Kwa hili la uchaguzi wa Mameya, CCM mmetutia aibu!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Kwa hili lazima tuseme, kwamba kama mwanachama halikunifurahisha hata chembe.
Ni jambo lililo wazi kuwa baada ya uchaguzi mkuu, CCM tumepigwa bao hasa hapa jijini Dsm.

Halmashauri nyingi waliochaguliwa ni wanachama wa vyama vya upinzani kwa wingi zaidi kuliko wa chama tawala.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kiuhalisia.

Dhambi kubwa na ya kutia aibu, ni kuleta mamluki toka Zanzibar, watuamulie mambo ambayo kwanza hawayajui ya DSM, na pili si wawakilishi wa wananchi wa DSM.
Katika kata yangu, diwani alichaguliwa wa CHADEMA, mimi nilimpa kura yangu(wa CCM) alishindwa vibaya.
Kushindwa kwa huyo mwana CCM mwenzangu kunatokana na kutoshughulikia kero , hasa za barabara huku Mbezi.

Sasa leo huyu mwana CHADEMA TUTAMPIMA KWA KIGEZO HICHO HICHO.

Sasa leo tunaletewa mamluki wa kutusaidia kuamua mambo yetu?
Mbaya zaidi ni kususia uchaguzi.
Hii ni AIBU KUBWA!
Huu ni Ukurunzinza usiokubalika.
 
Aliyezoea kushindwa akishindwa anakuwa mnyenyekevu kukubali matokeo lkn anaposhindwa alaiyezoea kushinda ni balaa!! ndo hayo ya Znbar.
 
Yaliyotokea Ilala yamenikumbusha miaka kadhaa iliyopita ( na ninadhani hapo ndio neno kutia mpira kwapani lilipoanza) Timu yangu ya Simba ikiwa inacheza na Yanga ilipofika halftime ikaamua kutokurudi uwanjani.
Hakuna kitendo kiliwahi kunisononesha kama kile hadi leo, kwanini ukimbie mtanange? Sii bora ushindwe kiume kama walivyoshindwa kwa heshima kule Kinondoni?
Najua kwa Ilala walioweka kwapani mpira ni pamoja na Mbunge Zungu, nadhani huyu hata kule mjengoni kama atataka kuwania uenyekiti abwagwe tuu hafai kabisa.
Mleta mada pole sana, najua unavyojisikia kwa kitendo hicho cha kuweka mpira kwapani.
 
Haiwezekani Ilala kusiwepo hata na kura moja ya mwana ccm kuna kitu hapa ,mshaanza fitina zenu ,muda utatuambia
Musa azan zungu ( aliyetaka kuwa spika wa bunge ) aliongoza madiwani wa ccm kuweka mpira kwapani , hakuna jambo lingine lililojificha mjomba .
 
Halafu Magufuli ndio anajifanya hataki kuwaweka upinzani karibu mbona yeye mwenyewe ataisoma namba ,CCM ni zaidi ya rais wa nchi ,mimi sioni ni vipi unakitenganisha chama na serikali kwa hii katiba tuliyonayo ya chama kimoja japo tupo kwenye mwamvuli wa demokrasia ya kinafiki (vyama vya vingi) ni swala la muda tu nakuambia ,Yaani sijapata kuona mabingwa wa fitina kama CCM

Hajateua baraza la mawaziri ,wakaanza kumletea picha za nguruwe ,sijui na kuchoma ngazi iliyokufikisha ulipo ,mimi yangu macho tu
 
Kwa hili lazima tuseme, kwamba kama mwanachama halikunifurahisha hata chembe.
Ni jambo lililo wazi kuwa baada ya uchaguzi mkuu, CCM tumepigwa bao hasa hapa jijini Dsm.

Halmashauri nyingi waliochaguliwa ni wanachama wa vyama vya upinzani kwa wingi zaidi kuliko wa chama tawala.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kiuhalisia.

