Kwa hili mh, naibu spika umetumia ubabe

Michael Scofield

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
1,225
471
Katika kipindi cha maswali na majibu cha leo, naibu amejionyesha ni jinsi gani alivyo tarishi wa CCM, Bahada ya kwisha kipindi cha maswali na majibu, Mh, Silinde alomba kutoa taarifa kwa naibu spika wa bunge Job Ndugai.
Taarifa ilikuwa inamhusu waziri mkuu. Naibu spika kwa kutumia kanuni ya 68 ya bunge ambayo mh, Silinde inampa haki yake ya msingi kufanya hivyo. bahada ya hilo mh Mnyika akaomba muongozo, kutumia kanuni ya 133 ya bunge kwa mujibu wa ibara ya 53a ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Huu ni ubabe wa kunyima haki na fursa ya wabunge katika kutoa ufafanuzi katika mambo yanayohusu mustakhbali wa nchi yao.
Mie nashindwa kuelewa, kwa nini ofisi ya spika inamkingia kifua waziri mkuu pale anapoelezwa ukweli.

Hivi naibu spika alijua taarifa ilyotaka kuulizwa na mh, Silinde? je kama waziri mkuu amepotosha umma kwa majibu aliyotoa ambayo hana uhakika na uthibitisho.

Mara nyingi majibu ya waziri mkuu yanakuwa ya kisanii tu, na hayakidhi.
Binafsi sioni umuhimu wa kuwa na hiki kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu, ni kupoteza muda tu kama majibu yenyewe yanatolewa KIMASABURI namna hii.
Najihisi kichefuchefu nikikumbuka naibu spika alivyokuwa anamtunishia misuli MNYIKA.
 
Inabidi wananch tuandae maandamano kupinga uongozi mbovu wa spika na naibu wake,rais, wazir mkuu na mawazir wngn la sivyo ITAENDELEA KULA KWETU
 
Back
Top Bottom