Kwa hili nimewapenda TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili nimewapenda TANESCO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by muonamambo, Feb 17, 2012.

 1. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Tanzania ndio nchii pekee ambapo mteja hathaminiwi. Shirika kubwa kama TANESCO wanaamka asubuhi wanaanzisha mgao kwa siku kadhaa bila kutoa taarifa na wako happy kabisa kama kila kitu kinaenda sawa kabisa...

  Watu wote nao wako happy kwamba hata wakikatiwa umeme kwao sio issue kubwa sana kwani hawastaili huduma bora bali bora huduma.

  Haya ni zaidi ya huduma mbovu sana za kuunganishiwa umeme ambapo pamoja na kulipa unaweza subiri miaka 2 mpaka mitatu na huna la kusema....

  Kwa mtindo huo bado unauuziwa nguzo , waya , sijui braketi sijuii nini ..... ili mradi tu nenda rudi na kuombwa hela kusiko isha... na baada ya kununua vyote hivyo bado huwezi sema kwamba ni mali yako....

  Du hii kweli ni kali na kwa hili nimewapenda TANESCO kampuni pekee inayoweza kufanya lolote itakalo na bado watu wakachekelea tu...

  Muonamambo Arusha
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Dawa ya Tanesco ni kupata mpinzani wake. Nakumbuka ile enzi ya simu ya kukoroga ttcl walitutesa sana. Lakini angalieni leo walivyonywea, na bado watu wanavyowafanyia kitu mbaya hawana hata hamu
   
 3. m

  mhondo JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kwao mteja siyo mfalme bali ni kero. Hata kukiwa na matatizo madogo ukiwapa taarifa wanaweza kuja kwenye eneo la tukio baada ya siku mbili na hapo ni baada ya kupiga simu sana (kuwasumbua). Sijui hawaoni kama wanajipunguzia mapato?.
   
 4. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Haswa tumechoshwa na huduma mbaya kupita kiasi kama za TANESCO. MGAO MWAKA MZIMA... mwaka jana bunge lilikataa kupitisha bajeti ya wizara ya nishati kwa kile tulichoelezwa waje na mpango mkakati wa kumaliza tatizo la umeme... baadaye tukaambiwa kuna mpango wa kuingiza MEGAWATI 300 ZA DHARURA...

  SASA MGAO WA KIMYA KIMYA HATA AIBU HAMUONI JAMANI... kweli nimeamini its ONLY IN TANZANIA....

  YAANI MAMBO SHAGLABAGLA.....
  kinachoniudhi zaidi wateja tupo kimya hivi hatuwezi ishitaki TANESCO IL IKUKOMESHA UJINGA HUU
   
 5. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Tatizo Serikali inawalea hawa TANESCO, makampuni yapo yenye uwezo wa kuzalisha Umeme nchini. lakini Serikali inataka kama wanaweza wazalishe kisha Waiuzie Tanesco na siyo kuuza kwa Wananchi moja kwa moja. Ndio maana wanapata kiburi hawa Tanesco.

  mfano hii bei mpya ya Umeme ni mzigo sana kwa mwananchi wa kawaida na hata kwa wawekezaji. Inachangia kiasi kikubwa kuwe na mfumuko wa bei katika bidhaa.

  IFIKIE SASA WAKATI TANESCO IBINAFSISHWE!!!!!!!!!!!!!!


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 6. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tatizo halipo Tanesco,ni Serikali iliopo madarakani,(Richmond,IPTL,)na wengine kama hao. ndiyo sababu Tanesco hawana wasiwasi wowote kwakua wanajua.
   
 7. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kama Tatizo sio TANESCO mbona sijawaona wakifunguka na kuwaambia wa Tz ubabe wanaofanyiwa na serikali na jinsi unavyowaathiri kutoa huduma ama tuwaone wakurugenzi wao wakijiudhuru kupinga kuingiliwa na serikali...? Naona wao wako happy na kwa kuwa hawajali wateja wao wanaona sawa tu na kundeleza rushwa zao za kugawa umeme...

  kuna Tatizo kubwa TANESCO zaidi unavyofikiria....
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,026
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hata mapato yakipungua,mishahara yao iko palepale,hawana cha kupoteza.
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  TANESCO mteja kwao ni ***** au ****.
  Uliona wapi duniani kampuni inatoa Tangazo la kudiscourage watu kutumia bidhaa yake ie kubana matumizi ya umeme iwe nyumbani au viwandani.
   
 10. n

  ngokowalwa Senior Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu, Mpinzani wa TANESCO atatokea tu kama utaratibu wa sasa wa kila mwekezaji kwenye umeme lazima ahakikishiwe mshiko wake safi wa capacity charge amezalisha hajazalisha lazima alipwe na TANESCO la sivyo nani ataacha kujizolea hela ya uhakika akasumbuke kufukuzana na wateja wa umeme.
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo tatizo kubwa la monopoly na suluhisho lake ni kupata mbadala wake
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ukiwa mlevi wa kitu flani ni hatari sana na sasa wao wamelewa na kutegemewa wao tu
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa serikali tuliyonayo ni ngumu sana kupata haki kwakutegemea mahakama labda tutafute njia mbadala
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi tunaweza kusema serikali inayokumbatia mambo yasiyokuwa na maendeleo pamoja na maovu
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ukiongeza na tatizo la serikali inakuwa janga
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ishajiona yenyewe ni yenyewe na hakuna nyingine zaidi ya yenyewe pasipokujifunza toka kwa wenzio TTCL ambayo kwa sasa inajuta
   
 17. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kwa Kuwa wawekezaji wanaingia nayo mikataba ya kuikamua kwa capacity charge hawaoni umuhimu wa kuwekeza kwenye distribution....

  Kweli Tz ni kichwa cha mwendawazimu....
   
 18. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukingatwa na mbwa usimlaumu mbwa mwenye kushitakiwa ni mwenye mbwa. Serikali ndiyo mmliki wa Shirika la Ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO ) kwa asilimia 100% Kuilaumu tanesco ni sawa na kumlaumu mbwa kwanza hasemi na pia ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa? Ngeleja na Tanesco yake wameshaingia MoU na makampuni kibao ikwepo Symbion/Aggreko makampuni ya Rostam lakini wamekataa kuingia MoU na NDC na Kampuni ya Makaa ya mawe ya Ngaka kule Songea ambako wako serious kuzalisha 400Mw tatizo Kikwete amekataa mpaka walipe hisani aliyomwahidi Rostam this is a big shame huo umeme tutaupata akishakufa au kuachia madaraka baada ya 2015 kwani kusanifu na kujenga njia kuu ya umeme Hadii Makambako kwenye gridi ya Taifa itachukua sio chini ya miaka 3 kwa fast truck tuendelee kugawiwa Giza
   
 19. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,080
  Likes Received: 4,664
  Trophy Points: 280
  I am so sick when i think of Tanesco, higher electricity rates, higher monthly service charges, ALMOST ZERO SERVICES TO CUSTOMERS, upate tatizo la LUKU, utajua these guys are sleeping day & 9t, i changed to higher solar power 320 watts enjoying life now. I hate Tanesco
   
 20. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hongera kaka kwa kuweka solar maana huu ****** wa Tanesco Unaweza pata kichaa kwa kuwafuatilia.
   
Loading...