Dhambi kubwa na ya kutia aibu, ni kuleta mamluki toka Zanzibar, watuamulie mambo ambayo kwanza hawayajui ya DSM, na pili si wawakilishi wa wananchi wa DSM.
Katika kata yangu, diwani alichaguliwa wa CHADEMA, mimi nilimpa kura yangu(wa CCM) alishindwa vibaya.
Kushindwa kwa huyo mwana CCM mwenzangu kunatokana na kutoshughulikia kero , hasa za barabara huku Mbezi.

Sasa leo huyu mwana CHADEMA TUTAMPIMA KWA KIGEZO HICHO HICHO.

Sasa leo tunaletewa mamluki wa kutusaidia kuamua mambo yetu?
Mbaya zaidi ni kususia uchaguzi.
Hii ni AIBU KUBWA!
Huu ni Ukurunzinza usiokubalika.
Kwa mara ya kwanza nikupe bonge la LIKE,umekuwa mwana ccm wa kwanza kukemea udhaifu baada ya marehemu kolimba kufanya hivyo,hongera sana mkuu"masopakyindi
 
Halafu Magufuli ndio anajifanya hataki kuwaweka upinzani karibu mbona yeye mwenyewe ataisoma namba ,CCM ni zaidi ya rais wa nchi ,mimi sioni ni vipi unakitenganisha chama na serikali kwa hii katiba tuliyonayo ya chama kimoja japo tupo kwenye mwamvuli wa demokrasia ya kinafiki (vyama vya vingi) ni swala la muda tu nakuambia ,Yaani sijapata kuona mabingwa wa fitina kama CCM

Hajateua baraza la mawaziri ,wakaanza kumletea picha za nguruwe ,sijui na kuchoma ngazi iliyokufikisha ulipo ,mimi yangu macho tu
Hapo naona upo kwa January
 
Ccm kila kona inaharibu zambi hii ya kuubadilisha ukwel itawatafuna
Km vijana wa uvccm wanavyokanusha lile bango la ubaguz wa rang
 
Yaliyotokea Ilala yamenikumbusha miaka kadhaa iliyopita ( na ninadhani hapo ndio neno kutia mpira kwapani lilipoanza) Timu yangu ya Simba ikiwa inacheza na Yanga ilipofika halftime ikaamua kutokurudi uwanjani.
Hakuna kitendo kiliwahi kunisononesha kama kile hadi leo, kwanini ukimbie mtanange? Sii bora ushindwe kiume kama walivyoshindwa kwa heshima kule Kinondoni?
Najua kwa Ilala walioweka kwapani mpira ni pamoja na Mbunge Zungu, nadhani huyu hata kule mjengoni kama atataka kuwania uenyekiti abwagwe tuu hafai kabisa.
Mleta mada pole sana, najua unavyojisikia kwa kitendo hicho cha kuweka mpira kwapani.
Mkuu hizi zote ni salaam tosha kuwa ccm sasa imechoka kila upande
 
Kwa hili lazima tuseme, kwamba kama mwanachama halikunifurahisha hata chembe.
Ni jambo lililo wazi kuwa baada ya uchaguzi mkuu, CCM tumepigwa bao hasa hapa jijini Dsm.

Halmashauri nyingi waliochaguliwa ni wanachama wa vyama vya upinzani kwa wingi zaidi kuliko wa chama tawala.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kiuhalisia.

Dhambi kubwa na ya kutia aibu, ni kuleta mamluki toka Zanzibar, watuamulie mambo ambayo kwanza hawayajui ya DSM, na pili si wawakilishi wa wananchi wa DSM.
Katika kata yangu, diwani alichaguliwa wa CHADEMA, mimi nilimpa kura yangu(wa CCM) alishindwa vibaya.
Kushindwa kwa huyo mwana CCM mwenzangu kunatokana na kutoshughulikia kero , hasa za barabara huku Mbezi.

Sasa leo huyu mwana CHADEMA TUTAMPIMA KWA KIGEZO HICHO HICHO.

