Kwa hili serikali ya Magufuli imekurupuka

Serikali ilipokubali kuingia kwenye mfumo wa Market economy ilijitoa kwenye biashara na kuanza ubinafsishaji, jukumu la serikali likabakia kukusanya kodi.ulikuwa ni ujinga uliovuka mipaka kwa serikali kujitoa ktk kutoa huduma kwa raia wake na ndio matokeo ya mfumuko wa shule nyingi binafsi na mahospital mengi binafsi. wenye shule ni wafanyabiashara waliowekeza kama wafanyabiashara nyingine. cha msingi serikali iboreshe shule zake na ikifanya hivyo kutakuwa na haja gani wazazi wakalipe mamilioni kwa huduma zinazopatikana bure?? soko huru liamue, vinginevyo turudi ya mwaka 1968, nationalization
Absolutely true
 
Hapa mawaźo yako hayajui maana uchumi wa soko huria. Soko huria ni pamoja na kuwa na utaratibu wa sheria. Shule binafsi zilikuwa zunafanya kufuru kwenye ada. Hazifuati ukuaji wa uchumi na upandaji wa kipato cha wananchi. Wawekewe bei elekezi kama ilivyo kwenye mafuta. Tusingefanya hivyo injini za magari zingekuwa zimeharibika mno
 
kusingekuwepo EWURA,
SEREKALI NDIYO PEKEE ITATOA MWONGOZO,KWA KILA JAMBO KATIKA KUPROTECT WANANCHI WAKE.
 
Tulieni serikali ipo na serikali yenyewe ni Dr JPM. Haiingii akilini kila shule kujifanyia ujinga wanaoutaka. Ada itashushwa na watoto wataendelea kupata elimu bora kabisa kwa bei reasonable kabisa. Kila anayelalamikia ujinga wa primary/nursary/sec kulipa ada kuliko hata bei ya kozi ya chuo namuona mtindio wake haupo sawa. Halafu mtu huyo huyo atataka mwanae asome UD! Kama unajiona unazo kamsomeshee nje hapa kwetu hatutaki matabaka ya kijinga. Yaani unamsomesha mwanao kwa miada hadi 2-3M kwa mwaka kisha akifika chuo unataka apewe mkopo au asome bure!! Kisha akili yako unaiona ipo sawa.
 
Niliandika kwa kirefu kwenye thread nyingine hapa kwa nini serikali kuweka price ceiling ni kuchemsha.

Masaa machache yaliyopita, nilinukuu mpaka mifano ya Venezuela.

Hapa nitarudia tu.

Katika free market ,au hata mixed economy, serikali inaweka platform tu, kwa kutumia fiscal policy, monetary policy, taxation, etc, haipangi mwisho wa bei.

Mwisho wa bei unapangwa na mafket forces.

Aliyesoma Econonics, akajua free market ni nini, atajua hilo.

Vinginevyo tunatafuta kurudi 1982.
 
Anaehawezi aende za kawaida tu, kila mtu ana standard zake....
 
Hakuna uhusiano wa mfano wako na mada husika. Kwa nini basi serikali isiamuru gharama ya taxi kutoka Mwenge kwenda Posta iwe sh 400?
Double Standard sio dhambi, km haujimudu private elekea serikalini. Mishahara ya walimu wa private sio sh kumi kumi unategemea walipwe mawe?
acha hasira mtoka pabaya ngoja ue;eweshwe-
  • shule za binafsi hazilipi Kodi wajati TAXI inalipa Kodi TRA, Bima, FireEX, Road/L, Parking ya Manispaa, na hairuhusiwi kuvuka eneo la kibiashara
  • shule za binafi ni wizi mtupu Wazazi ndio wanaochangia ujengaji wa mabweni, chakula masomo nk
  • shule za binafsi mmiliki hataki kushare na mzazi hata km mlichangia katika ada matofali (hakuna Hisa)
ndio maana Magufuli na serikali imesema mwisho sasa elimu iwe 350,000 upili au 150,000/ awali kwa mwaka vitakavypzidi ni maamuzi ya mzazi km usafiri, sare, chakula nk lakini sio fagio au karatasi za mitihani
 
Serikali ilipokubali kuingia kwenye mfumo wa Market economy ilijitoa kwenye biashara na kuanza ubinafsishaji, jukumu la serikali likabakia kukusanya kodi.ulikuwa ni ujinga uliovuka mipaka kwa serikali kujitoa ktk kutoa huduma kwa raia wake na ndio matokeo ya mfumuko wa shule nyingi binafsi na mahospital mengi binafsi. wenye shule ni wafanyabiashara waliowekeza kama wafanyabiashara nyingine. cha msingi serikali iboreshe shule zake na ikifanya hivyo kutakuwa na haja gani wazazi wakalipe mamilioni kwa huduma zinazopatikana bure?? soko huru liamue, vinginevyo turudi ya mwaka 1968, nationalization

Wewe unajua market economy?kama unajua niambie nini maana ya price ceiling na price floor.
 
Wewe ndio umekurupuka,serikali lazima itoe bei elekezi hata Kama soko huria....Ingekua serikali haitoi bei elekezi wafanyabishara wangemonopoly soko kwa bei watakazo cement ingeuzwa elfu 60 sukari elfu 5.
 
Serikali ilipokubali kuingia kwenye mfumo wa Market economy ilijitoa kwenye biashara na kuanza ubinafsishaji, jukumu la serikali likabakia kukusanya kodi.ulikuwa ni ujinga uliovuka mipaka kwa serikali kujitoa ktk kutoa huduma kwa raia wake na ndio matokeo ya mfumuko wa shule nyingi binafsi na mahospital mengi binafsi. wenye shule ni wafanyabiashara waliowekeza kama wafanyabiashara nyingine. cha msingi serikali iboreshe shule zake na ikifanya hivyo kutakuwa na haja gani wazazi wakalipe mamilioni kwa huduma zinazopatikana bure?? soko huru liamue, vinginevyo turudi ya mwaka 1968, nationalization

Naunga mkono hoja anaeona private gharama aende shile za bure
Mbona kuna EWURA na SUMATRA wanatoa bei elekezi kwenye Petrol na vyombo vya moto, mbona hamlalamiki, mmetafsiri vibaya hiyo kauli issue ni ada kwa sasa wasipandishe waendelee na za awali yaani kama unatoza 6 million, 2million au laki tano usipandishe kwanza mpaka utaratibu mpya utakavyotoka. Kinachofanyika hapa huduma iendane na hali halisi sio mwananchi hata kama una uwezo wa kulpa basi ulipe tu kiwango cha juu wakati gharama za uendeshaji zipo chini
 
Pamoja na kwamba naunga sana mkono suala la gharama elekezi,lakini 350,000 bweni na 150,000 day ni jambo lisilofikirika achilia mbali kutekelezeka.
Ada elekezi ni muhimu! Japo naunga mkono kuwa labda wangereview hivi viwango. Ila kwa kweli asante sana Mh. Magufuli wengine huchanganya biahsara huria its not equal to biashara holela na ndio tuliyonayo Tanzania as if hamna serekalim Ntu anaamka nyumbani na kuja kubadilisha ada apendavyo timesema no enough is enough. Wengine hapa ni wahanga wa mabei ya shule hizi! Tatizo wenye shule wanataka wazazi ndio wawajengee shule kwa hizo hizo ada. This is not acceptable at least kwa Dr. Magufuli ameliona hili. Halafu watanzania tusiwe wajinga eti ooh kama huna mpeleke shule za kata. Yaani hawana hata muda wa kuquestion uhalali wa hizo ada. Tena hapa Tanzzania unakuta madada makubwa lakini service very very poor.
Tofauti na Kenya kama unalipa ada kiasi fulani inaendana na hali ya shule hata mzazi unaridhika. Binafsi nililipa hela nyingi sana lakini hiyo shule mtoto aliyosoma- mazingira ya shule excellent, curricullum exceleent, vyakula ni vizuri sana balanced diet, elimu wanayotoa nzuri sana. Sasa nilienda shule moja, sitaitaja jina at least kwa sasa, mamilioni ya pesa, hayo mabweni ya wanafunzi, hayarishishi hata kidogo, elimu hovyo. Sanasana majengo tu ndio yanaongezeka kutumia ada za watoto. Big no as this is exploitation.
Namshauri Mhe. Magufuli kwa kuwa Shule za Private zinaota kama uyoga, aweke kitengo maalumu chini ya wizara ya elimu ( najua kipo lakini kiimarishwe) ili kiweze kuchambua shule zoote za private na bei zake na huduma zake ili kuja na bei elekezi ambayo ni ya uhalisia. Kitengo hiki ( sijui kama kimeimarishwa- maana tukumbuke miaka ya zamani kulikuwa na very few private schools) hivyo Wizara ya elimu iliweza kumanage.
 
Hata kwenye market economy bado serikali inabakia na role adhimu ya regulation, ndio maana ya uwepo wa regulatory authorities za sekta mbali mbali. Kwa hiyo badala ya kutumia neno hasi " kukurupuka" ungeshauri serikali ianzishe kitu kama National schools regulatory authority NSRA ifanye classification ya shule zote kama ilivyo kwenye mahoteli then itoe bei elekezi; au ifute kabisa SSRA, TACRA, EURA, SUMATRA, POLISI, TISS nk nk ili tubakie kama Banana republic nchi iende hobela hobela, ang'adu ang'adu, mwenye kuua auwae, mwenye nguvu asigine wanyonge etc etc!

Serikali ilipokubali kuingia kwenye mfumo wa Market economy ilijitoa kwenye biashara na kuanza ubinafsishaji, jukumu la serikali likabakia kukusanya kodi.ulikuwa ni ujinga uliovuka mipaka kwa serikali kujitoa ktk kutoa huduma kwa raia wake na ndio matokeo ya mfumuko wa shule nyingi binafsi na mahospital mengi binafsi. wenye shule ni wafanyabiashara waliowekeza kama wafanyabiashara nyingine. cha msingi serikali iboreshe shule zake na ikifanya hivyo kutakuwa na haja gani wazazi wakalipe mamilioni kwa huduma zinazopatikana bure?? soko huru liamue, vinginevyo turudi ya mwaka 1968, nationalization
 
Ni upuuzi wa kiwango cha juu sana..mbona watu wanakula chakula cha elfu 20 wakati kwa mama ntilie ni 1000 na hii wataweka bei elekezi..kweli ujinga ni mzigo

huwezi fananisha suala la elimu,na shibe ya mtu binafsi,hata chakula wakati mwingine usipokula kwa mpango ni tatizo.
YAPO MAMBO NI LAZIMA SEREKALI IYASIMAMIE;-
Tiba
Elimu
mshahara
petroli
gasi
************
 
Lazima serikali iingilia kati,soko huria bila serikaki linasababisha Injustice nyingi
 
Serikali ilipokubali kuingia kwenye mfumo wa Market economy ilijitoa kwenye biashara na kuanza ubinafsishaji, jukumu la serikali likabakia kukusanya kodi.ulikuwa ni ujinga uliovuka mipaka kwa serikali kujitoa ktk kutoa huduma kwa raia wake na ndio matokeo ya mfumuko wa shule nyingi binafsi na mahospital mengi binafsi. wenye shule ni wafanyabiashara waliowekeza kama wafanyabiashara nyingine. cha msingi serikali iboreshe shule zake na ikifanya hivyo kutakuwa na haja gani wazazi wakalipe mamilioni kwa huduma zinazopatikana bure?? soko huru liamue, vinginevyo turudi ya mwaka 1968, nationalization

Sambamba na kutenganisha uongozi na biashara
 
nationalism ndio njia mbadala wa serikali kujimilikisha tena raslimali kama migodi, viwanda, sekta za usafiri nk...
 
Back
Top Bottom