Habari za mida hii wadau wa Jf ,Leo nimepatwa na tatizo naomba msada wa ufumbuzi kidogo,swala lipo kama hivi,mnano tarehe 21/07/2018 nilifanya biashara na jamaa mmoja ambaye niliwasiliana naye kupitia simu. Baada ya makubaliano ya biashara yetu ,then akanitumia pesa na Mimi nikamtumia mzigo kumbe wakati huohuo mwenzangu hakuwa na lengo nzuri kibashara ,Leo tarehe 24/07/2018 nimepokea ujumbe kutoka Airtel kwamba pesa iliyotumwa kimakosa kutoka namba X imerejesha (kurudishwa) kwa aliyeituma kimakosa .Baada ya kufanya mawasiliano na airtel wakaniambia niwapigie voda kwa sababu mteja aliyetuma pesa ndiye aliyeomba pesa irudishwa kwamba imetuma kwangu kimakosa,kila nikipiga simu voda wananiambia wapigie airtel ndio walioruhusu pesa irudishwe.Sasa swali langu ni kwamba haya makampuni ya simu yanawezaje kurudishwa muhamala uliofanyika bila hata kunipigia simu? Pia haki ya mteja kama Mimi inatuzwaje kama mtu anaweza tu kupiga simu ya kusitisha muhamala na makampuni yakafanya hivyo?