Sasa leo tunaletewa mamluki wa kutusaidia kuamua mambo yetu?
Mbaya zaidi ni kususia uchaguzi.
Hii ni AIBU KUBWA!
Huu ni Ukurunzinza usiokubalika.
Well said mkuu.....Kuna vyama vingine wamejfanya miungu vyama.....Hili la Mamluki linatusumbua sana Arusha wamefanya wanaleta wabuge toka Tanga...! Kwa nini vyama hatukubali kushindwa?? Of all people nilitegemea Lowasa atabisha sana lakini alifika mahali akasema sawa .....Nimeshindwa. Angalia majimbo mengi wlioshinda upinzani kuna kesi mahakamani mgombea amekataaa kusaini......Why ?????
 
Kwa hili lazima tuseme, kwamba kama mwanachama halikunifurahisha hata chembe.
Ni jambo lililo wazi kuwa baada ya uchaguzi mkuu, CCM tumepigwa bao hasa hapa jijini Dsm.

Halmashauri nyingi waliochaguliwa ni wanachama wa vyama vya upinzani kwa wingi zaidi kuliko wa chama tawala.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kiuhalisia.

Dhambi kubwa na ya kutia aibu, ni kuleta mamluki toka Zanzibar, watuamulie mambo ambayo kwanza hawayajui ya DSM, na pili si wawakilishi wa wananchi wa DSM.
Katika kata yangu, diwani alichaguliwa wa CHADEMA, mimi nilimpa kura yangu(wa CCM) alishindwa vibaya.
Kushindwa kwa huyo mwana CCM mwenzangu kunatokana na kutoshughulikia kero , hasa za barabara huku Mbezi.

Sasa leo huyu mwana CHADEMA TUTAMPIMA KWA KIGEZO HICHO HICHO.

Sasa leo tunaletewa mamluki wa kutusaidia kuamua mambo yetu?
Mbaya zaidi ni kususia uchaguzi.
Hii ni AIBU KUBWA!
Huu ni Ukurunzinza usiokubalika.
Quinine ni chungu sana mdomoni lakini inatibu malaria sugu
 
Mi nafikiri ishu ya Ilala ni planned kwa maamuzi uchaguzi wa marudio Zanzibar.
mkuu hii naipinga , uhusiano wa Tanganyika na zanzibar unaingiaje hapa ? halafu zanzibar ccm imeshindwa uchaguzi , unasubiriwa muda tu maalim seif aapishwe , unaambiwa hata shein hajui kilichosababisha uchaguzi ufutwe , Anajua jecha peke yake !
 
Chama kuwachukulia hatua endapo hawatakuwa na maelezo yya kutosheleza. Waziri alitoa maelekezo, lakini kama yalipuuzwa, hilo ni suala zito sana kwa ustawi wa chama na demokrasia.
 
Vyama tawala katika Afrika vinafikiri ni dhambi kwa vyama vya upinzani kushinda uchaguzi. Ajabu ni kuwa viko tayari kutenda dhambi ili kuzuia vyama vya upinzani visiingie madarakani. Na kwa kweli mambo yanayofanya vyama vingi tawala vishinde wala si mambo mazuri. mojawapo ni ujinga wa raia na mbinu chafu. Kuna methali inasema mjinga aking'amua mwerevu yu mashakani. Unaweza kujiuliza ni kwa nini mijini wapinzani hupata kura nyingi zaidi ya chama tawala!
 
Ccm kwa hili na lile la Zanzibar wamejiaibisha sana,inaonyesha jinsi ambavyo hawamaanishi kile wanachokisema,na hawasemi kile wanachokimaanisha.Huu uongo,wizi (ref.majipu) na uzandiki wanaoufanya unawachimbia kaburi.Ccm ni ile ile,lakini wa Tanzania si wale wale,wamebadilika!Jiandaeni kisaikolojia
 
Back
Top Bottom