Kwa hili Stanbic Bank waombe radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili Stanbic Bank waombe radhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Sep 17, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 17, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  KWA HILI STANBIC BANK WAOMBE RADHI

  Niko Mbali na mjini , Njia yangu rahisi zaidi ya kuchukuwa pesa kutoka kwenye benki ninayohifadhi pesa zangu ni kwa kutumia Kadi za ATM , ambapo inaniruhusu kutumia ATM za benki nyingine kama zao zinakuwa hazina pesa au sehemu hiyo hakuna mashine za ATM zao ndivyo ninavyofanya kazi kila wakati kwa sababu niko nje ya mji - wengine ni kutokana na kazi zao na vitu vingine uharaka na nini wanatumia hizi mashine za ATM kwa ajili ya kuchukuwa pesa zao .

  Sasa toka jana saa 6 mchana benki inayohifadhi pesa zangu STANBIC imekuwa na tatizo kwenye utoaji pesa kwenye mashine za ATM mpaka kwenye teller zao ndani ya benki zao karibu zote nchini hata unapotumia ATM kadi hii kwa ajili ya kujichukulie pesa kutumia mashine za benki zingine napo hazifanyi kazi .

  Leo imeingia siku ya pili sijapata taarifa yoyote kutoka kwa STANBIC ya kimaandishi au hata ya maneno , wakati najisajili kwenye huduma zao niliwapa Barua pepe zangu 3 zote zinazofanya kazi , nikawapa mpaka namba zangu za simu 2 zote ambazo ziko hewani masaa 24 hata nikiwa nje ya nchi zote huwa zinafanya kazi .

  Nakuambia leo ni siku ya pili na sasa ni saa 7 mchana huduma za kibenki kwenye benki ya STANBIC bado hazijarudi kawaida zaidi ya masaa 24 haya , wengi wamepata hasara kwa kupotezewa muda wao na hata kupoteza wateja kama watu hao walikuwa wanataka kutoa pesa kwa ajili ya kuendesha biashara zao mbali mbali .

  Namba zetu za simu wanazo wanashindwa kutupa taarifa hata kwa sms tu , kwani sms 1 ni bei gani kumtaarifu tu mteja kwamba kwa sasa kuna tatizo na tutarekebisha baada ya muda fulani ? hiyo inaweza kuwa gharama lakini email zetu wanazo kwanini hata wasitutumie basi email kutupa taarifa badala ya kutumia email hizo kututumia matangazo ya biashara ?

  Huu sio uungwana hata kidogo wanatumia amani tuliyokuwa nayo na utulivu kudhubutu kufanya mambo kama haya kama vile hakuna hata mmoja atakayenyoosha kidole kuuliza au kuwafokea , wanafikiri watu wote ni mbumbumbu wameridhika kwahiyo watakaa kimya tu bila kufanya chochote .

  Nimepotezewa muda wangu na nimepata hasara sana kwa haya masaa 24 ambapo benki haifanyi kazi nashindwa kufanya shuguli zingine zinazonilazimu kutumia hela yangu ambayo nimehifadhi kwenye benki yao kwa maarifa yangu mwenyewe , leo sipewi taarifa na wala sina haki ya kupata taarifa hizo

  Nimeangalia kwenye vyombo vyote vya habari , mpaka kwenye magazeti mpaka kwenye tovuti mbalimbali hata ya benki hiyo hakuna taarifa zozote za tatizo hili zaidi ya masaa 24 sasa .

  Nauomba Uongozi wa benki hii utoe taarifa rasmi kwa ummah na kuomba msamaha kwa wateja wao wote ambao wamesumbuliwa na tatizo hili kwa namna moja au nyingine , na wasimamizi wa mabanki haya kama ni benki kuu au taasisi zingine ziwabane waendeshaji wa benki hizi kuhusu viwango vyao vya utoaji huduma na mawasiliano yao mengine waliyokuwa nayo kwa wateja wao .
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,049
  Likes Received: 24,051
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenistua, manake hata mimi hiyo ndiyo bank yangu. Yasije yakawa ya Meridian Biao au Greenland bank. Kalaghabaho!
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Shy,
  Pole sana na ni imani baadhi ya wafanyakazi hupitapita humu ujumbe wameupata pole sana kwa usumbufu. Kama kutaendelea hivyo ni bora kubadilisha Bank kwanI wakiona WATEJA WANAZIDI KUPUNGUA LABDA WATAJIFUNZA.
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ilo ni tatizo la Bank Karibu zote. Nakushauri wakisha tautua tatizo, ukacheck balance kwani yawekana hukuchukua pesa lakini mashine hizo zikaonyesha kuwa umechuka pesa kwenye account yako. Kuepuka huu usumbufu, naona bora watu watumie Bank za asili kama kuchimbia chini/maboksi/vyungu nk.
   
 5. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nisije nikawa na bahati mbaya ya aina yake maana mchana wa leo ndio kwanza nimetoka kufungua akaunti katika benki hiyo, na wakati huo ATM zilikuwa hazifanyi kazi na ni kwa nchi nzima.

  Wahusika wa benki hiyo mtoe taarifa kwa wateja wenu na MUWAOMBE RADHI KWA USUMBUFU ULIOTOKEA
   
Loading...