Kwa hili la Samatta, Serikali inafanya double standards

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Wapendwa wanajukwaa na watanzania kwa ujumla, ni dhahiri kwamba sote tunapenda kuona nchi yetu ikisonga mbele kitaifa na kimataifa katika michezo na sanaa mbalimbali. Tumeshuhudia baadhi ya vijana wetu wakifanya vinzuri kimataifa na kuiletea heshima tele nchi yetu.

Sasa pamoja na heshima hii nina jambo ambalo naliona hakika halijakaa sawa na pengine linaleta picha mbaya kwa wananchi kuanza kudhani labda ni michezo au sanaa za aina fulani tu ndizo ambazo serikali inazithamini. Ni wiki iliyopita ambapo tumeshuhudia mchezaji wa soka Mbwana Samatta akitangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika. Tumeshuhudia namna serikali ilivyomtembeza mtaani kama kumpongeza kwa tuzo aliyopata. Leo hii muda huu Vodacom na serikali wameandaa hafla ya kumpongeza kwenye Hotel ya Hyat Regend. Kwa mujibu wa posts zinazowekwa na Vodacom katika mtandao wa instagram ni kwamba Samatta amepewa zawadi na serikali pesa taslim na kiwanja huko Kigamboni. Napongeza kwa hilo ni jambo jema hasa katika kutia moyo.

Sasa hoja yangu inakuja hapa, je serikali inayatambua mafanikio ya mpira wa miguu peke yake na si sanaa zingine pia? Nasema hivi nikichukulia mfano Diamond Platinumz. Hakuna mtu asiyetambua mafanikio aliyopata Diamond katika muziki kiasi cha kuiletea heshima kubwa nchi yetu katika Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mbali na tunzo nyingi alizopata Diamond katika Afrika hii, ameweka historia ya kuwa msanii wa kwanza Afrika kushinda tunzo ya dunia inayotolewa na MTV. Ni msanii aliyewafanya waafrika na dunia kwa ujumla waanze kujifunza na kukielewa kiswahili hasa kutoka na nyimbo zake kutumia kiswahili na hata katika nyimbo anazoshirikishwa nazo anaimba kwa kiswahili. Ni msanii aliyefanya soko la mziki wa Tanzania likabadilika hasa katika suala la malipo wanayopewa wasanii katika matamasha na shoo wanazoalikwa. Ni mwanamuziki pekee wa Tanzania aliweza kuzivuta media za kimataifa kama BBC, Aljazeera na CNN kuweza kufanya naye interview.

Pamoja na mafanikio yote hayo hakuna hata kiongozi mmoja aliyediriki kumpa hongera Diamond kwa tunzo kubwa ya Dunia aliyoipata. Nimejiuliza sana na kudhani labda michezo na sanaa zinazothaminika na serikali ni mpira wa miguu tu.

vodacomsamatta.jpg


Diamond-Platnumz-EMA-e1445846769260.jpg

 
Ahsante sana kwa kuliona hili na kulisemea.
Mkuu, binafsi sijapendezwa na hizi double standard za serikali. Kiuhalisia inawavunja moyo hawa wasanii wengine kwa kuona kumbe wao hawana thamani yoyote.
 
ebu acheni ujinga daimond alikuwa anaingia ikulu jana chooni tena kabebwa sana na serikali kuliko msanii yeyeto hata sammata hajafikia alipofikia daimond tumembeba sana embu acheni hizo team zenu sijui team kiba team daimond ndizo zinazo waharibu ninyi
 
kwani dai alikuwa anaenda kufanya nini ikulu enzi za mkwere, wabongo sisi bhana wepesi kusahau
 
We jamaa bana umeandika makala ndefu nikajua kuna hoja ya maana kumbe ndo yale yale ya kina timu nani cjui anywey ni mawazo huru ila mie nazani hoja yako ungeipeleka insta kwa kina team kiba na team wema huko ndo mahala pake.
Ila hapo huna hoja ya maana
 
Hivi mzee kikwete si alikuwa mpaka promota na kumkutanisha Hugo jamaa na wasanii wengine marekani mbona huyo msanii ikulu kwake ilikuwa Kama kwenda chooni. nilidhani kuna hoja kumbe ndo huu ujinga wenu wa kufananisha vitu. Kama kuna watu walichezea Sana kuinjoi kipindi cha mkwele ni hawa wasanii maana ikulu ilikuwa sehemu ya kawaida kuingia.
 
Sasa wewe unalinganishaje mpira wa miguu na hao wakata viuno aisee. Huoni aibu?
Hapo sasa, watueleze kuna shirikisho la Muziki Africa? Au Mtu tu anakaa na kuandaa vigezo vyake akatoa tuzo kama alivyofanya James Dandu ktk Kilimanjaro awards!!! Hivi hata Okwi akichaguliwa kuwa mchezaji bora na Tff akirudi kwao Uganda apokelewe kama mfalme? Hii si sawa. Caf ni shirikisho rasmi la Mpira Africa pia ni mwanachama halali wa shirikisho la Mpira Duniani Fifa hivyo Samata anatambulika hadi Fifa kua ni Mwanasoka bora wa Africa kwa wachezaji wa ndani.

Tuacheni utani mpira unachezwa hadharani na kila mtu anaona, tena unatambulika na mashirikisho yaliyonamlaka na yamayotambulika rasmi hivyo binafsi naona ni sahihi kumpongeza Mtu aliyeshinda Olympic, Madola, Ngumi zinazotambuliwa na mashirikisho ya Kimataifa, sio Tuzo za Mashauzi Airpot!! Na muache ushabiki maandazi...
 
Watanzania ni mabingwa wa kutoa lawama..juzi hapa mlitoa lawama sana na leo bado mnaendelea kutoa lawama!
 
Last edited:
Hapo sasa, watueleze kuna shirikisho la Muziki Africa? Au Mtu tu anakaa na kuandaa vigezo vyake akatoa tuzo kama alivyofanya James Dandu ktk Kilimanjaro awards!!! Hivi hata Okwi akichaguliwa kuwa mchezaji bora na Tff akirudi kwao Uganda apokelewe kama mfalme? Hii si sawa. Caf ni shirikisho rasmi la Mpira Africa pia ni mwanachama halali wa shirikisho la Mpira Duniani Fifa hivyo Samata anatambulika hadi Fifa kua ni Mwanasoka bora wa Africa kwa wachezaji wa ndani.

Tuacheni utani mpira unachezwa hadharani na kila mtu anaona, tena unatambulika na mashirikisho yaliyonamlaka na yamayotambulika rasmi hivyo binafsi naona ni sahihi kumpongeza Mtu aliyeshinda Olympic, Madola, Ngumi zinazotambuliwa na mashirikisho ya Kimataifa, sio Tuzo za Mashauzi Airpot!! Na muache ushabiki maandazi...


Aina haja ya kuandika maelezo yote haya. Huyu mleta mada atakuwa mzaramo tu kulinganisha mpira na mziki.
 
Mwacheni huyu Sammata sasa akacheze mpira maana wabongo hamna dogo, msimtie gundu bure akaenda kukalia benchi huko anakokwenda
 
Back
Top Bottom