Unamwuunga au humwuungi ni juu yako. Haitatokea akaungwa mkono kwa jambo lolote na watu wote. Mi binafsi namwuunga mkono. Pamoja na kuwa rais bado ana uchungu na miundombinu. Inaonyesha ana uchungu na barabara zetu na bila shaka mtu huyu pesa ikikaa vizuri atatandika mikeka nchi nzima. Si mwizi ila uchungu wa miundombinu mibovu humtia hasira. Pia anaakisi jina tingatinga. JK hakukosea.
Mimi namuunga mkono kuhusu barabara. Na simuungi mkono jinsi alivyo iwasilisha taarifa pale sio mahala pake. YEYE ange rudi ofisini kwake na angetoa taarifa. Ila tu angepigiwaje makofi, hapo ndio naona nivizuri ametolea taarifa pale ili apate walau kongole.