kufuata (yaani kuonesha njia unao waongoza nasiyo wao kukuonesha njia).

  Hili lingekuwa linazingatiwa sidhani kama viongozi mzigo kama Ngeleja, Hosea ……n.k wangekuwa wanaendelea kutuumiza sisi wananchi kwa kutumia magari, nyumba na marupurupu mengine tunayoghalimia kwa jasho letu sisi walipa kodi. Sioni mantiki ya Ngeleja kuendelea kula kiyoyozi bungeni wakati wajasiriamali bidhaa zao zinakufa dukani kwa kukosa umeme, wakati ndio hao hao wanasubiri kuwakamua kwa kodi lukuki.

  Sioni sababu ya Hosea kuendelea kushikilia ulaji huku kati ya kesi 100 TAKUKURU ilizofungua hakuna hata moja imesha shinda. Na kwanini akomalie kesi za laki moja na kuacha kesi za mabillion? Hata kesi ya rada aliyo saidiwa na SFO bado anasita kuwashughulikia waliotafuna vijisenti vyetu nakuvificha huko mamtoni (au na yeye yumo?) na kwanini serikali iombe chenji wakati waliotusababishia hasara hiyo bado wanadunda serikalini na bungeni bila kuguswa?

  Kwakuwa nina imani na kambi (rasmi) ya upinzani bungeni kwanini wasilete hoja binafsi yakutokuwa na imani na mkurugenzi wa TAKUKURU pamoja na Ngereja kama Zitto alivyofanya dhidi ya Mh. Karamagi enzi hizo?? Hata kama mtafukuzwa tena bungeni ni bora mje mhangaike na kukaa huku mtaani na watanzania wenzenu kuliko kuendelea kula sahani moja kwenye mjengo na wabunge ambao tunajua damu zao zimesha badilika rangi na kuwa za kijani hivyo siyo wenzetu tena.

  Nahisi hata hili jina la Mheshimiwa linawapumbaza sana viongozi wetu kwani wanafikiri wao ni zaidi ya watanzania wote, mimi naona bora turudi enzi hizo tulipokuwa tunaitana ndugu fulani kwani sote tulionekana kitu kimoja.

  Watakaopata nafasi yakusuka katiba mpya naomba msisahau kipengele cha mwananchi kumuwajibisha waziri au mtu yeyote aliyeteuliwa na rais maana hao watu wanaviburi sana kwavile wanajua sisi wananchi wa kawaida hatuna chakuwafanya.

  Naomba kutoa hoja, samahi kiswahili changu hakijanyooka vizuri maana sijakaa nchini mda mrefu.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. n

  nampenda New Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hawa wenzetu wamesahau kama ni wajibu wao kuwatumikia wananchi.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  HTML:
  Ila sijawahi, wala sitawahi hata sikumoja kuunga mkono falsafa yake ya kufanya Tanzania kuwa socialist state kitu kinachotugalimu hadi leo. 
  
  
  Binadamu hawana wema!
  Angeamua kuwa Tanzania iwe ya kibepari naamini kuna wengi tu wangemlaani!
  Tukubali kuwa miongo hiyo ilikuwa lazima kuwa upande fulani kwa maslahi ya nchi!
  Je Wajamaa wangekamata uchumi wa dunia kwa sasa ungekuwa na la kusema?
  Tuna akili na uongozi wetu sasa, tuzitumie kufanya maamuzi ya kusongesha nchi mbele..kuongelea mambo ya 50 yrs back ni wastage ya kufa mtu!
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna mambo yanakera nchi hii, Kagoda , meremeta, Rada, umeme, kuuzwa ardhi kwa wageni n.k. ninachopendekeza wapinzani watoe hoja ya kutokuwa na imani na watawala ili wapigwe chini, kwa kuanzia kwa Ngeleja wabunge waondoe shilingi
   
Loading...