Kwa hili la michango kuanzishwa shuleni kinyemela, wizara ya elimu ikubali kubeba lawama

Mkuu hio ni itikadi ya kizamani,kwasasa hakuna shule zenye mafunzo mazuri kama za serikali
Serous?! Hivi hata aibu huoni wakati kila mwaka kwenye 10 bora mbovu kwa kila hatua zinajaa shule za serikali!!!
Zamani ndio tulikuwa tukiziona shule za private babkubwa na kuzidharau shule za aerikali,
Zamani ipi ambayo watu ndo walikuwa wanaziona private school bab kubwa? Binafsi hiyo zamani nilisoma private na watu walikuwa wanatuona vilaza hadi tulipoanza kuziburuza government schools ndo adabu ikatamalaki!!

Btw, unaweza kutaja shule 5 bora za serikali na mimi nitaje 5 bora za private halafu tuangalie matokeo yao?
...lkn mambo yakabadilika mimi nilimtoa shule ta private mmt wangu na kumhamishia shule ya serikali kwasbb nilishaona na kuyapima maendeleo ya masomo ya mtoto
Private za uchochoroni hizo na zimejaa kibao kuibia watu!!
Sambamba na hospitali wengi wanazidharau hospitali za rufaa na kuzithamini hospitali za private kwa mfano Aghakhan,TMJ,au Hindumandal,lkn ukizama kiundani zaidi hsptl za rufaa ndio zinawataalam wa uhakika vifaa vya kutosha navya kisasa kuliko hata hosptl za privates
Kwasasa zimebakia majina tu,lkn sio kwa huduma
Mada ni shule sio hospitali lakini kwa kukusaidia tu, watu wanajali sana private hospital kwa ajili ya huduma. Watu wangependa waende mara moja, wahudumiwe waondoke wakafanye shughuli zingine na sio siku ya mtu kwenda hospitali ndo basi tena kila kitu kisimame!!!

Hospitali inaweza kuwa na madaktari wote ambao ni maprofesa na vifaa vyenye hadhi ya platinum but what matters ni uwajibikaji wa hao wataalamu na sio vyeti vyao!!!

Unaongea siasa!!!!
 
Mwalimu unaposema watoke kama walivyoingia ina maaana hutaki kazi, na utafanya kazi tuuu endapo wanafunzi watatozwa michsngo kumbuka kwenye mkataba wako uliojaza haukukuambis kwamba wanafunzi wasipo changa usifundishe
Hivi umeelewa hoja yake?! Hoja yake ni hii:
Hata kwa maigizo haya ya Jana utaona watu wanatoka kumsifu mfalme na b/n 23.8 utafikiri zinacover kila kitu. Walimu nawashauri; kuliko kupoteza vibarua vyenu acheni watoto wetu watoke kama walivyoingia maana midomo ya kuongea bila uhalisia tunayo wengi. Ni shule gani ya kata Tanzania ina walimu wote wa PCB O-level? Walimu wakuu mkifanya ubunifu wenu mkaleta Part time hired teachers wanaolipwa kwa michango kidogo ya wazazi, wanajitokeza wapinzani miongoni mwa wazazi wanapeleka taarifa kwa "Wambea Wa Taifa" ili wapeleke wanazoita wao taarifa za siri kuonyesha nyinyi mnanyanyasa wanyonge wao. Mwalimu linda ajira yako achana na ubunifu utakukosesha mkate.
Sasa unatarajia Mwalimu wa Historia afundishe Chemistry au Fizikia?! Sasa kama watu kama nyinyi mnaleta upinzani hata kwenye mambo yenye tija; sasa matokeo yake yatakuwa nini kama sio mtoto kutoka kama alivyoingia? Au hufahamu kuna shule kadhaa za serikali wanategemea walimu wanaotokana na michango ya wazazi?!
 
