Katiba yetu imeweka bayana kwamba serikali haina Dini, japo viongozi wa serikali wana Dini zao! Rais Magufuli anafahamika kwamba yeye ni m-Kristo m-Katoliki! Kwamba kwa utashi wake anaamua kwenda kusali kwenye makanisa ya madhehebu mengine, ni swala lake binafsi!
Simuungi mkono anapokwenda kwenye makanisa hayo na waandishi wa habari/kamera na anapopewa nafasi ya kutoa salamu badala ya kuzungumza tu kama muumini, anazungumza kama Rais na anazungumzia mambo yenye mwangwi wa kisiasa! Kipekee zaidi simuungi mkono kwa kwenda kuzungumzia swala la barabara ya Ubungo - Kibangu Kanisani kwa mzee wa upako!
Hata kama kweli aliguswa na mzee wa upako kwa vile anampenda, angaliweza kufanya ziara hata ya kushtukiza kwa wananchi wa eneo husika na kuwaahidi hilo!
Tena hili lingemletea heshima kubwa kwa jamii na hata kumjenga kisiasa!