Kwa hili tu, Upinzani nchini usiwe Mzigo.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,111
2,000
Yaani mikutano ya Chama inafanyikia ikulu watu wako kimya?? Hakuna anayehoji kitu hata mmoja??hakuna hata kunyoosha kidole au kukemea? Huu uoga umeanza lini? Hiki kitu kinashangaza sana na kinaumiza mno!!! Tena katika mfumo ambao kila chama kina haki ya kwenda ikulu endapo kikapewa ridhaa na wanamchi.

Kwa uelewa Wangu mimi wa elimu ya hapa na pale katika sharia ni kwamba Ikulu ni kama nyumba taifa! Ikulu haijawa nyumba ya kufanyia shughuli za kichama!! Huu ni mwiko! Kwanini miiko ya kitaifa inavunjwa kiasi hiki?

Kama watu wanatumia Ikulu kufanyia shughuli za chama watashindwaje kuchota pesa benki kuu kwa matumizi ya shughuli za chama? Kunatofauti gani kutumia Ikulu kwa shughuli za Chama na kutumia pesa za walipa kodi zilizopo benki kuu kendesha shughuli za chama?

Kwahiyo CHADEMA, CUF,NCCR,ACT,TLP na vyama vingine navyo vinanavyo wajibu wa kutumia Ikulu kwa shughuli za vyama vyao endapo wakihitaji? Hili ndio mara ya kwanza linatokea Tanzania tu! Sidhani kama hayati Baba wa taifa angalikua hai angekubaliana na vitendo hivi.

Hivi itokee Mwenyekiti Wangu wa wataa wa hapa Sanaware akaita wanachama wenzake kama walikua na mkutano wa kichama wafanyie kwenye ofisi ya serikali tena wakavaa na sare zao hali itakuaje? Wananchi walichukuliaje hilo tukio ikiwa ni ngazi ya mtaa tu? Siasa za mtaa huu zitatafsiriwa vipi?

Kwa hili ninawashangaa wapinzani wa nchi hii kikaa kimya, inamaana wao wanaona sawa? Wapinzani Mara nyingi hubeba sauti za wananchi lakini kwa ukimya huu wanakatisha tamaa wanamchi.
 
The dream

JF-Expert Member
May 10, 2015
1,001
2,000
Mkuu muda mwingine hawa wapinzani tutawaonea tu bure, ulitaka Mbowe au Lema ndio wajitokeze kukemea suala hili kweli?

Hao kina Mbowe nao ni binadamu tofauti na upinzani wana mambo yao ya maisha pia.

Natamani 2020 iwe ni Wananchi Vs Ccm na sio Ukawa Vs Ccm
 
Boom J8

Member
Dec 20, 2016
92
125
Upinzan sasa hv umevurugwa....wanaonesha hawako pamoja kabsaa....ccm hongeren kwa hl lengo lenu limetimia....
 
Katasheka jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2016
528
500
Yaani mikitano ya Chama inafanyikia ikulu watu wako kimya?? Hakuna anayehoji kitu hata moja??hakuna hata kunyoosha kidole au kukemea? Huu uoga umeanza lini? Hiki kitu kinashangaza sana na kinaumiza mno!!! Tena katika mfumo ambao kila chama kina haki ya kwenda ikulu endapo kikapewa ridhaa na wanamchi.

Kwa uelewa Wangu mimi wa elimu ya hapa na pale katika sharia ni kwamba Ikulu ni kama nyumba taifa! Ikulu haijawa nyumba ya kufanyia shughuli za kichama!! Huu ni mwiko! Kwanini miiko ya kitaifa inavunjwa kiasi hiki?

Kama watu wanatumia Ikulu kufanyia shughuli za chama watashindwaje kuchota pesa benki kuu kwa matumizi ya shughuli za chama? Kunatofauti gani kutumia Ikulu kwa shughuli za Chama na kutumia pesa za walipa kodi zilizopo benki kuu kendesha shughuli za chama?

Kwahiyo CHADEMA, CUF,NCCR,ACT,TLP na vyama vingine navyo vinanavyo wajibu wa kutumia Ikulu kwa shughuli za vyama vyao endapo wakihitaji? Hili ndio mara ya kwanza linatokea Tanzania tu! Sidhani kama hayati Baba wa taifa angalikua hai angekubaliana na vitendo hivi.

Hivi itokee Mwenyekiti Wangu wa wataa wa hapa Sanaware akaita wanachama wenzake kama walikua na mkutano wa kichama wafanyie kwenye ofisi ya serikali tena wakavaa na sare zao hali itakuaje? Wananchi walichukuliaje hilo tukio ikiwa ni ngazi ya mtaa tu? Siasa za mtaa huu zitatafsiriwa vipi?

Kwa hili ninawashangaa wapinzani wa nchi hii kikaa kimya, inamaana wao wanaona sawa? Wapinzani Mara nyingi hubeba sauti za wananchi lakini kwa ukimya huu wanakatisha tamaa wanamchi.
Mbowe alivyouza chama chetu kwa Fisadi Lowasa, wananchi walihoji?
 
