Kwa hili, mama umenikosea huruma Mimi mwanao.

Vamigo

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
456
Reaction score
994
Wakuu kuanzia majira ya saa 1 usiku napitia kipindi kigumu Cha msongo wa mawazo, jioni hii ya leo imekua ngumu licha ya kupooza mawazo kwenye game ya timu yangu pendwa ya yanga iliyo ibuka na ushindi mnono.

Wakuu juzi Kati hapa niliwaletea kisa Cha kua "Nilianguka, nimeinuka na kuanza upya japo kua nachechemea" nilitoa mkasa wangu mzima kwa mlio bahatika kuusoma nadhani mtaukumbuka. Unaweza kupitia hapa...[emoji117]

Back to my story, nilimuachiaga mama yangu mzazi ofisi yangu aisimamie baada ya kukumbwa na dhoruba pale ofisini kwangu, mm niliamua kutafuta changamoto kwingine, baada ya Kama mwaka mmoja Sasa huko niliko kwenda Mambo yangu yalienda tofauti na mategemeo yangu kifupi maisha yalizidi kua magumu kwangu.

Baada ya kutafakari mstakabari wa maisha yangu niliamua kumuhusisha mama kua Sasa umefika wakati wa kurejea ofisini kwangu ili nijipange upya.
Mama alinikubalia na tukapanga siku ya kupiga hesabu na tarehe ya kukabidhiana. Skua na namna kumchomoa maza pale ofisni.

Kuna sku nilienda nyumbani kujadiri na mama kuhusu maendeleo ya ofisi, mama alinifungukia kwa aibu na uoga kua pale hakuna chochote alicho ingiza, nilishikwa na mshangao wa ndani kwa ndani, inakuaje mama hajaingiza chochote yapata mwaka mzima.!? Wakati nyumbani alikua akiishi pekeake?

Mama niliacha nimemlipia Kodi ya miezi 6, nikamuachia mtaji wa sh 500,000 kuzungushia pale, (ofisi ni M-pesa) kakaa pale mwaka mzima na alikua anafanya biashara yake pale ya urembo. Lakini sku napiga nae hesabu alinikabidhi 1,115,000/ wakati huo ananikabidhi alikua pia amekopa kwenye huduma ya wezesha sh 300,000/=

Kuna siku, tulikua mm, dada angu mkubwa na maza, tukijadiri mstakabari wa mama baada ya kunipisha pale ofisini, tulipendekeza kua maza tumtafutie ofisi ya M-pesa, kwakua mm Nina till mbili, Basi moja nitampa afanyie kazi, lakini kwenye kile Kias alicho ingiza tutakigawana yeye kaingiza Kama lakisita hivi alipo kua pale, maanake tutagawana 300k kwa Kila mtu. Mama alianza harakati za kutafuta site alifanikiwa kupata, akalipia ile site.

Sasa Leo kaja anaiambia kua j3 anataka aanze biashara pale hivyo tupige hesabu nimpe hela. Nikamuuliza hesabu gani ambazo unataka mama .? Akanambia si utoemo ile hela yako kwani sku ile nilikukabidhi sh ngap.?

Mmmh.! Hesabu za maza nikawa sizielewi nikampa nafasi ya kufanya anavyo hitaji yeye. Maana yake tulichukua mtaji alio niachia ikiwa ni pamoja na vocha Total 1115000 - 500000 = Kuna pesa nyingine baba walimtuaga ilikua pale kwangu Kama 125,000. Mama nikamkabidhi sh 700,000 Mimi akaniacha na sh 500,000 tu ambayo ni pamoja na vocha, float za mitandao yote na cash.

Kinacho Nipa mawazo ni shida nilizo nazo kwa Sasa ambazo mama angu mzazi anazielewa,mama Amekua mtu wangu wa karibu sana anae fahamu Kila changamoto nayo pitia na hatua nilizopo.

Natakiwa kulipa kodi ya pango la biashara sh 600k mwezi wa 11 mwaka huu,mwezi wa 10 pia natakiwa kulipia pesa ya Kodi ya sehemu ninayo ishi.