Hivi umeelewa hoja yake?! Hoja yake ni hii:
Sasa unatarajia Mwalimu wa Historia afundishe Chemistry au Fizikia?! Sasa kama watu kama nyinyi mnaleta upinzani hata kwenye mambo yenye tija; sasa matokeo yake yatakuwa nini kama sio mtoto kutoka kama alivyoingia? Au hufahamu kuna shule kadhaa za serikali wanategemea walimu wanaotokana na michango ya wazazi?!
Chige una muda Wa kubishana na vilaza. Nimeshamjibu kuwa mimi sibishani naye kwa sababu wenye ufahamu wamenielewa, we achana naye huyo mtetezi Wa haki za Ikulu.
 
inabidi Dalichako na raisi watuweke wazi,maana raisi anasema hataki kusikia michango na Ndali anasema tulipe michango ya maendeleo sasa tunachoitaji kujua kwanza ni michango ipi ni ya maendelea na michango ipi sio ya maendeleo,kwa mfano pale Arushaday Arusha ili motto aanze kidato cha kwanza anatakiwa kuchangia mambo yafuatayo
1. 80,000/= ya chakula
2. 40,000/= ya uniform
3. 20,000/= rim ya karatasi
4. fagio mbili
5. ndoo ya maji ya kufanyia usafi
6. Track suit ya michezo
7. 20,000/= ya masomo ya ziada,hii ni baada ya kikao cha wazazi
8. 10,000/= kwa waalimu wa dini
9. 20,000/= kwa ajili ya madaftari 12
sasa hapo tuilezwe kati ya michango hiyo niliyoitaja ni ipi ni ya maendeleo na ipi sio ya maendeleo
 
Haya sasa... wanafunzi 300, 1 Million... wastani wa Sh.3500 kwa mwanafunzi!

Yaani unaamini kabisa TZS 3500 inatosha ku-cover capitation cost kwa mwezi mzima kwa mwanafunzi?!
Yaap 3500 per month kwa miezi 12 ni sh 42000. Haitoshi hiyo unaitaji miujiza gani tena?
 
inabidi Dalichako na raisi watuweke wazi,maana raisi anasema hataki kusikia michango na Ndali anasema tulipe michango ya maendeleo sasa tunachoitaji kujua kwanza ni michango ipi ni ya maendelea na michango ipi sio ya maendeleo,kwa mfano pale Arushaday Arusha ili motto aanze kidato cha kwanza anatakiwa kuchangia mambo yafuatayo
1. 80,000/= ya chakula
2. 40,000/= ya uniform
3. 20,000/= rim ya karatasi
4. fagio mbili
5. ndoo ya maji ya kufanyia usafi
6. Track suit ya michezo
7. 20,000/= ya masomo ya ziada,hii ni baada ya kikao cha wazazi
8. 10,000/= kwa waalimu wa dini
9. 20,000/= kwa ajili ya madaftari 12
sasa hapo tuilezwe kati ya michango hiyo niliyoitaja ni ipi ni ya maendeleo na ipi sio ya maendeleo
HUYU NI JIPU NA SIJUI KAMA ATAPONA KWA MWENENDO HUO ELFU 8O YA CHAKULA AAAAHHHH?!!!! JAMBAZI HILO
 
Kwa michango ya chakula daaah wasiingilie kwani kuna wanafunzi wanakaaa hostell kwani imesaidia kupunguza mimba mimi mwanafunzi wangu wa urambo namlipia kilo zifuatazo
MAHINDI DEBE 4.
MAHARAGE KG 23.
MCHELE KG 6.5KG.
PESA 20000 KWA AJILI YA KUWALIPA WAPISHI NA MATRONI.
GHARAMA ZOTE NI MUDA WA MIEZI 6.
 
Mkuu hio ni itikadi ya kizamani,kwasasa hakuna shule zenye mafunzo mazuri kama za serikali
Zamani ndio tulikuwa tukiziona shule za private babkubwa na kuzidharau shule za aerikali,lkn mambo yakabadilika mimi nilimtoa shule ta private mmt wangu na kumhamishia shule ya serikali kwasbb nilishaona na kuyapima maendeleo ya masomo ya mtoto
Sambamba na hospitali wengi wanazidharau hospitali za rufaa na kuzithamini hospitali za private kwa mfano Aghakhan,TMJ,au Hindumandal,lkn ukizama kiundani zaidi hsptl za rufaa ndio zinawataalam wa uhakika vifaa vya kutosha navya kisasa kuliko hata hosptl za privates
Kwasasa zimebakia majina tu,lkn sio kwa huduma
Kwenye hospital sina uzoefu sana ila, kwenye elimu rudia kufanya utafiti hasa kwa elimu ya msingi na upili.. Kumi bora kwenye matokeo huwa ni private tu.
 
