Kwa hili Mbowe ndiye anayeiua CHADEMA kwa kuhofia uwezo mkubwa wa Zitto

Ha ha ha mbona hii habari inaonekana kuwaumiza vichwa sana watu wa CCM, Kama hawa mabwana ni wazuri CCM wachukueni. jirani yako akifukuza mwanamke au mwanamke akimkacha mwanaume nawe unamwona anafaa oa au olewa naye, ndo dawa pekee ya kudhihirisha kuwa huyo mtu ni mzuri.
 
Kwa mtu yeyote mwenye maono ziito akiwa mwenyekiti CDM hatakiacha chama nikiwa salama na imara jama kilivyo sasa ni uroho tu wa madaraka nakuhakikishia hata akienda huko CCM hawezi kuwa salama yake nwani CCM wanajua kuwa ni mtu hatari na mroho wa madaraka atataka hata kugombe urais kwa tuketi ya ccm
 
Inashangaza sana Magamba kuumia na uamuzi wa CDM , kwani nani aliumia wao wakimweka Tembo dentist kuwa Katibu mkuu wao? Kamaliza tembo wote.

CDM haiwezi kuwakumbatia washenzi wanoboma nchi kama ninyi. Mbinu zenu zimegonga mwamba.
 
Maamuzi ya CDM hayatuhusu CCM! Nyie mna chama chenu na sie tuna chama chetu!

Mkitaka kufukuza kila mwanachama haitihusu! Kilichopo Mbele yetu kwa sasa ni kuimarisha chama vijijini na kukagua Ilani ya CCM
 
Wewe Team Lowasa na cdm wapi na wapi bhana ! Usilete uongo humu , utakula ban nzito sana ! Unaweza kuthibitisha kwamba Mengi anaipa hela cdm ? Eti asilimia 98 cdm wameletwa na zito ! Ndiyo mnavyodanganyana ?
 
Uimla, uroho wa madaraka na ubinafsi ndio vimekuwa chimbuko la anguko la vyama vyote vilivyokuwa maarufu. Angalia ilivyoanguka nccr ya 1995, tlp na cuf (utazidi kuona ikizikwa hata zanzibar 2015).
 
Mleta mada, nani alikwambia kuwa chadema wana cheo cha katibu mwenezi wamkoa?au Huyo wa morogoro unayemwongelea ni wa ccm?
 
Matumizi ya fedha za taasisi.
Hakuna mtu anayejua hivi sasa
fedha za chama zinatumikaje zaidi
ya kakikundi ka watu watatu yaani
mkuu kabisa, mtendaji mkuu na
mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao
hayaheshimiki tena na mabwana
hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010
vikao halali vilielekeza kiasi na
aina ya fedha ambazo
hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya
uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu
akaunti hiyo haina fedha bali
hakuna akaunti yoyote yenye
fedha. Watu watatu ndo
wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya
kikao cha juu mno cha hivi
karibuni kilichoamua kwamba kiasi
cha fedha inayotoka serikalini
kipelekwe kwenye mikoa na wilaya
na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano
maamuzi hayo hayajatekelezwa.
Lakini kuna michango ya watu
binafsi kama yule mtanzania
mwenye asili ya kihindi, hizo nazo
hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na
hatimaye zimetumikaje. Hapo
hatujataja fedha zinazopatikana
kutoka kwenye fundraising events
mbalimbali kama ile ya Dar es
salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na
walioendesha hizo fundraising,
uaminifu wao kwenye masuala ya
fedha ni questionable!!
hivi kuhoji haya ni kosa??
 
Kupeana vyeo kiundugu na kiswahiba; hii ndio Demokrasia ya CHADEMA?
WanaJF!

Kama miongoni mwetu kutakuwa na watu wenye hofu, wasiwasi na woga wa kuhoji mambo yanayo kinzana na usawa na haki basi huyo sio sehemu ya wapenda mabadiliko ya kweli na wenda akawa kikwazo katika kuyafikia mabadiliko.

katika kulifafanua hili la kuona usawa, haki na demokrasia vikitendeka na kuonekana kutendeka, ningependa tujiangaze kwenye nafasi za viti maalumu vya CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, nafasi hizi za viti maalumu ndani ya CHADEMA hupangwa na viongozi wa chama hicho na kiukweli hakukuwa na uwazi na ukweli katika kupanga nafasi hizo za viti maalumu.

Kwa mfano, mwenyekiti wa CHADEMA alipoulizwa kuhusu vigezo vilivyo tumika katika kugawa nafasi hizo hakuwa na jibu la kueleweka na badala yake aliishia kujiuma uma tu na kisha kusema hayupo tayari kulizungumzia hilo. Lakini baada ya kubanwa kisawa sawa ndipo akafunguka kuwa vigezo vilikuwa ni elimu, uzoefu, muda na jitihada katika kukitumikia chama.

Ifuatayo ni orodha ya wabunge wa viti maalumu wa CHADEMA kutoka kwenye majimbo mbalimbali;

1. Christina Lissu, huyu ni dada yake na Tundu Lissu (mb) na pia ni kiti maalumu kutokea Iramba mashariki. Huyu hana hata kigezo kimoja kati ya hivyo ambavyo bwana Mbowe alidai vimetumika kumpa ukiti maalumu.

2. Rose Kamili, huyu alikuwa mke wa Dr Slaa kabla ya kuwa na Josephine. Huyu nae pia hana kigezo hata kimoja kati ya hivyo alivyo vibainisha Mbowe.

3. Lucy owenya, huyu ni shemeji wa mzee Ndesambulo ambae ni mlezi wa CHADEMA na pia ni mbunge wa Moshi mjini. Aidha, huyu nae hana kigezo hata kimoja kati ya alivyo vitaja Mbowe.

4. Grace Kiwelu Ndesambulo, kama jina linavyo jieleza, huyu ni binti wa mzee Ndesambulo wa kumzaa na pia ni mbunge wa viti maalumu kutokea Moshi mjini.

MJADALA,

Hivi ndani ya CHADEMA hakuna makamanda wenye uwezo nje ya hawa makamanda ambao wana mahusiano na viongozi wa chama?

CHADEMA walijifikiria nini kutoa madaraka kwa watu wenye mahusiano nao ya kiundugu ilhali CHADEMA imekuwa ikiinyooshea kidole CCM kuwa ni chama cha familia?

Kwa hali kama hii ya CHADEMA kuwapatia madaraka watu wenye mahusiano nao aidha kiundugu ama kwa namna nyingine yoyote ile, ni kosa kwa watanzania kukiita chama hicho ni cha kifamilia?

kwa hali hii tu ya ngazi ya chama tuna shuhudia ukiritimba wa aina hii, vipi CHADEMA ikitwaa dola hali itakuwaje pale Ikulu na maeneo mengine ya kiutendaji?​
 
Wakati Walid Kaborou alipotoka CHADEMA alikua na nguvu sana na chama kilikua hakina mvuto kama ilivyo sasa. Kila jambo na wakati wake, kama tunaamini kuna uwezekano wa kujenga hoja zikakubalika ni vyema kufuata utaratibu uliowekwa kutumia mbinu chafu hakutasaidia chochote kwa hatima ya nchi,chama au mtu. Wakati utakapofika kila jambo litakua hadharani tutajua tu mbivu na mbichi. Nchi, chama au watu walipuuza maslahi ya wengi kwa kutangulizi ubinafsi hatma yake hua yakusikitisha. Dhahabu husafishwa kwa moto, baada ya hapo pia thamani yake huongezeka,kama ni dhahabu ya kweli lakini. Tusubiri tuone dhahabu ya kweli ni ipi!!
 
Back
Top Bottom