Najiuliza kwanini mama amekosa huruma kwa mwanae kiasi kwamba kaamua kuchukua kiasi kile Cha biashara na kuniacha na mtaji kidogo ambao hautoshi kwa biashara ile wakati yeye nyumbani, anachakula Cha kutosha ( gunia la mahindi) na Kama wiki moja mbele atakua pekeake nyumbani. ( Dogo aliepo atarudi masomoni mda si mrefu)

Najiuliza ikiwa mama halipi kodi nyumbani, baba yupo na anamhudumia, sisi watoto wake tupo hawezi lala njaa hata Kama nikidogo tutampa, kwanini mama amekosa uvumilivu kwa mwanae nikalipa Kodi zote ambazo anafahamu kua zipo mbele yangu na Nina takiwa kuzilipa Kisha baadae ndo atafute ofisi afungue, haraka ya nini.?

Kiukweli nimekosa namna, nimekosa jinsi ya kumzuia, wakati namkabidhi nilizuia hisia asigundue Kama sjapendezwa na hili, na ni mama angu sa nitafanyaje.?

Kiukweli Nina mawazo sana namna ya kuvuka hizo Kodi zilizopo mbele yangu, kiukweli mama amekosa huruma kwa mwanae maana mama angu anafahamu Kila stuation niliyo pitia na ninayo pitia. Nimeumia sana.

Mwisho: inaweza kua sjapangilia vizuri kwenye uandishi ila nadhani wakuu mmenielewa. Karibuni kwa faraja zenu naumia kimya kimya, Sina mtu wa kumlilia ndo maana nimeandika haya ili nipate maoni kutoka kwenu.
 
ꨄ︎Mwaka mzima hujafuatilia hesabu? ulikua kuzimu au?
Dah! Nilitoka nikaenda mikoa ya mbali sana, nilikaa miezi 8 mpaka kurudi mkoa nilio kuwepo. Maana yake nilimuachia dhamana nikiamini ni mama anauchungu na ataipambania ofisi yangu.

Kilicho niumiza ni kiasi alicho chukua wakati anayafahamu yaliyopo mbele yangu.
 
Heri Yako unae mama hata wa kukupa stress

Siku Moja utatamani awepo hata achukue hesabu yote wewe uanze upya zero kabisa.
[emoji123][emoji123][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nilifuatilia ile story yako ya Mpesa ulisafiri ukamuachia mama, we issue zikafeli umerudi.

Sasa mzee kwanini usijaribu issue nyingine naonaga kama Mpesa zinakuaga slow sana kurudisha. Au unaonaje.

Au fanya 2 in 1 mzee, uza nguo au electronics ndogo ndogo (chaja, earphones, memory card, flash, makava baadhi..) uku ukiendelea na Mpesa.
 
Heri Yako unae mama hata wa kukupa stress

Siku Moja utatamani awepo hata achukue hesabu yote wewe uanze upya zero kabisa.
Hahaha ukiwa hauna sawa. Ila ukiwa naye wa hivyo tena anaboa.
 
Nilifuatilia ile story yako ya Mpesa ulisafiri ukamuachia mama, we issue zikafeli umerudi.

Sasa mzee kwanini usijaribu issue nyingine naonaga kama Mpesa zinakuaga slow sana kurudisha. Au unaonaje.

Au fanya 2 in 1 mzee, uza nguo au electronics ndogo ndogo (chaja, earphones, memory card, flash, makava baadhi..) uku ukiendelea na Mpesa.
Hizo biashara zinapendwa na watu wavivu au uwe na mtaji mkubwa sana. Laini nyingi plus uwakala wa mabenki.
 
Mkuu

Pole sana kwa mkasa uliokupata.

Kwanza kubali umeshuka kimapato na amini kuwa,Wewe ni sababu kubwa ya hali uliyonayo.

Kabla ya kuhamishia mpira kwa mtu au hali yeyote,Amini Kuna sehemu ulikosea au umekosea hata unapitia kipindi ulichonacho hivi Sasa.

Wanadam tunatofautiana , Hivyo siku nyingine jifunze kuzungumza hisia zako na yule ambae unadhani anapaswa kujua.

Usiamini yale uliyonayo kichwani na unatamani yatokee Kila mmoja anayajua na atafata vile nafsi yako inavotamani.

Lakini pia jifunze kutoa kwa kadiri ya uwezo,Mzazi ni nguzo muhimu Kwenye maisha.Ila huduma kwake iendane na uwezo ulionao.

Bado hujachelewa,Jifunze kuwa na vipaumbele siku zote katika maamuzi unayofanya.