CHAPTER5

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
558
500
Wadau mbalimbali walisha zungumzia kuhusu uhalali wa ccm kufanyia mkutano ikilu.
Walichojibiwa ni kuwa vyama vingine haviku zuiwa kufanyia mikutano ikulu.
 
chendelela

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
933
1,000
Upinzan sasa hv umevurugwa....wanaonesha hawako pamoja kabsaa....ccm hongeren kwa hl lengo lenu limetimia....
Wewe umewaona tu wapinzani kwani nchi hii viongozi wa dini hawapo ? hata wakizungumza kuwakilisha mawazo yao mbadala mnawasema ni wachochezi,waroho wa madaraka,wachumia tumbo na eti wana taka kuvuruga amani ya nchi.
Mimi nawapongeza wapige tu kimya mpaka 2020 kwa sababu hata wakizungumza hawasikilizwi,ninaamini wananchi wakiisoma namba vizuri polepole wataanza kuelewa umuhimu wa upinzani na siasa za ushindani wa kivyama na hatima ya maisha yao.
 
ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,436
2,000
Magufuli alishawaambia ni ruksa kufanyia mikutano yao ikulu,ila tu wamjulishe ajenda zao kwanza!
 
Hoja nghwani

Member
Nov 4, 2014
49
125
Ikulu ni ya watanzania wote, kwa hiyo kila mmoja ana haki ya kutumia ukumbi huo, ila tu uzingatie sheria na taratibu zinazo takiwa basi,
 
Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Katika historia ya marekani ...kuna raisi Aliishawahi kupeleka Samani za ikulu kwenye kamari(betting)....hivyo usimshangae huyu mbumbu wetu maana anapitia hatua za ukuaji katika utawala. ...
 
Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
12,968
2,000
Mbona wandishi wa habari hamkuhoji walikula na kunywa kwa hela ya nani na kipindi cha jk alivyo kuwa anawaita ikulu wapinzani mbona hamkuhoji au kipindi hicho hazikuwa kodi za wananchi
 
Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
upinzani hufanya kazi vema kama kuna watu hai na wenye uelewa, lkn siyo kwenye watu wafu kama watz. upinzani leo ukiitisha maandamano juu ya suala hili hata ww mtoa mada huendi. maana watz sote ni maiti na wachache walio mahututi ni mbumbumbu,
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,748
2,000
Yaani mikutano ya Chama inafanyikia ikulu watu wako kimya?? Hakuna anayehoji kitu hata mmoja??hakuna hata kunyoosha kidole au kukemea? Huu uoga umeanza lini? Hiki kitu kinashangaza sana na kinaumiza mno!!! Tena katika mfumo ambao kila chama kina haki ya kwenda ikulu endapo kikapewa ridhaa na wanamchi.

Kwa uelewa Wangu mimi wa elimu ya hapa na pale katika sharia ni kwamba Ikulu ni kama nyumba taifa! Ikulu haijawa nyumba ya kufanyia shughuli za kichama!! Huu ni mwiko! Kwanini miiko ya kitaifa inavunjwa kiasi hiki?

Kama watu wanatumia Ikulu kufanyia shughuli za chama watashindwaje kuchota pesa benki kuu kwa matumizi ya shughuli za chama? Kunatofauti gani kutumia Ikulu kwa shughuli za Chama na kutumia pesa za walipa kodi zilizopo benki kuu kendesha shughuli za chama?

Kwahiyo CHADEMA, CUF,NCCR,ACT,TLP na vyama vingine navyo vinanavyo wajibu wa kutumia Ikulu kwa shughuli za vyama vyao endapo wakihitaji? Hili ndio mara ya kwanza linatokea Tanzania tu! Sidhani kama hayati Baba wa taifa angalikua hai angekubaliana na vitendo hivi.

Hivi itokee Mwenyekiti Wangu wa wataa wa hapa Sanaware akaita wanachama wenzake kama walikua na mkutano wa kichama wafanyie kwenye ofisi ya serikali tena wakavaa na sare zao hali itakuaje? Wananchi walichukuliaje hilo tukio ikiwa ni ngazi ya mtaa tu? Siasa za mtaa huu zitatafsiriwa vipi?

Kwa hili ninawashangaa wapinzani wa nchi hii kikaa kimya, inamaana wao wanaona sawa? Wapinzani Mara nyingi hubeba sauti za wananchi lakini kwa ukimya huu wanakatisha tamaa wanamchi.
mkuu, kwa sasa upinzani unakatisha tamaa sana. ni kama vile umeufyata. hovyo kabisa!

sympathetic institutions kama vile viongozi wa dini, etc wanapata nguvu ya kuikemea serekali kwa yasiyofaa pale tu opposition inapoonekana ku-take lead kwanza.

kama viongozi wameshindwa waseme tu tutafute ustaarabu mwingine... badala ya kutupotezea muda wa kuendelea kuamini tuna viongozi wa upinzani kumbe ni maboya tu!

[HASHTAG]#tuanzishechamakipyachaupinzani[/HASHTAG]
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom