Kwa hili serikali ya Magufuli imekurupuka

Wagabuli

Member
Joined
Nov 28, 2015
Posts
78
Reaction score
144
Serikali ilipokubali kuingia kwenye mfumo wa Market economy ilijitoa kwenye biashara na kuanza ubinafsishaji, jukumu la serikali likabakia kukusanya kodi.ulikuwa ni ujinga uliovuka mipaka kwa serikali kujitoa ktk kutoa huduma kwa raia wake na ndio matokeo ya mfumuko wa shule nyingi binafsi na mahospital mengi binafsi. wenye shule ni wafanyabiashara waliowekeza kama wafanyabiashara nyingine. cha msingi serikali iboreshe shule zake na ikifanya hivyo kutakuwa na haja gani wazazi wakalipe mamilioni kwa huduma zinazopatikana bure?? soko huru liamue, vinginevyo turudi ya mwaka 1968, nationalization
 
Wewe ndio umekurupuka? Hivi unafikiri sheria za kuendesha shule binafsi ni sawa na kuanzisha duka la sigara?
 
shule za serekali si zipo? kuna aliyelazimishwa kumpeleka mtoto wake shule za binafsi? unajua maana ya market economy? una hela unaenda kepski huna unaenda kwa mama ntilie!! tulikurupuka tokea zamani.
 
Magufuri mlimchagua wenyewe acheni awanyooshe ngeke nyie.

Alieichagua ccm hana haja ya kulalamika,karo bweni isizidi 350000, kutwa isizidi 150000.

Hutaki hamia kenya au rwanda.
 
Afu usikute huyu aloandika hii kitu ni mwalim wa Private, tulieni muisome namba huyo ndo Magufuli
 
Walimu wenyewe mnawatumia wale waluosomeshwa na serikali halafu mnataka kuleta mbwembwe
 
Wewe ndio umekurupuka? Hivi unafikiri sheria za kuendesha shule binafsi ni sawa na kuanzisha duka la sigara?

Hakuna uhusiano wa mfano wako na mada husika. Kwa nini basi serikali isiamuru gharama ya taxi kutoka Mwenge kwenda Posta iwe sh 400?

Double Standard sio dhambi, km haujimudu private elekea serikalini. Mishahara ya walimu wa private sio sh kumi kumi unategemea walipwe mawe?
 
Walimu waliosomeshwa na serikali ni wale waliopata alama za chiiiini kabisa. Walimu wa shule za St.Nonino walienda ualimu kwa kuchagua na si kwa sababu walifeli, sema ndio hivyo JINGALAO, huna ubongo wa kutofautisha hilo
 
Hakuna uhusiano wa mfano wako na mada husika. Kwa nini basi serikali isiamuru gharama ya taxi kutoka Mwenge kwenda Posta iwe sh 400?

Double Standard sio dhambi, km haujimudu private elekea serikalini. Mishahara ya walimu wa private sio sh kumi kumi unategemea walipwe mawe?

Double standard kama unavyopenda wewe, Je, unafahamu sheria ya kuanzisha taxi? J, hiyo sheria ni sawa na ya kuanzisha shule?
 
shule za serekali si zipo? kuna aliyelazimishwa kumpeleka mtoto wake shule za binafsi? unajua maana ya market economy? una hela unaenda kepski huna unaenda kwa mama ntilie!! tulikurupuka tokea zamani.

Wazazi wanapeleka watoto wao shule za watu binafsi ili kuepuka matatizo kama haya
 
Magufuri mlimchagua wenyewe acheni awanyooshe ngeke nyie.

Alieichagua ccm hana haja ya kulalamika,karo bweni isizidi 350000, kutwa isizidi 150000.

Hutaki hamia kenya au rwanda.

its service that matters. ni kukurupuka.
 
Ni upuuzi wa kiwango cha juu sana..mbona watu wanakula chakula cha elfu 20 wakati kwa mama ntilie ni 1000 na hii wataweka bei elekezi..kweli ujinga ni mzigo
 
shule za serekali si zipo? kuna aliyelazimishwa kumpeleka mtoto wake shule za binafsi? unajua maana ya market economy? una hela unaenda kepski huna unaenda kwa mama ntilie!! tulikurupuka tokea zamani.

Mkuu kepski ndio nini
 
Wewe ndio umekurupuka? Hivi unafikiri sheria za kuendesha shule binafsi ni sawa na kuanzisha duka la sigara?

No offence mkuu but comment yako inaonesha ni kiasi gani unapenda vya bure,nenda mombasa tu
Watu wawekeze halaf uwapangie bei zako za kiboya una kichaa nn?wekeza na ww kwenye shule za serikali uone kama tutapeleka watoto wetu huko private
 
Ndio, serikali ijikite katika uboreshaji wa shule zake tu, wasimshauri vibaya Mh. Rais katika hili. Serikali isianzishi mivutano isiyo ya msingi, na ambayo itamuharibia sofa Mh. Rais.
 
Back
Top Bottom