Elimu bure Tanzania haiwezekani kwasasa, huko ni kuwachelewesha watoto kupata elimu, matokeo yake watajiendeleza baadae.
Kuna mambo mengi yanachangie elimu bure isifanikiwe;
1. Miundo mbinu mibovu
2 Shule kukosa waalimu
Kabla ya zuio la michango baadhi za shule zilikuwa zinachangisha wazazi pesa ndogo ili kulipa waalimu wa sayansi ambao waliajiriwa na shule kwa muda kuziba pengo.

3. Elimu bure lkn ruzuku za shule toka serikalini 50, 000/, halafu baadhi za waalimu wakuu wanazifuatilia hizo pesa kwenda kusaini halmashauri kwa gharama ya 60.000???

Tunategemea nini?
 
Mwalimu unaposema watoke kama walivyoingia ina maaana hutaki kazi, na utafanya kazi tuuu endapo wanafunzi watatozwa michsngo kumbuka kwenye mkataba wako uliojaza haukukuambis kwamba wanafunzi wasipo changa usifundishe
Umeambia utaje shule hata moja ya kata yenye walimu wa masomo hawa PCBM halafu wewe unakuja na majibu ya Kibashite.. Then unajiita msomi.
 
Michango mashuleni kimsingi haikwepeki,serikali inapeleka fedha ila hazikidhi mahitaji mfano shule inapata mgao wa capitation grant 42000 kwa mwezi ww km ndiyo mwl unamlipaje mlinzi,mitihani,ukarabati,michezo,vifaa vya kufundushia na kujifunzia,posho za nauli,na mambo mengine madogo madogo.Hapa ndipo wazazi pamoja na umasikini wao wakaamua tuchangie ili tutatue baadhi ya changamoto. Hivi karibuni kulikuwa na semina inayohusu utunzaji wa fedha za serikali kwa njia ya mfumo FFARS kila taasisi ilitoa watumishi wawili na mafunzo siku tatu kwa maelezo yaliyotolewa posho zilipwe kutoka mfuko wa shule jee unalipaje kwa gawio la kila mwezi 42000?
Tatizo ni kujipendekeza kwa wakuu wa shule na roho za upigaji walizo nazo kwa nn wasifanye yale yaliyondani ya uwezo wao kulingana na bajeti walizonazo.
 
Hii ishu ni simple sana, kwa wale ambao tumesoma elimu ya zamani hasa shule za vijijini tulikuwa tunatoka saa 10:30 jioni na mambo yanaenda sawa tu.

Tulikuwa na break ya saa 4 na tulikuwa na break kubwa kuanzia saa 6:30 - 8:00 mchana kwa ajiri ya kwenda kula kisha tunaondoka majumbani saa 10:30 jioni. Sasa sijui huu ubishano ni wa nini, kama ni kula si watoto warudi makwao wale huko huko? kama pesa ni kwa ajiri ya kula, basi waachwe wakale majumbani kwao kisha warudi saa 8 mchana shuleni
 
Yaap 3500 per month kwa miezi 12 ni sh 42000. Haitoshi hiyo unaitaji miujiza gani tena?
Trust me, you're very funny! Issue iko hivi! Kwa hizo hoja zako hata 1,000 "inatosha" kwa sababu "sio lazima" kufanya test. "Sio lazima" kuchapisha mitihani. Sio lazima kwa mambo mengi tu na kwa staili hiyo hata jero inatosha!!
 