Chagua,Unataka kurekebisha hisia zako juu ya MAMA,Au kuachana na mawazo juu yake na kutafuta mbinu za kukusaidia kuinuka kiuchumi?

Sisi tutaishia tu kuandika,Ila uzito wa unayopitia ,pasi na shaka weye ndo waujua.

Una nafasi ya kusimama tena mkuu.

Moyo ukiwa na maumivu hautoona mazuri kwa mwingine kwa sababu huwezi toa kitu usichonacho,Mfano huwezi penda kama huoni upendo ndani yako.

Niko tayari kusaidia kwa kutenga muda kuona namna gani utakabiliana na hali unayopitia.

Karibu muda wowote.
 
hyo hela yako uza bhange soon unatajirika achana na huduma za fedha
 
"BUSINESS ENTITY CONCEPT" inasema usichanganye undugu, mapenzi au urafiki na biashara UTAANGUKA vibaya mno.

Mwambie ukweli mama yako, kama kiukweli alikuzaa na anakupenda atakuelewa ila kama ni mdangaji wa mjini na yupo kimaslahi zaidi atanuna!.
 
Wakuu kuanzia majira ya saa 1 usiku napitia kipindi kigumu Cha msongo wa mawazo, jioni hii ya leo imekua ngumu licha ya kupooza mawazo kwenye game ya timu yangu pendwa ya yanga iliyo ibuka na ushindi mnono.

Wakuu juzi Kati hapa niliwaletea kisa Cha kua "Nilianguka, nimeinuka na kuanza upya japo kua nachechemea" nilitoa mkasa wangu mzima kwa mlio bahatika kuusoma nadhani mtaukumbuka. Unaweza kupitia hapa...[emoji117]

Back to my story, nilimuachiaga mama yangu mzazi ofisi yangu aisimamie baada ya kukumbwa na dhoruba pale ofisini kwangu, mm niliamua kutafuta changamoto kwingine, baada ya Kama mwaka mmoja Sasa huko niliko kwenda Mambo yangu yalienda tofauti na mategemeo yangu kifupi maisha yalizidi kua magumu kwangu.

Baada ya kutafakari mstakabari wa maisha yangu niliamua kumuhusisha mama kua Sasa umefika wakati wa kurejea ofisini kwangu ili nijipange upya.
Mama alinikubalia na tukapanga siku ya kupiga hesabu na tarehe ya kukabidhiana. Skua na namna kumchomoa maza pale ofisni.

Kuna sku nilienda nyumbani kujadiri na mama kuhusu maendeleo ya ofisi, mama alinifungukia kwa aibu na uoga kua pale hakuna chochote alicho ingiza, nilishikwa na mshangao wa ndani kwa ndani, inakuaje mama hajaingiza chochote yapata mwaka mzima.!? Wakati nyumbani alikua akiishi pekeake?

Mama niliacha nimemlipia Kodi ya miezi 6, nikamuachia mtaji wa sh 500,000 kuzungushia pale, (ofisi ni M-pesa) kakaa pale mwaka mzima na alikua anafanya biashara yake pale ya urembo. Lakini sku napiga nae hesabu alinikabidhi 1,115,000/ wakati huo ananikabidhi alikua pia amekopa kwenye huduma ya wezesha sh 300,000/=

Kuna siku, tulikua mm, dada angu mkubwa na maza, tukijadiri mstakabari wa mama baada ya kunipisha pale ofisini, tulipendekeza kua maza tumtafutie ofisi ya M-pesa, kwakua mm Nina till mbili, Basi moja nitampa afanyie kazi, lakini kwenye kile Kias alicho ingiza tutakigawana yeye kaingiza Kama lakisita hivi alipo kua pale, maanake tutagawana 300k kwa Kila mtu. Mama alianza harakati za kutafuta site alifanikiwa kupata, akalipia ile site.

Sasa Leo kaja anaiambia kua j3 anataka aanze biashara pale hivyo tupige hesabu nimpe hela. Nikamuuliza hesabu gani ambazo unataka mama .? Akanambia si utoemo ile hela yako kwani sku ile nilikukabidhi sh ngap.?