Mimi ni miongoni mwa wazazi niliewatolea nje walimu swala la mchango na walini mind saaana pia walijaribu kuwatumia wazazi wenzangu kunishawishi lkn nilikataa katakata
Leo wameyakuta sasa.nachompendea rais wetu anayafukunyua mambo ya chini kabisa na kuyaweka bayana hadharani ambayo kwa kiongozi mwingine atayapuuza tu na kuchukukia ni jambo dogo tu,hali yakuwa mambo kama hayo ndio yanayotuumiza saaana watu wa chini
Maumivu yake wanayafahamu watoa michango
WEWE UNATAKA MWANAO APATE BORA ELIMU NA SIO ELIMU BORA
 
nionavyo mimi hatuna haja ya kubishana, wazazi kaeni na walimu wawaeleze bajeti zao na matatizo yao yote, mkimaliza hapo ulizeni TAMISEMI mnaleta shilingi ngapi hapa shuleni? jibu mtakalopewa litawaongoza kuamua
 
Ni ishu ndogo tu hapa, walimu wajitoe kabisa na michango ya wanafunzi. Mzazi ajue mwanafunzi wake atakula wapi baasi! Mwalimu kama chaki zimeisha toa lecture tu.
Elimu bure aliiweza baba wa taifa maana wakati ule hata madaftari tuliyapata shuleni, hawa wengine wanaoimba uzarendo sijui nini hamna kitu wabwabwaja siasa tu.
Enzi zetu hizo. Daftari likiisha mwalimu analichana kidogo anakupa jingine. Siasa imeingia sana kwenye elimu na hao wanaoitwa wanyonge watazidi kunyongwa tu kwa kukosa Elimu
 
Ukiona hivyo basi ujue changamoto ni nyingi zaidi..! Nawaonea huruma sana wazazi wanaochukua maneno ya wanasiasa kama chiriku..! Pesa inayotoa serikali haitoshi..! Niliwahi kumtembelea mkuu wa shule yangu ya sekondari niliyosoma miaka kadhaa iliyopita (jina kapuni), mwalimu alinionyesha matumizi na gawio la serikali kuu, unaweza kulia..! Maana matumizi ni mengi na pesa wanayopewa ni kiduchu..! Wakati huo huo serikali inawaban walimu wafaulishe na miundombinu ni mibovu unategemea nn??

Ukiwaambia wazazi wanaojua umuhimu wa elimu lazima wataliongelea kwa wazazi wengine and so watatafuta solution.. Sasa kama wewe pesa huna or unaona walimu wanajaa sana basi usitoe.. Na sio unakuja huku kusnitch wazazi wenzio wenye uchungu na watoto wao..! Au ungeenda kwa mwalimh mkuu, ukamuomba data zote za matumizi na gawio wanalopewa, then baada ya kuangalia ndo ungetoa neno lisilo na bias..!
Mi huwa kila mara huwa najiuliza, inawezekanaje kwa mtu mzima, mwenye uwezo wa kununua simu tena smartphone na kuitumia, tena ni mwenye kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Jf, inawezekana walau Ameshafikia levo ya vidato kadhaa kama si chuo na awards anazo, lakini bado tu, hajui maana ya elimu wala umuhimu wake.

Hili si swala la kiitikadi wala mavyama, hili ni swala nambari moja kwa umuhimu na mustakabali chanya wa taifa letu. Ukiua elimu umeliua taifa lote.

Kiukweli, hii sekta ina changamoto nyingi sana, kiasi kwamba serikali pekee, itaichukua milongo kadhaa kulimaliza. Fedha zitolewazo si chochote, mwaka huu, watoto wengi wanakaa chini, tena mpaka ktk shule za sekondari.

Madarasa hayatoshi, na kwa shule nyingi, yanahitajika zaidi ya mara tatu ya yale yaliopo. Shule hazina ofisi, hazina nyumba za walimu, hazina walimu wa kutosha haswa kwa masomo ya sayansi hawapo kabisa, walimu huwatumia wazazi kuchangia ili wawalipe walimu walio nje ya ajira, ni viposho tu.

Lini shule zetu zulikamilika bila kuwepo kwa changamoto hizi? Kwa mzazi mwenye kujitambua, lazima ahamasishe wenzake kusaidia kuzitatua hizi changamoto kwa manufaa ya watoto wake.

Hivi majuzi tu, kuna post ilikuwa ikisambazwa kwenye ma group ya whatsapp, shule zenye gharama kubwa nchini, kuna shule imelenji milioni 42, hawa watoto hawatakwenda kuishi Mwezini ama Pluto, ni hapa hapa Tanzania, na wata compite na wanetu watokao kwenye hii elimu bure yetu yenye changamoto lukuki. Life is a race!
 
Back
Top Bottom