Mmmh.! Hesabu za maza nikawa sizielewi nikampa nafasi ya kufanya anavyo hitaji yeye. Maana yake tulichukua mtaji alio niachia ikiwa ni pamoja na vocha Total 1115000 - 500000 = Kuna pesa nyingine baba walimtuaga ilikua pale kwangu Kama 125,000. Mama nikamkabidhi sh 700,000 Mimi akaniacha na sh 500,000 tu ambayo ni pamoja na vocha, float za mitandao yote na cash.

Kinacho Nipa mawazo ni shida nilizo nazo kwa Sasa ambazo mama angu mzazi anazielewa,mama Amekua mtu wangu wa karibu sana anae fahamu Kila changamoto nayo pitia na hatua nilizopo.

Natakiwa kulipa kodi ya pango la biashara sh 600k mwezi wa 11 mwaka huu,mwezi wa 10 pia natakiwa kulipia pesa ya Kodi ya sehemu ninayo ishi.

Najiuliza kwanini mama amekosa huruma kwa mwanae kiasi kwamba kaamua kuchukua kiasi kile Cha biashara na kuniacha na mtaji kidogo ambao hautoshi kwa biashara ile wakati yeye nyumbani, anachakula Cha kutosha ( gunia la mahindi) na Kama wiki moja mbele atakua pekeake nyumbani. ( Dogo aliepo atarudi masomoni mda si mrefu)

Najiuliza ikiwa mama halipi kodi nyumbani, baba yupo na anamhudumia, sisi watoto wake tupo hawezi lala njaa hata Kama nikidogo tutampa, kwanini mama amekosa uvumilivu kwa mwanae nikalipa Kodi zote ambazo anafahamu kua zipo mbele yangu na Nina takiwa kuzilipa Kisha baadae ndo atafute ofisi afungue, haraka ya nini.?

Kiukweli nimekosa namna, nimekosa jinsi ya kumzuia, wakati namkabidhi nilizuia hisia asigundue Kama sjapendezwa na hili, na ni mama angu sa nitafanyaje.?

Kiukweli Nina mawazo sana namna ya kuvuka hizo Kodi zilizopo mbele yangu, kiukweli mama amekosa huruma kwa mwanae maana mama angu anafahamu Kila stuation niliyo pitia na ninayo pitia. Nimeumia sana.

Mwisho: inaweza kua sjapangilia vizuri kwenye uandishi ila nadhani wakuu mmenielewa. Karibuni kwa faraja zenu naumia kimya kimya, Sina mtu wa kumlilia ndo maana nimeandika haya ili nipate maoni kutoka kwenu.
Ndio wazazi hao mzee
 
Pesa inaweza kuharibu..... anyway at least shukuru Kuna pa kuanzia. Angekuwa mke ndio ungeona chamoto zaidi
 
Maisha huwa yanaacha kukuumiza pale tu yanapomaliza kukufunza, uzembe ni wako
 
Heri Yako unae mama hata wa kukupa stress

Siku Moja utatamani awepo hata achukue hesabu yote wewe uanze upya zero kabisa.
Huu ni unaa,
unayajua maumivu ya kuanza upya?
Then jamaa kasema mama anavyo vyanzo vingine kwanini amchukulie kijana wake kila kitu?

Washwahili wanasema "mzazi hamuui mtoto,ila mtoto ndiye humuua mzazi"(funzo,mzazi anatakiwa ajinyime kwa ajili ya mustakabali mzuri wa mtoto wake na siyo kinyume chake!

Kijana;mimi niseme tu "hawa ndo aina ya wazazi na ndugu zetu wa kimaskini/kiafrika tulionao.Usikate tamaa.

Embu angalia hiyo kodi ni kubwa mno,kwanini usiingie kwenye mishe mingine zisizohitaji makodi rukuki kihivyo.Yaani kwa kodi na pango ya hapo unapotaka kuendelea napo ni kubwa kuliko mtaji,jiulize hiyo kodi ukizungusha hata kwa mwaka itakuwa imerudi na faidi juu??
Pia kumbuka ktk kipindi chote utakuwa ukihitaji kula na kuvaa,je haya yote yatawezekana kwa kutegemea biashara hii??

Kuna mdau kasema kama utafanya hiyo,basi ichanganye na mambo mengine ili kuongeza faida.

Kwakuwa tayari uposehemu rasmi na leseni nadhani unazo basi zitumie kuombea mkopo mdogo(kulingana na mahitaji) kisha weka bidhaa mbalimbali zitakazo kuletea faida mapema.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom